200 Wakamatwa Kariakoo kwa Uzembe na Uzururaji

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Nilikuwa naangalia mlimani tv, watu zaidi ya 200 wamekamatwa na jeshi la polisi katika eneo la kariakoo kwa kosa la uzembe na uzururaji.

Muda mrefu sijasikia watu wakikamatwa kwa makosa ya uzembe na uzuraraji. Isijekuwa polisi wameshindwa kukamata majambazi na wahalifu sugu
na sasa wameamua kuwaumiza wamachinga!
 
Samahani, hivi ni vigezo gani vinavyotumika kumtambua Mtu kwamba ni mzembe au mzururaji?....ninawasiwasi wa uonevu katika utekelezaji wa sheria hii.
 
kariakoo kuna wazururaji?
Wamejiridhisha vipi kuwa hao ni wazururaji?
Wametumia vigezo gani?
 
kariakoo kuna wazururaji?
Wamejiridhisha vipi kuwa hao ni wazururaji?
Wametumia vigezo gani?

Mimi nafahamu kariakoo shughuli zinafanyika 24/7 sasa niliposikia kuna watu wanashitakiwa kwamba ni wazembe na wazururaji nimeshindwa kuelewa!
 
wamezembea nini? wamezurura wapi? ilikuwa wawe wapi that time wanakamatwa? ilikuwa wawe wanafanya nini muda huo na wakawa hawafanyi!!!!!!!!

Jogi umenena vyema mkuu,nilipoiona hiyo taarifa kwenye TV nilishituka kidogo nikajiuliza ni cliteria gani ilitumika na maswali uliyouliza hasa ndio key tools ku-identify uzembe wao na uzurulaji wao,najiuliza watakwenda kuwalaza wapi,je kuna chakula walichowaandalia?je wana utaratibu wa emergence ya tiba in case wengineo wakiugua?
Anyway ndio CCM yenye maisha bora
 
wamezembea nini? wamezurura wapi? ilikuwa wawe wapi that time wanakamatwa? ilikuwa wawe wanafanya nini muda huo na wakawa hawafanyi!!!!!!!!

Haya ni maswali muhimu sana na yanapaswa kujibiwa na jeshi la polisi wanatumia vigezo gani kuwatambua wazembe na wazururaji.
Labda kama kuna mwanasheria hapa anaweza kutusaidia ufafanuzi wa sheria hiyo.
 
hahahahahahaaaa......aseee...kuzurura maana yake ni nini?
Mimi ninavyojua, watoto wadogo wasioweza kufanya maamuzi na vichaa ndio huwa wanazurura.
Mtu mzima ametoka kisukulu asubuhi, ameenda kupanda daladala kwa nauli kubwa tu, halafu unamkuta kariakoo unamwambia anazurura????!!!

Pumbafu kabisa!
 
ooooh! usikute ni wale vijana wetu waliobeba bahasha zao za kaki za A4 zilizosheheni vyeti vya sekondari na vyuo pamoja na cv wakijaribu kwenda kwa wachina kuomba vibarua, ndo wapo wengi sana mtaani.
 
Back
Top Bottom