20 Percent

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Jamani huyu kaka mie ananivutia sana na nyimbo zake. Havumi lakini wamo

Nasikiliza Ya nini malumbano!!

Ya nini malumbano, ya nini maneno
najiweka pembeni naepusha msongamano
Bora nitulie, ningoje changu na mie
Mola nijalie haya yasijirudie

Nenda nenda hata kama zamani nilipenda!
 
Jamani huyu kaka mie ananivutia sana na nyimbo zake. Havumi lakini wamo

Nasikiliza Ya nini malumbano!!

Ya nini malumbano, ya nini maneno
najiweka pembeni naepusha msongamano
Bora nitulie, ningoje changu na mie
Mola nijalie haya yasijirudie

Nenda nenda hata kama zamani nilipenda!

Mama unasikiliza clouds nini?
 
20% kwa hapa Bongo ni kipaji ambacho kimefichwa na wenye dhamana wenye upofu, unaposikiliza nyimbo zake hakika huyu kijana anastahili shahada ya heshima, sikiliza wimbo kama Money money, Neema na mwingine wa msichana mwenye penzi la pesa pekee.

Nafurahi mdau umeweza kuleta taarifa hii humu
 
hivyo visenti kidogoo pokeaaaaa
nimemtuma bashiiri akuleteeeeeee
na vinepi vya mtoto pokeaaaaaaa
usijali nitarudi pokeaaaaaaaaaaaa
najua watoto hawamjui babaaaaa
............................
 
hivyo visenti kidogoo pokeaaaaa
nimemtuma bashiiri akuleteeeeeee
na vinepi vya mtoto pokeaaaaaaa
usijali nitarudi pokeaaaaaaaaaaaa
najua watoto hawamjui babaaaaa
............................

so sad, lakini ndoi mashairi walau yameenda shule...kipaji kweli hiki lakini kama hawezi kuhonga maDJ ndoivo wanampotezea tu mpwa
 
kuna ngoma kali sana aliitoa 2008 na bushoke; ile ya "mtoto tulia"

mnaikumbukaa? to me that was the best shot!!!

halafu akapiga maisha ya bongo
 
kipaji halisi
tatizo muziki wa bongo umetawaliwa na mabitozi...
bila kuwa bitozi mwenzao huwezi shine.
 
we ndo umesema kweli yaani huyu kijana basi tu! Angekuwa Bitoz tungekuwa na Chameleon wetu

yaani huyo 20 percent
ana kipaji cha kuandika nyimbo.
na nyimbo zake zinawagusa watu wa mjini
mpaka vijijini
ni bonge la biashara.
lakini mabitozi wa muziki wa bongo hawaelewi.
 
20% percent ni mwanamuziki kwani anajua sana kutunga na nyimbo zake zote zina ujumbe mkali. Unakumbuka ile ya Bangi, yeye anaita Bange na Mama Neema. Lakini nahisi msuba unamchanganya sana.

Kuna mwaka sikumbukini upi alikuwa anahojiwa na Gen. Ulimwengu Channel 10, Gen alivofunga kipindi jamaa si akanyayuka na kuanza kuondoka kabala ya camera kuzimwa au kuweka matangazo-aliniacha hoi sana huyu kijana wangu wa chanika
 
kuna ngoma kali sana aliitoa 2008 na bushoke; ile ya "mtoto tulia"

mnaikumbukaa? to me that was the best shot!!!

halafu akapiga maisha ya bongo
.
Ebwanaee! Hiyo ngoma imekwenda shule, lakini ndio hivyo tena wanambania
 
MJ1, kweli huyu dogo makini

amekuja na movie inayohusu nyimbo zake... musical ya kibongo nadhani

the clouds review was good and it seems its a movie to watch... tumsapoti huyu jamaa afike mbali
 
.washikaji waliniambia kwamba demu nikiruka njia
nilidhani wamepanga kunikandia mie nakupuuzia
chezo lilipoanza si akaniaga anakwenda mwanzaa
ile kurudi nakuta kidume kimejalaza ghetooooooo

Dogo yupo juu ila ndo hivyo tena Bongo kubaniana ..afu hyu dogo kweli jani linamchanganya sometimes
 
Simsikii kabisa siku hizi jamani.....
Yuko wapi siku hizi Abasi Kisinza aka 20 Percent???
 
Moyo moyo tamaaa
Moyo sifa yake kutamani
Unatamani kuzaa
Wakati bado upo shuleni
Tumia akili kukataza
Kabla ujawa matatizoni
 
Ukivumilia mbeele kweupe, ukivumilia mbele kweupe! .....kama unaishi shamba, wewe tambua ya kwamba, umezungukwa na mamba, vifaru, chui na simba...., hapa anawaasa vijana wawe wavumilivu, hasa wanafunzi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom