2.5TRILLION BILA MAFANIKIO!HUU NI UFISADI au DHARAU? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2.5TRILLION BILA MAFANIKIO!HUU NI UFISADI au DHARAU?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchaichai, Jun 13, 2012.

 1. m

  mchaichai JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 650
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mabilioni ya elimu yateketea, watoto bado hawajui kusoma [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 12 June 2012 11:31 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]
  Fredy Azzah
  RIPOTI ya utafiti, iliyotolewa na Shirika huru la Uingereza la Independent Commission for Aid Impact (ICAI), imeeleza kwamba msaada unaotolewa na Serikali ya nchi hiyo kwa Tanzania, umechangia kuporomosha kiwango cha elimu katika nchi hizo.

  Mbali na Tanzania, ripoti hiyo pia imesema misaada hiyo imechangia kuporomosha elimu kwa nchi za Ethiopia na Rwanda.

  Ripoti hiyo ina kichwa cha habari, DFID’s Education Programmes in Three East African Countries, inasema msaada wa Paundi bilioni moja sawa na Sh2.5 trilioni uliotolewa ndani ya miaka 10, lakini haujazisaidia nchi hizo badala yake watoto wamekuwa wakihitimu elimu ya msingi bila kuwa na msingi wa kusoma, kuandika na kuhesabu.

  Kwa mjibu wa ripoti hiyo, Tanzania ni nchi ya pili ambayo inapewa misaada hiyo, Ethiopia inaongoza na Rwanda ni ya mwisho.

  Ripoti hiyo inafafanua kwamba kufikia mwaka 2014/ 15, Tanzania itakuwa inapokea Paundi 60 milioni kwa ajili ya bajeti yake, Ethiopia itakuwa ikipokea Paundi 100 milioni na Rwanda Paundi 20 milioni.

  Takwimu hizo zinaonyesha fedha zinazotolewa kwa Rwanda zinapungua, lakini Tanzania na Ethiopia kinapanda kwa kasi kila mwaka.

  Inaonyesha pia mwaka 2011/12 Tanzania ilipokea Paundi 44 milioni na asilimia 94 zilielekezwa kwenye sekta nyingine na kusaidia bajeti ya Serikali na asilimia sita pekee ilipelekwa kwenye elimu.
  Ethiopia ilipewa Paundi 61 milioni na asilimia 51 zilienda kusaidia bajeti ya Serikali, asilimia 45 ilipelekwa kuboresha elimu na maeneo mengine asilimia nne.

  Pia inasema Rwanda ilipokea Paundi 24 milioni kwa ajili ya sekta ya elimu na asilimia 98 ilielekezwa kusaidia bajeti ya Serikali wakati asilimia 1.5 kwa ajili ya shughuli za utafiti.

  Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, kati ya mwaka 2002 na 2003 Tanzania ilipata takribani dola 280 milioni za Marekani kwa ajili ya elimu wakati Ethiopia ilipewa takribani dola 90 milioni za Marekani, Rwanda ni ya mwisho na ilipewa dola 60 milioni za Marekani.

  Pia katika mwaka 2007, Tanzania ilipewa wastani wa dola270 milioni za Marekani, Ethiopia dola 330 za Marekani na Rwanda dola 90 za Marekani na mwaka 2008, Tanzania ikipokea takribani dola 200 milioni za Marekani, Ethiopia dola 230 milioni za Marekani na Rwanda dola 100 milioni za Marekani.

  Uchunguzi umeonyesha kwamba watoto zaidi ya 52 milioni, wanapata elimu kwa sababu ya msaada huo, huku walimu wasio na sifa ya ualimu wakiajiriwa kukabiliana na ongezeko hilo la wanafunzi.

  Kutokana na hali hiyo, ripoti hiyo inailaumu Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DfiD) kwa kushindwa kufuatilia kama wanafunzi wanajifunza au la.

  “Kiwango cha elimu ambacho kimekuwa kikitolewa katika hizi nchi tatu, ni cha chini kwa kuwa kinapunguza thamani ya matokeo ya maendeleo kinyume na DfiD’s ilivyokuwa ikitarajiwa,” inasema ripoti hiyo.

  Pamoja na hayo ripoti hiyo ilishindwa kuainisha kama DfiD ilifuatilia kama walimu na wanafunzi walikuwa wakiingia darasani.

  “Watoto wengi kujiunga na elimu ya msingi, huku wengi wakiitimu elimu hiyo bila kuwa na msingi wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, kwa maoni yetu ni matokeo ya matumizi mabaya ya fedha zetu,” inaeleza ripoti hiyo.

  Katika kipindi cha mwaka 2005/2015, msaada wa DfiD kwa nchi hizo tatu, unatarajiwa kuwa paundi bilioni moja kwa ajili ya kusaidia bajeti za nchi hizo.

  Katika hatua nyingine ili kukabiliana na hali hiyo, ripoti hiyo inasema mambo kadhaa yanatakiwa kufanyika kwa lengo la kuzisaidia wizara za elimu kukabiliana na tatizo la walimu kutembea umbali mrefu kwenda kuchukua mishahara na kucheleweshewa fedha za ruzuku shuleni.

  Ripoti hiyo inashauri unapaswa kufanyika mara kwa mara ili kukabiliana na vitendo vya rushwa na ukiritimba.

  Kwa upande wa rushwa ripoti hiyo inaonyesha kuwa Tanzania kuna tatizo kubwa la rushwa kutokana na walimu wengi waliofariki dunia kulipwa mishahara.

  Ripoti hiyo inaweka wazi kwamba tatizo lingine ni fedha zinazotolewa sekta ya elimu kutofika shuleni kama ilivyopangwa.

  Kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali ili kufikia lengo la milenia la kuhakikisha ifikapo mwaka 2015, watoto wote wanaweza kuhitimu shule ya msingi.

  Ripoti hiyo inaanisha kwamba, katika kipindi cha mwaka 2010/ 11, elimu imekuwa ni sehemu kubwa ya misaada inayotolewa na DFiD's na mpaka kufikia mwaka 2014, itakuwa ndiyo eneo kubwa zaidi linalopewa fedha.

  Ripoti hiyo iliishauri DFiD kuangalia upya vipaumbele vyake ili ubora wa elimu inayolewa iwe moja ya ajenda zake muhimu katika kutoa misaada yake kwenye elimu katika nchi hizo.

  Malcolm Bruce ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya maendeleo ya kimataifa ya bunge la nchi hiyo limeshauri msaada huo uendelee kutolewa kutokana matatizo hayo.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mfunzi ya Ufundi Philipo Mulugo anasema taarifa alizopokea katika mikoa mbalimbali zinaonyesha kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, hawajui kusoma wala kuandika.

  Wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana walikuwa 983,545, waliofaulu ni 567,567. Kati yao wasichana walikuwa 278,377 sawa na asilimia 54.48 na wavulana walikuwa 289,190 sawa na asilimia 62.49.

  Ripoti ya asasi isiyokuwa ya kiserikali ya mwaka 2010 iliyokuwa na kicha cha habari, Je, watoto wetu wanajifunza?,

  inabainisha baada ya ada za shule kufutwa mwaka 2001, uandikishaji wa watoto, uliongezeka kwa asilimia 70 mpaka asilimia 110.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Bure Ghali...!!!
   
Loading...