1st April fools Day, 2013: Tahadhari - Leo ni siku ya wajinga kuweni makini

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,220
1,665
April 1, 2013 – Tahadhari wadau “wanaJF” leo ni siku ya wajinga dunia, kuweni makini na matapeli.
Kuna uwezekano wa kuwepo topic na mambo mengi ya kipuuzi na uzushi kwa siku ya leo ya Jumatatu ya Pasaka.
 
April 1, 2013 – Tahadhari wadau “wanaJF” leo ni siku ya wajinga dunia, kuweni makini na matapeli.
Kuna uwezekano wa kuwepo topic na mambo mengi ya kipuuzi na uzushi kwa siku ya leo ya Jumatatu ya Pasaka.

Isije ikawa kama hii hapa!
APIGWA FAINI KWA KUITA ZIMA MOTO SIKUYA WAJINGA
Mkazi mmoja wa eneo la Mikanjuni jijini Tanga alipigwa faini shilingi laki tano kwa kutoa taarifa ya uongo kuhusutukio la moto katika eneo lake.
Tukio hili lilitokea miakamiwili iliyopita kwa mujibu wa mchangiaji mmoja kwenye redio Nuur FM 94.5 ya jijini hapa.
Mchangiaji huyo alikuwa akitoa mawazo yake baada ya nasaha za sheikh Mohammed Abbas aliyekuwa akitahadharisha juu ya ubaya wa waislamu kushiriki katika matendo ya siku ya wajinga duniani maarufu kama Aprilfool.
Baada ya kupokea simu magari kadhaa ya kikosi cha zimamoto yaliongozana mpaka eneo lilitajwa na mpiga simu.Walipofika ikabidi magari yazunguke kuangalia sehemu yoyote yenye dalilil ya kuungua mpaka walipogundua baadae kuwa ilikuwa ni moja yasherehe za siku ya wajinga.
Kwa ushirikiano wa kikosi hicho na mashirika ya simu mtu huyo alikamatwa na kupelekwa mahakamaniambapo alipigwa faini ya shi.laki tano."Ni nani mjinga hapo?" aliuliza msikilizaji na mchangiajihuyo.
Katika mawaidha yake sheikh Mohammed Abbas aliwataka waislamu wawache kujiingiza kwenye matendo ya siku hii kwani yanakwenda kinyume na mafundisho ya uislamu yanayomtakamuislamu daima awe mkweli na awache kuigamambo ambayo hayatokani na mafundisho ya Mtume swalaLlaahu alayhi wa sallam. Hapo juzi katika kipindi cha kidokezo cha redio Imani ya Morogoro kilichojadili suala hili hilila siku ya wajinga msikilizaji mwengine kutoka Zanzibar alieleza kwamba miaka kadhaa iliyopita Radio ya serikali ya Zanzibar-Sauti ya Zanzibar iliwahikutoa tangazo la kuwaita watu kupokea mchele wa bure kituoni hapo.Watu walipofika wakakuta hakukua na mchele wowote uliokuwa ukitolewa bali wakajulishwa kuwa ilikuwa ni utani tu wa siku ya wajinga .Hata hivyo msikilizaji huyo hakufafanua jinsi tangazo hilo lilivyofika na kutangazwa redioni hapo.
Islamic Calendar Tides © 2011 . All rights reserved.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom