1995: Siku Jakaya Kikwete alivyomuinua kitini Rais mstaafu Nyerere

Najiuliza why upendo huu haupo tena ndani ya ccm kiasi chuki nikali Sana
Huo si upendo tu.

Kikwete was playing a Machiavellian power move.

Angefanya tofauti pale, ungekuwa ndiyo mwisho wake wa kisiasa.

Kwa nini leo watu hawafanyi hivyo?

Hakuna sauti yenye nguvu ya mtu kama Nyerere kumzima yeyote anayeleta fyokofyoko.

Hata huyo Magufuli watu wamemuona alivyokuja mjini na wana faili lake. Pia vyama vya upinzani vimeongeza ushawishi na vinasubiri wanachama maarufu waondoke CCM kama fisi anayesubiri mkono wa mtu uanguke.

Zamani kulikuwa na uongozi ambao uliweza kushawishi watu kwamba unajali. Leo tunaona kabisa siasa zimezidi maadili. Maji yamezidi unga, ugali uko mashakani kuwa uji

Zamani viongozi waliandaliwa kimaadili na kisiasa. Kikwete alipikwa na kuandaliwa. Kafanya kazi za chama level ya mkoa na hata chini zaidi. Kawa kamisaa wa chama jeshini. Anajua kwamba kanuni za vita haziruhusu jeshi lianzishe vita ambayo haliwezi kushinda.

Alifanya kitu kinaitwa "tactical retreat" jeshini. Move za Shaka Zulu hizo. Anarudi nyuma kama kapigwa, kisha anakuzunguka, anakupiga vizuri sana.

Siku hizi wanasiasa wanatumia nguvu zaidi ya akili, hisia zaidi ya mkakati, ubabe zaidi ya ushawishi.

Zamani, viongozi walikuwa wanaamini zaidi itikadi za chama na habari za kumaliza matatizo ya nchi. Waliheshimu kazi zaidi ya leo. Si kwa 100%, lakini zaidi sana ya leo.

Leo viongozi wote washaona uongozi ni sehemu ya kupiga ma deal tu. Hata hao wanaojinadi kuongoza vita dhidi ya rushwa, wananunua ndege bila tender wala auditing. Unaona hapa wakifqnya upigaji hata hatujui, watasema vipi wanapinga rushwa?

Sasa ukifananisha uongozi wa mtu kama Nyerere na uongozi wa sasa, utaona kabisa uongozi wa sasa unatumia vitisho zaidi ya kutumia heshima ya uongozi.

Zamani si kwamba hakukuwa na migongano kati ya viongozi. Ilikuwapo.Ila viongozi waliweza kuimaliza kwenye vikao vya ndani.

Siku hizi zinapigwa wazi wazi.

Na ukielewa hapo, utaelewa kwa nini kuna migongano sana siku hizi.
 
Ohh hivi utamaduni huu ulioasisiwa miaka hiyo .
Kwenu wana CCM wenye tamaa ya madraka mnauelewa?mnaushi?MNA udumisha?MNA uamini?au nyinyi ni akina tamaa mbere na adui rushwa huufunika utamaduni huu?
 
Back
Top Bottom