1995: Siku Jakaya Kikwete alivyomuinua kitini Rais mstaafu Nyerere

Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
17,062
2,000
..EL alitapeliwa na JK.

..ilipofika kwenye suala la Richmond JK hakumpa support EL.

..na EL alipoondoka serikalini wanasema alikuwa depressed akaanza kunywa pombe kupindukia na kuathiri afya yake.

..kundi la Samuel Sitta, Harrison Mwakyembe, etc ndilo lililozima ndoto za Uraisi za EL.

..JK alipaswa kulishughulikia kundi hilo ili aweze kumlinda mwenzie na kutimiza ahadi walizowekeana na EL.

..nakubaliana na wewe 100% kwamba Uraisi siyo jambo rahisi. Unahitaji uwe na bahati kwelikweli.

NB:

..siyo kama namfagilia EL, ila nilitaka kueleza kilichotokea ndani ya ccm.

Utu uzima dawa. Tuna mengi ya kuendelea kujifunza
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,480
2,000
Najiuliza why upendo huu haupo tena ndani ya ccm kiasi chuki nikali Sana
Huo si upendo tu.

Kikwete was playing a Machiavellian power move.

Angefanya tofauti pale, ungekuwa ndiyo mwisho wake wa kisiasa.

Kwa nini leo watu hawafanyi hivyo?

Hakuna sauti yenye nguvu ya mtu kama Nyerere kumzima yeyote anayeleta fyokofyoko.

Hata huyo Magufuli watu wamemuona alivyokuja mjini na wana faili lake. Pia vyama vya upinzani vimeongeza ushawishi na vinasubiri wanachama maarufu waondoke CCM kama fisi anayesubiri mkono wa mtu uanguke.

Zamani kulikuwa na uongozi ambao uliweza kushawishi watu kwamba unajali. Leo tunaona kabisa siasa zimezidi maadili. Maji yamezidi unga, ugali uko mashakani kuwa uji

Zamani viongozi waliandaliwa kimaadili na kisiasa. Kikwete alipikwa na kuandaliwa. Kafanya kazi za chama level ya mkoa na hata chini zaidi. Kawa kamisaa wa chama jeshini. Anajua kwamba kanuni za vita haziruhusu jeshi lianzishe vita ambayo haliwezi kushinda.

Alifanya kitu kinaitwa "tactical retreat" jeshini. Move za Shaka Zulu hizo. Anarudi nyuma kama kapigwa, kisha anakuzunguka, anakupiga vizuri sana.

Siku hizi wanasiasa wanatumia nguvu zaidi ya akili, hisia zaidi ya mkakati, ubabe zaidi ya ushawishi.

Zamani, viongozi walikuwa wanaamini zaidi itikadi za chama na habari za kumaliza matatizo ya nchi. Waliheshimu kazi zaidi ya leo. Si kwa 100%, lakini zaidi sana ya leo.

Leo viongozi wote washaona uongozi ni sehemu ya kupiga ma deal tu. Hata hao wanaojinadi kuongoza vita dhidi ya rushwa, wananunua ndege bila tender wala auditing. Unaona hapa wakifqnya upigaji hata hatujui, watasema vipi wanapinga rushwa?

Sasa ukifananisha uongozi wa mtu kama Nyerere na uongozi wa sasa, utaona kabisa uongozi wa sasa unatumia vitisho zaidi ya kutumia heshima ya uongozi.

Zamani si kwamba hakukuwa na migongano kati ya viongozi. Ilikuwapo.Ila viongozi waliweza kuimaliza kwenye vikao vya ndani.

Siku hizi zinapigwa wazi wazi.

Na ukielewa hapo, utaelewa kwa nini kuna migongano sana siku hizi.
 

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
304
250
Ohh hivi utamaduni huu ulioasisiwa miaka hiyo .
Kwenu wana CCM wenye tamaa ya madraka mnauelewa?mnaushi?MNA udumisha?MNA uamini?au nyinyi ni akina tamaa mbere na adui rushwa huufunika utamaduni huu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom