1995: Siku Jakaya Kikwete alivyomuinua kitini Rais mstaafu Nyerere

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Magnanimous and graceful oratory.

A senseful humility that propelled him into greater heights.
What surprised me is how close he almost became the nominee.

He only lost to Mkapa by less than 100 votes.

It was a fierce battle to the end.

It was said Nyerere put his thumb on the scales to get Mkapa across the finish line.
 
Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
12,872
2,000
CCM ni genge la uhuni, hakuna jema lolote lilifanyikwa kupitia CCM.

Acha watukuzane wao kwa wao.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
52,914
2,000
What surprised me is how close he almost became the nominee.

He only lost to Mkapa by less than 100 votes.

It was a fierce battle to the end.

It was said Nyerere put his thumb on the scales to get Mkapa across the finish line.
Nyerere changed the rules of he game, during the game. To support Mkapa.

But Mkapa, in his book, says Nyerere's first choice was Salim. Salim was slacking.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,833
2,000
What surprised me is how close he almost became the nominee.

He only lost to Mkapa by less than 100 votes.

It was a fierce battle to the end.

It was said Nyerere put his thumb on the scales to get Mkapa across the finish line.
Nyerere aliingilia kati, ndiyo maana alinyanyuka baada ya hotuba ya Kikwete .
Alifahamu CCM itapata mpasuko kama Kikwete atakuwa na grudge.
Alijua kumuuza Mkapa kama 'kijana mpendwa namba 2 ni kazi'' kubwa hasa baada ya vyama vingi.

kijana namba 1 alikuwa Salim, tatizo lake alipingwa na Wazanzibar! Nyerere alijua litaleta shida katika muungano.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Nyerere aliingilia kati, ndiyo maana alinyanyuka baada ya hotuba ya Kikwete .
Alifahamu CCM itapata mpasuko kama Kikwete atakuwa na grudge.
Alijua kumuuza Mkapa kama 'kijana mpendwa namba 2 ni kazi'' kubwa hasa baada ya vyama vingi.

kijana namba 1 alikuwa Salim, tatizo lake alipingwa na Wazanzibar! Nyerere alijua litaleta shida katika muungano.
Tatizo la Mkapa nadhani lilikuwa ni kukosa charisma.

Uwezo wa kuwa Rais alikuwa nao.

Ila ikija kwenye ku connect na wananchi, hakuwa kabisa na uwezo huo, for whatever reason.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,833
2,000
Tatizo la Mkapa nadhani lilikuwa ni kukosa charisma.
Uwezo wa kuwa Rais alikuwa nao.
Ila ikija kwenye ku connect na wananchi, hakuwa kabisa na uwezo huo, for whatever reason.
Katika hilo la Charisma Hayati Mkapa hakuwa nalo hata kidogo.
Watu waliofanya naye kazi wanamtambua kwa umakini na umahiri, lakini hawamkubali kwasababu tu ya charisma.
Nyerere alijua Mkapa alikuwa right candidate na kijana aliyemuandaa.
Hata hivyo, alijua pia ni ngumu sana kumuuza kwasababu hana Charisma kama ya Salim Ahmed Salim.

Alipokuwa Rais bado tatizo la charisma lilimfuata.
Mkapa alirekebisha sana uchumi na kuinua sana kada 'ya chini kuwa ya kati''.
Watu hawa appreciate kwasababu tu ya charisma.

Katika Diplomasia ya kimataifa hasa viongozi wa Afrika, Mkapa alikuwa anaogopwa, lakini si kwa charisma.

Wenyewe walikuwa wanamwita administrator kuliko politician.

Kutokana na kukosa charisma, Mauaji ya Zanzibar yamemfanya aonekane mbaya licha ya kusimama na kuomba msamaha. Ni viongozi wachache sana wanafanya hivyo.

Tofauti na Mkapa, CD Msuya ana 'moderate charisma'' lakini anasaidiwa sana na ''personality''
Charisma ipo ni kwa Dr Salim!
 
Mtyela Kasanda

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
385
1,000
Kutoka mwaka 1995. Baada ya mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.

Akiwa anatoa hotuba ya kukubali matokeo, Rais mstaafu Kikwete aliongea maneno ambayo yalionekana kumgusa kwa furaha Rais mstaafu Nyerere hadi akanyanyuka na kuanza kupiga makofi huku akitabasamu.

Jionee mwenyewe jinsi mambo yalivyokuwa.

MAELEZO KUHUSU VIDEO
Kikwete alitoa kauli ya kumuunga mkono Rais Mteule wa CCM wa kipindi hiko, ambaye alikuwa Benjamini William Mkapa, na akataka mashabiki wake wakubaliane na hilo kwa kuwa uchaguzi(Wa ndani) umeshaisha.

Aidha aliposema kuwa kamati yake ya kampeni na kamati zote zisiszo rasmi kwa wakati huo akazitaka ziwe ni kamati za Mkapa, ndipo watu wakapiga makofi akiwemo Hayati Julius Kambarage Nyerere
Ndio siku hiyo makundi yalianza CCM. Ila bahati nzuri yalipunguzwa mwaka 2000
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
52,914
2,000
Tatizo la Mkapa nadhani lilikuwa ni kukosa charisma.

Uwezo wa kuwa Rais alikuwa nao.

Ila ikija kwenye ku connect na wananchi, hakuwa kabisa na uwezo huo, for whatever reason.
Mkapa alikuwa bonge la mbabe na disciplinarian.

Tulivyokuwa wadogo, kaka mmoja wa kwa Mkapa alikuwa analalamika nyumbani mshua alikuwa anapiga mkwala, wakati wa kula, hamna mtu kunywa maji mpaka umalize kula.

I found that rather old school and Draconian.

Mwaka 2001 Mkapa alimpandishia Tim Sebastian kwenye BBC "Hard Talk". Tim akambana tena, akamuuliza, "Sasa umekasirika"?

Tim nafikiri aliona labda Mkapa atasema sijakasirika nataka kujadili issues tu.

Ha, si Mkapa akamwambia damn right nimekasirika!

Nikasema huyu Mzee anakwambia haoni vibaya kusema amekasirika, haoni ni unprofessional kusema amekasirika, anaona ana assert right yake ya kukasirika kwa maswali yale.
 
sysafiri

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
267
250
Kimsingi alikuwa bado kijana mdogo asingeweza kupewa nchi wakati huo! Angevuruga nchi mapema.
Anyway kukubali kwake kuliwapendeza wazee.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,094
2,000
JK played it very smartly. He couldn't become the next president if he had persisted on being the rightful winner of the party election in 1995
..Na alikuwa amesafiria nyota ya Lowassa mpaka kufika hapo.

..aliyekuwa anautaka Uraisi seriously mwaka 1995 ni Lowassa, siyo Kikwete.

..baada ya Lowassa kukatwa kibabe na Mwalimu Nyerere, vijana waliokuwa ktk timu yake ya kampeni wakaamua kuhamishia nguvu zao kum-support Kikwete.

..Na walikuwa wamejizatiti kifedha na kimikakati. Lowassa na Kikwete ndio wagombea pekee waliokodisha ndege wakati wa zoezi la kutafuta wadhamini mwaka 1995.

..wadadisi wakaanza kujiuliza vijana hawa wachanga ktk siasa za Tz wametoa wapi mapesa ya kukodisha ndege?
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Katika hilo la Charisma Hayati Mkapa hakuwa nalo hata kidogo.
Watu waliofanya naye kazi wanamtambua kwa umakini na umahiri, lakini hawamkubali kwasababu tu ya charisma.
Nyerere alijua Mkapa alikuwa right candidate na kijana aliyemuandaa.
Hata hivyo, alijua pia ni ngumu sana kumuuza kwasababu hana Charisma kama ya Salim Ahmed Salim.

Alipokuwa Rais bado tatizo la charisma lilimfuata.
Mkapa alirekebisha sana uchumi na kuinua sana kada 'ya chini kuwa ya kati''.
Watu hawa appreciate kwasababu tu ya charisma.

Katika Diplomasia ya kimataifa hasa viongozi wa Afrika, Mkapa alikuwa anaogopwa, lakini si kwa charisma.

Wenyewe walikuwa wanamwita administrator kuliko politician.

Kutokana na kukosa charisma, Mauaji ya Zanzibar yamemfanya aonekane mbaya licha ya kusimama na kuomba msamaha. Ni viongozi wachache sana wanafanya hivyo.

Tofauti na Mkapa, CD Msuya ana 'moderate charisma'' lakini anasaidiwa sana na ''personality''
Charisma ipo ni kwa Dr Salim!
Charisma na personality nadhani ndo vilivyombeba Nyerere na kuendelea kupendwa licha ya kuboronga kwenye uchumi!

Imagine enzi zile za Nyerere kuhusu mambo ya maduka ya ugawaji, mambo ya uhujumu uchumi, hata Colgate kupatikana madukani ni shida, na kila aina ya ugumu wa maisha uliokuwepo, lakini bado aliendelea kupendwa na anaendelea kupendwa mpaka leo hii.

Pia, Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana wa ku connect na watu wengi wa kada tofauti tofauti.

Alikuwa na uwezo wa kuongea na masela wa kitaa na kukaa chini na kupiga nao stori, kunywa kahawa, na kucheza nao bao na pia kukaa na akina Margaret Thatcher kwenye mavikao huko Ulaya na kukata ishu kuhusu mambo ya kimataifa.

Pia, nahisi Nyerere alikuwa ni mwalimu mzuri sana shuleni kiasi kwamba akimfundisha mwanafunzi, halafu huyo mwanafunzi asielewe, basi tatizo ni la mwanafunzi na si mwalimu.

Alikuwa na uwezo mzuri sana wa kuelezea mambo na watu wakaelewa.

Sipati kabisa picha eti Rais Mkapa anakaa chini na kupiga stori na masela wa kitaa.

Wataongelea nini?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,833
2,000
Nyani Ngabu, post: 36713976, member: 188"]
Charisma na personality nadhani ndo vilivyombeba Nyerere na kuendelea kupendwa licha ya kuboronga kwenye uchumi!
Absolutely! Pamoja na hivyo viwili , Nyerere alisaidiwa sana na mambo mengine ya kujifunza
1. Alikuwa anasoma na uelewa wake wa mambo ulikuwa mkubwa sana.
2. Alikuwa ni msikivu tofauti na watu wanavyodhani.
3. uwezo wake wa kuzaliwa wa ku connect ilikuwa plus plus.
Imagine enzi zile za Nyerere kuhusu mambo ya maduka ya ugawaji, mambo ya uhujumu uchumi, hata Colgate kupatikana madukani ni shida, na kila aina ya ugumu wa maisha uliokuwepo, lakini bado aliendelea kupendwa na anaendelea kupendwa mpaka leo hii.
Hapa alitumia charisma na personality yake akaunganisha na 'connect' yake na audience. Yaani alikuwa akiongea utadhani anaongelea jambo nyumbani kwako.
Audience yake ilikuwa kubwa kwasababu ali-connect na wajinga sana na werevu sana. Wote walimwelewa
Pia, Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana wa ku connect na watu wengi wa kada tofauti tofauti.
Siku akiongelea kilimo utadhani yeye ni mkulima na hajawahi kuwa Rais. Siku akiongea na wafanyakazi utadhani yeye ameajiriwa na si Rais. Siku akiwa Nkrumah hall pale UDSM utajiuliza huyu ni profesa nani.
Alikuwa na uwezo wa kuongea na masela wa kitaa na kukaa chini na kupiga nao stori, kunywa kahawa, na kucheza nao bao na pia kukaa na akina Margaret Thatcher kwenye mavikao huko Ulaya na kukata ishu kuhusu mambo ya kimataifa.
yes !
Sipati kabisa picha eti Rais Mkapa anakaa chini na kupiga stori na masela wa kitaa.
Sina uhakika hata washikaji wa kawaida alipiga nao story. Sijui ilikuwa ni 'introvert' au ni kukosa tu charisma. Personality ya Mkapa ilijengwa, haikuwa natural.
Hata akiwa waziri, uwepo wake unajieleza kwa watu wanaomzunguka kama walinzi na wapambe, bila hao huwezi kuhisi uw epo wake. kwa vile hakuweza ku connect ilikuwa mbaya zaidi.

Tofauti na mtu kama Mzee Malecela au CD Msuya ambao personality tu itakusukuma kuuliza huyu ni nani.
Niliwahi kukutana tete a tete na Salim Ahmed, mzee ni mkarimu na mchesi sana. Ile Charisma na personality yake nilijikuta nime 'freeze'' baadaye nikawauliza wenzangu kila mmoja alikiri kitu tofauti alichohisi.

Charisma na personality ya Salim na uelewa vilimbeba akagombea kuwa UN SG akiwa na 35yrs.
 
TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,301
2,000
Kutoka mwaka 1995. Baada ya mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.

Akiwa anatoa hotuba ya kukubali matokeo, Rais mstaafu Kikwete aliongea maneno ambayo yalionekana kumgusa kwa furaha Rais mstaafu Nyerere hadi akanyanyuka na kuanza kupiga makofi huku akitabasamu.

Jionee mwenyewe jinsi mambo yalivyokuwa.

MAELEZO KUHUSU VIDEO
Kikwete alitoa kauli ya kumuunga mkono Rais Mteule wa CCM wa kipindi hiko, ambaye alikuwa Benjamini William Mkapa, na akataka mashabiki wake wakubaliane na hilo kwa kuwa uchaguzi(Wa ndani) umeshaisha.

Aidha aliposema kuwa kamati yake ya kampeni na kamati zote zisiszo rasmi kwa wakati huo akazitaka ziwe ni kamati za Mkapa, ndipo watu wakapiga makofi akiwemo Hayati Julius Kambarage Nyerere
Najiuliza why upendo huu haupo tena ndani ya ccm kiasi chuki nikali Sana
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,833
2,000
Najiuliza why upendo huu haupo tena ndani ya ccm kiasi chuki nikali Sana
Ni kwasababu ya vitu vinavyoitwa ''loyal na Stalwart''
Loyal ni utiifu tu kwa mtu au watu. Stalwart ni utiifu kwa taasisi iwe serikali , chama n.k.

Siku za nyuma CCM ya akina Warioba, Malecela n.k. ilikuwa na stalwart, kwamba, waliweza kusimama na kutetea masilahi ya chama wakiamini wanatetea masilahi mapana ya nchi. Walikubaliana na hata kukubaliani kutokubaliana.
Walikaa meza moja, na kwamba mawazo tofauti ilikuwa ni 'afya' si kukosa uzalendo au uadui.

CCM ya sasa ni ya ''loyalists' kwamba ili uweze ku-survive lazima uwe mmnyenyekevu kwa mtu au watu.
Ni kwasababu hiyo, hakuna stalwarts na loyalists wamebaki kuwa opportunists tu.
Kwahiyo chama hakina nguvu, mtu akisema tofauti anakuwa adui na si mzalendo.

Kutoka na hilo kuna resentment kubwa sana ndani ya chama. Resentment inakuwa na mood, grudge, hatred, disappointment etc. Kutokana na hilo utaona jambo moja kubwa sana linalotokea sasa hivi.
Kama uchaguzi ungekuwa huru CCM ingekuwa katika wakati mgumu sana.

Fikiria hivi, miaka 5 ya kampeni wakiwa wao wenyewe. Miaka 60 ya kutawala kama chama.
Tazama inavyohangaika katika kampeni licha ya ''msaada'' kutoka taasisi muhimu.

Ukiona watu wanakwenda au kushabikia upinzani kuna mawili
1. Wamechoka na CCM na wanadhani kunahitajika mabadiliko
2. Wamechoshwa na hawawezi kukabili ''resentment'' ndani ya CCM ambayo sasa si taasisi bali kakikundi tu ambako ili uweze kudumu lazima uwe 'loyal'' na ufunge mdomo, kinyume chake wewe si Mzalendo, ni adui na unatumiwa.
 
Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
16,807
2,000
..Na alikuwa amesafiria nyota ya Lowassa mpaka kufika hapo.

..aliyekuwa anautaka Uraisi seriously mwaka 1995 ni Lowassa, siyo Kikwete.

..baada ya Lowassa kukatwa kibabe na Mwalimu Nyerere, vijana waliokuwa ktk timu yake ya kampeni wakaamua kuhamishia nguvu zao kum-support Kikwete.

..Na walikuwa wamejizatiti kifedha na kimikakati. Lowassa na Kikwete ndio wagombea pekee waliokodisha ndege wakati wa zoezi la kutafuta wadhamini.
EL amebakia na ndoto zake moyoni. He couldn't make it. Urais sio kitu rahisi kama walivyofikiria. Ingawa masihala masihala angeweza kabisa kuwa Rais
 
Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
16,807
2,000
Ni kwasababu ya vitu vinavyoitwa ''loyal na Stalwart''
Loyal ni utiifu tu kwa mtu au watu. Stalwart ni utiifu kwa taasisi iwe serikali , chama n.k.

Siku za nyuma CCM ya akina Warioba, Malecela n.k. ilikuwa na stalwart, kwamba, waliweza kusimama na kutetea masilahi ya chama wakiamini wanatetea masilahi mapana ya nchi. Walikubaliana na hata kukubaliani kutokubaliana.
Walikaa meza moja, na kwamba mawazo tofauti ilikuwa ni 'afya' si kukosa uzalendo au uadui.

CCM ya sasa ni ya ''loyalists' kwamba ili uweze ku-survive lazima uwe mmnyenyekevu kwa mtu au watu.
Ni kwasababu hiyo, hakuna stalwarts na loyalists wamebaki kuwa opportunists tu.
Kwahiyo chama hakina nguvu, mtu akisema tofauti anakuwa adui na si mzalendo.

Kutoka na hilo kuna resentment kubwa sana ndani ya chama. Resentment inakuwa na mood, grudge, hatred, disappointment etc. Kutokana na hilo utaona jambo moja kubwa sana linalotokea sasa hivi.
Kama uchaguzi ungekuwa huru CCM ingekuwa katika wakati mgumu sana.

Fikiria hivi, miaka 5 ya kampeni wakiwa wao wenyewe. Miaka 60 ya kutawala kama chama.
Tazama inavyohangaika katika kampeni licha ya ''msaada'' kutoka taasisi muhimu.

Ukiona watu wanakwenda au kushabikia upinzani kuna mawili
1. Wamechoka na CCM na wanadhani kunahitajika mabadiliko
2. Wamechoshwa na hawawezi kukabili ''resentment'' ndani ya CCM ambayo sasa si taasisi bali kakikundi tu ambako ili uweze kudumu lazima uwe 'loyal'' na ufunge mdomo, kinyume chake wewe si Mzalendo, ni adui na unatumiwa.
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda, lazima wajifunze kwamba kutumikia wananchi sio tena suala la hiari. Ni lazima.
CCM ya mwanzoni ilijengwa na msingi huo wa kutumikia watu. Ila baadae, wakaamua kuruhusu kula kwa walio karibu na chama. Resentment lazima iwepo sababu, sasa sio tena kundi la walaji.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,094
2,000
EL amebakia na ndoto zake moyoni. He couldn't make it. Urais sio kitu rahisi kama walivyofikiria. Ingawa masihala masihala angeweza kabisa kuwa Rais
..EL alitapeliwa na JK.

..ilipofika kwenye suala la Richmond JK hakumpa support EL.

..na EL alipoondoka serikalini wanasema alikuwa depressed akaanza kunywa pombe kupindukia na kuathiri afya yake.

..kundi la Samuel Sitta, Harrison Mwakyembe, etc ndilo lililozima ndoto za Uraisi za EL.

..JK alipaswa kulishughulikia kundi hilo ili aweze kumlinda mwenzie na kutimiza ahadi walizowekeana na EL.

..nakubaliana na wewe 100% kwamba Uraisi siyo jambo rahisi. Unahitaji uwe na bahati kwelikweli.

NB:

..siyo kama namfagilia EL, ila nilitaka kueleza kilichotokea ndani ya ccm.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,833
2,000
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda, lazima wajifunze kwamba kutumikia wananchi sio tena suala la hiari. Ni lazima.
CCM ya mwanzoni ilijengwa na msingi huo wa kutumikia watu. Ila baadae, wakaamua kuruhusu kula kwa walio karibu na chama. Resentment lazima iwepo sababu, sasa sio tena kundi la walaji.
Wananchi wamepoteza imani na CCM, siyo suala la kusema bali linaonekana. Tazama kampeni za leo.
Ukizingatia miaka 5 CCM walikuwa na ''lee-way' ya kufanya lolote na chochote Bungeni ikiwemo matumizi ya fedha bila kuidhinishwa na Bunge n.k. CCM walitumia media za umma , wametumia kila resource hata kununua madiwani na wabunge. CCM wametumia mkono wa serikali kuwatia jambajamba Wapinzani ambao kila siku wapo mahubusu na mahakamani. Against all odds leo Wapinzania wanakimbizana na CCM kwenye kampeni!!!
Tena CCM wakiwa na msaada tu, kuvunja sheria kama za mikutano ya ''kikabila'' n.k.

CCM na taasisi zake muhimu watashinda uchaguzi, hata hivyo, wanafahamu kwamba umma unawakataa
Kitakachotokea ni siku moja umma wote wakiwemo hao wa taasisi nyeti kuamua kama mbwai iwe mbwai.

Kwa bahati mbaya CCM haitaindoka kwa heshima kama UNIP au KANU. Itaondoka tofauti kabisa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom