1981 Israel Raid on the Reactor: Jeshi la anga la Misri linaweza kufanya shambulizi la ghafla (Blitzkrieg) kwenye bwawa la umeme huko Ethiopia?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu watanzania;

Jeshi la anga la Misri linaweza kufanya shambulizi la ghafla (Blitzkrieg) kwenye bwawa kubwa la kuzalishia umeme huko Ethiopia (Grand Ethiopian Renaissance Dam) kama ambavyo Israel Defense Force (IDF) walivyofanya "Raid on the Nuclear Reactor" huko Iraq mwaka 1981?

SOMA KWA UFUPI KISHA CHA ISRAEL NA UVAMIZI KATIKA KINU CHA NYUKLIA HUKO NCHINI IRAQ:

Mnamo mwaka 1976, Iraq ilinunua kinu cha nyuklia (nuclear reactor) kutoka Ufaransa. Wakati Iraq na Ufaransa walikuwa wakiiendelea na ujenzi wa kinu kile cha nyuklia, ambacho wafaransa wenyewe waliamua kukipa jina la OSIRAK, na kilikusudiwa kwa matumizi ya amani hususan katika utafiti wa kisayansi, Waisrael waliutazama mradi ule kwa jicho la mashaka sana, wakiamini ya kwamba ulilenga katika kutengeneza silaha za nyuklia.

images (1).jpg


Mnamo tarehe 7 mwezi wa June Mwaka 1981, msafara wa midege ya kivita ya Israel aina ya F-16A ikisindikizwa na ndugu zake aina ya F-15As iliangusha makombora na mabomu mazito na kuharibu nyang'anyang'a kinu hicho cha OSIRAK. Israel wali iita operation ile kuwa ni ya kujilinda (pre-emptive attack) wakisema kwamba kinu kile kilikuwa kina si zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kuanza kutumika (before it might have become critical).

images.jpg


Askari kumi wa Iraq pamoja na engineer mmoja wa Ufaransa waliuawa. Shambulizi hilo lilifanywa wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu ndani ya bunge la Israel (Knesset).

Kwa wakati ule, shambulizi hili lilikutana na ukosoaji mkubwa sana kutoka jumuiya za kimataifa, ikiwemo Marekani, baraza la usalama pamoja na mkutano mkuu wa umoja wa mataifa katika matamko mawili tofauti.

Baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa vilifikia mpaka hatua ya kusema kuwa huu ulikuwa ni ugaidi wa kufadhiliwa na serikali (state-sponsored terrorism) na kwamba kitendo cha Israel kushambulia kinu hicho kwa kuvizia ni hatua ya ubabe na uchokozi usiosameheka.

images (7).jpg


Uharibifu wa kinu cha Osirak umekuwa ukitizamwa na baadhi ya wataalam wa masuala ya usalama, siasa pamoja na sheria za kimataifa kama mfano moja wapo wa shambulizi za kuzuia hatari (preventive strike) ambao wanasema pia ya kwamba liliirudisha nyuma sana Iraq kutoka hatua chache za kuwa na uwezo wa nyuklia (it brought back Iraq from the brink of nuclear capability) na kuzima kabisa ndoto za Rais Saddam Hussein kuja kumiliki silaha za nyuklia hapo baadae.

MZOZO BAINA YA MISRI NA ETHIOPI JUU YA BWAWA KUBWA LA KUZALISHIA UMEME:

118966735_10158220352551001_89250570897.jpg


Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Ethiopia inataka kujaza bwawa la Grand Renaissance kwa miaka 6 lakini Misri imependekeza angalau mradi huo uchukue kipindi cha miaka 10 kwa kuhofia kwamba kuchukua kipindi kifupi kutaathiri mtiririko wa maji ya Mto Nile ambayo inategemea asilimia 90 ya maji ya mto huo.

118966735_10158220352551001_89250570897xsdv.jpg


Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Ujenzi wa Bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia ukishamalizika, mradi huo unaogharimu kima cha bilioni 5 za Marekani, litakuwa ndio bwawa kubwa zaidi la uzalishaji umeme barani Afrika lenye uwezo wa 6,000MW.

(1) JE, AFRIKA ITAARAJIE KWA MARA YA KWANZA KUPOKEA "BREAKING NEWS" KAMA ZILE TULIZOZOEA KUZISIKIA KATIKA ARDHI YA MASHARIKI YA KATI?

(2) Njia ipi sahihi itumike katika matumizi ya maji ya mto Nile ili uhusiano miongoni mwa nchi za Africa uendelee kuwa mwema na imara??

WADAU KARIBUNI SANA KWA MICHANGO.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mto ambao ni chanzo cha huo mgogoro siyo mto Nile bali ni Blue Nile
[QUOTE="Infantry Soldier, post: 36223247, member:

Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

[/QUOTE]
Maji ya mto unaohusishwa na mgogoro huo siyo ya mto Nile bali ni Blue Nile na chanzo cha mto huo si Uganda na Tanzania bali ni Ethiopia.
Mto Nile ndiyo Chanzo chake kinazihusisha nchi za Tanzania na Uganda. Unge edit eneo hilo ili kuliweka sawa andiko lako.
 
Mto ambao ni chanzo cha huo mgogoro siyo mto Nile bali ni Blue Nile
[QUOTE="Infantry Soldier, post: 36223247, member:

Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.
Maji ya mto unaohusishwa na mgogoro huo siyo ya mto Nile bali ni Blue Nile na chanzo cha mto huo si Uganda na Tanzania bali ni Ethiopia.
Mto Nile ndiyo Chanzo chake kinazihusisha nchi za Tanzania na Uganda. Unge edit eneo hilo ili kuliweka sawa andiko lako.
[/QUOTE]
Mkuu, Njia ipi sahihi itumike katika matumizi ya maji ya mto Nile ili uhusiano miongoni mwa nchi za Africa uendelee kuwa mwema na imara??
 
Egypt wakileta uchuro, Israel na marekani wataingilia. Na namshauri Magu naye awe upande wa Ethiopia cz Misri imezidisha kujimwambafy
Mkuu, njia ipi sahihi itumike katika matumizi ya maji ya mto Nile ili uhusiano miongoni mwa nchi za Africa uendelee kuwa mwema na imara?
 
Alafu ile mada haijahoji solutions sahihi, ila mimi nimehoji njia za upatanishi
Sawa jamaa alisema tuchague upande wa kuunga mkono.

Mimi nilitofautiana naye kuhusu hili jambo la kuunga mkono, nikasema kuwa hili suala si la Misri na Ethiopia pekee, bali ni kwa nchi zote 'zinazotengeneza' mto Nile, wakae chini wajadili suluhisho la haki.

Ujue na sisi tuna mpango wa matumizi makubwa ya maji ya Victoria ambacho ni chanzo kikuu.

Maji yamefika Shinyanga, Tabora na sasa Igunga, yanatarajia Singida na hatimaye Dodoma.

ukiona mwenzako akinyolewa, tia sabuni kichwani kujiandaa
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom