1969 mwanadamu hakuweza kutua mwezini!

Mtoa mada unaweza kuwa na hoja za msingi maana nimeangalia Kile Chombo cha anga wanachotengeneza Boeing kwa kushirikiana na Lockheed Martin kinaitwa orion wamekitengeneza wakakirusha juu sana ya Tabaka la Dunia kupita ISS na satellite zote kikapita van allen radiation belt huku wakiweka sensors za aina mbalimbali kukusanya data.
Hii van Allen radiation belt ina chembechembe zenye chaji za nguvu kubwa zinazotokana na miale ya jua , milipuko ya nyota, Black holes, asteroids nk. Hili eneo ni hatari sana kiumbe hai chochote kikipita Lazima kipikwe kwa hio miale. Kwahiyo wataalamu wa Boeing na Lockheed Martin wanaumiza kichwa teknolojia ya kutengeneza shield ambayo itamlinda binadamu na hii miale.Nasa wamekubali mpaka sasahivi binadamu haijawezekana kumpitisha kwenye hii van Allen’s belt radiation. Safari yoyote ya mwezini,mars nk lazima ipitie van Allen’s belt radiation.
Kaka huelewi unachojadili, pamoja na mwenzako # Hammaz.
  • There are two main Van Allen belts – the inner belt and the outer belt – and a transient third belt. The inner belt is the more dangerous one, containing energetic protons. The outer one has less-dangerous low-energy electrons (Beta particles). The Apollo spacecraft passed through the inner belt in a matter of minutes and the outer belt in about 1+1⁄2 hours. The astronauts were shielded from the ionizing radiation by the aluminum hulls of the spacecraft. Furthermore, the orbital transfer trajectory from Earth to the Moon through the belts was chosen to lessen radiation exposure. Even James Van Allen, the discoverer of the Van Allen belt, rebutted the claims that radiation levels were too harmful for the Apollo missions. Phil Plait cited an average dose of less than 1 rem (10 mSv), which is equivalent to the ambient radiation received by living at sea level for three years. The total radiation received on the trip was about the same as allowed for workers in the nuclear energy field for a year and not much more than what Space Shuttle astronauts received.

Je, unaelewa vipimo vya "rem" na "mSv" vinavyotajwa katika matini ni ni ni? Unahitaji tafsir kwa Kiswahili?
 
Mwaka 2012, NASA walituma twin Van Allen Probes Instruments ili kufanya uchunguzi zaidi kuhusu Van belt radiation. Walichogundua ni kwamba ni impenetrable barrier in space, na ipo umbali wa Km 600 kutoka earth's surface. David Sibeck kutoka NASA Goddard Space Center anasema kwamba: Teknolojia yetu tuliyonayo sasa hivi bado si rafiki wa kuweza kupita kwenye hiyo mionzi , kwa sababu kuguswa kidogo tu kwa chombo kitakachopita kwenye hiyo mionzi hata kwa mara moja, ina uwezo wa kuleta athari ya moja kwa moja kwa chombo na astronauts.
Kaka mbona unatumia nukuu bandia?
1. Kwanza ni kweli NASA walichungulia Ukanda wa Van Allen kuanzia mwaka 2012 hadi 2019. Muda huu unaonyesha tayari kwamba hakuna "mpaka usiopitika" (impenetrable barrier in space) maana chombo chao kilipitapita huku kwa miaka saba!
2. Ni kweli kwamba Bw David Sibeck alikuwa katika uongozi wa mradi huu LAKINI MANENO UNAYOLETA SI MANENO YAKE! Ukidai menginevyo, lete ushahidi na chanzo chake!
3. Maelezo yake utakuta hapa:
 
1969 MWANADAMU HAkUWEZA KUTUA MWEZINI !!

Wamarekani walijitahidi sana kuudanganya Ulimwengu Mwaka 1969 kwa malengo yao binafsi kisiasa na kiuchumi, lakini Ukweli utabaki kuitwa Ukweli. Picha yote ya kwenda Mwezini Mwaka huo ilibuniwa ili kuulaghai Ulimwengu kwa sababu zifuatazo :

1- Mwezini hakuna Upepo unaovuma kama hapa kwetu,cha ajabu ilionekana Bendera ya Marekani ikipepea juu ya Mwezi tena kwa nguvu kubwa kabisa.

2- Picha zote walizo piga Angani zilikuwa za rangi,wakati ambao Teknolojia haikuwa na Uwezo wa kutoa Picha za rangi huko juu, bali ilitakiwa ziwe za rangi mbili tu, nyeupe na nyeusi.

3- Alama za Viatu vyao zilionekana kuzama sana chini,wakati Mwezini Vitu mfano wa Binadamu lazima vitakuwa vinaelea kwa sababu kitu kinachopima Kilo 60 Ardhini kitakuwa na kilo 10 Mwezi ni, na hii hutokana na Ukweli kuwa Mwezi hauna nguvu kubwa ya Uvutano (Gravitational Force) kama ilivyo Sayari ya Dunia.

4- Hakuna hata Nyota moja ilioonekana kwenye Picha za Wanaanga wakati wapo Mwezini. Ilitakiwa Nyota zionekane kwa sababu Matabaka hewa ya Mwezi (Atmosphere) ni sawa na hakuna. Hivyo, ni rahisi kuziona Nyota juu ya Mwezi.

5- Warusi waliwaomba Wamarekani kuwaelekeza wapi walipotua na kuweka Vyombo vyao vya Anga ili wavipige picha na kupata Ushahidi wa kuwepo na Ziara hiyo Mwezini.Kitu ambacho kilishindikana mpaka hii leo.

6- Waandaaji wa tukio lile hususan Upande wa Kamera,walijisahau na Vivuli vyao vilionekana kwa chini, wakati wakitoa maelekezo ya nini kifanyike.

Ndugu Msomaji,safari hii pamoja na kuwa ya mashaka, ilitangazwa mno na Ulimwengu mzima kuaminishwa kwamba,Wamerekani walitua Mwezini mnamo mwaka wa 1969.Mpaka leo hii Shule zote Ulimwenguni huwafundisha Wanafunzi wao juu ya Ukweli wa tukio hilo lililobuniwa.
Wewe una chuki binafsi na Marekani,umetoa sababu ambazo hazina mashiko kabisa,ukiwa kwenye mwezi na ukiwa Duniani ni Mambo mawili Tofauti kabisa, siyo lazima uzione nyota.
Halafu usilazimishe eti kwa sababu Urusi alikosa technology ya picha za Rangi eti na Marekani alikosa pia.
Haya sasa hivi Marekani ni Taifa Tajiri kuliko Urusi kwa hiyo huo utajiri wanaigiza pia?
Acha chuki wewe
 
Safi sana umeelezea in details Maana hii van Allen’s Kama ulivyoelezea ipo kms 600 kutoka duniani wakati astronauts na cosmonauts wa ISS wapo Kwenye Safe zone kms 300 kutoka duniani.In the space it is a very trouble place full of hazards and dangers. Juzi juzi alikuja visitor from outside solar system for the first time anaitwa oumuamua hii ni natural object ilikuja kwa kasi ya Ajabu ikazunguka Jua ikarudi ilipotoka sasahivi ipo maeneo ya Saturn Ikizidi kutokomea
Hizi ni hoja za kichekesho mno ,kwamba Wamarekani wasingeweza kwenda na kupenya hilo eneo ila warusi waliwezaje?
Huu ni utoto mtupu
 
Safi sana umeelezea in details 👌🏿 Maana hii van Allen’s Kama ulivyoelezea ipo kms 600 kutoka duniani wakati astronauts na cosmonauts wa ISS wapo Kwenye Safe zone kms 300 kutoka duniani.In the space it is a very trouble place full of hazards and dangers. Juzi juzi alikuja visitor from outside solar system for the first time anaitwa oumuamua hii ni natural object ilikuja kwa kasi ya Ajabu ikazunguka Jua ikarudi ilipotoka sasahivi ipo maeneo ya Saturn Ikizidi kutokomea
Izo kilometa zipo sahihi kweli.....
 
Jamani ujinga wa aina hiyo inaweza kusambazwa bila upingamizi?
1. Bendera: kwenye picha inaoyekana vema kwamba kuna fimbo iliyoingizwa ndani ya bendera ili ionekane. Si picha ya kitambaa kinachosukumwa na upepo.
View attachment 2029547

2. Alidai hapakuwa na picha za rangi wakati ule. Picha za rangi zimepatikana tangu karne ya 19! yaani miaka 100 kabla ya kutua mwezini.
220px-Tartan_Ribbon.jpg

(The first color photograph made by the three-color method suggested by James Clerk Maxwell in 1855, taken in 1861 by Thomas Sutton. The subject is a colored ribbon)
3. Nyayo za viatu haviko chini sana! Graviti mwezini ni 1/6 ya duniani; maana mtu mzima pamoja na suti yake ni takriban kilogramu 90, hivyo mwezini kama kilogramu 15- Je mtoto wa kilogramu 15 haachi nyayo ndefu alitembea kwenye vumbi laini (jinsi ilivyo uso wa Mwezi)???
4. Hakuna nyota kwenye picha: je umewahi kuelewa kamera? Wako mwezini wakati wa mchana kwenye Jua kali, hivyo Kamera itafunguka kifupi sana. (very short shutter speed). Basi haitoshi kupata nuru hafifu ya nyota.
5. Kuhusu Warusi sina habari; Wahindi walithibitisha kuiona Apollo: In April 2021 the ISRO Chandrayaan-2 orbiter captured an image of the Apollo 11 Lunar Module Eagle descent stage. The orbiter's image of the Apollo landing site was released to the public in a presentation on September 3, 2021. ONA Third-party evidence for Apollo Moon landings - Wikipedia
6. Viwuli: ni kawaida kabisa!
Yote ujinga mtupu. Walitua mwezini, si mara 1 tu, kati ya 1969 hadi 1972.
Nina swali jepesi sana mdau samahani lakini

Dunia ya leo imeadvance sana kwenye teknolojia nini kinachowashinda wamarekani kurudi tena mwezini???
 
Nina swali jepesi sana mdau samahani lakini

Dunia ya leo imeadvance sana kwenye teknolojia nini kinachowashinda wamarekani kurudi tena mwezini???
Wanapanga sasa kurudi. Kizuizi kilikuwa gharama na swali la kusudi. Pale mwanzoni walifika, waliona na kuonyesha kwamba binadamu anaweza kufika. Ilikuja: sasa wafanye nini? na je, safari mpya ilenge kufanya nini? Ilionekana kwamba katika mengi shabaha ziliweza kutimizwa kwa kutumia mitambo pekee; yaani kamera na vifaaa viliboreshwa, kwa hiyo hata vipimaanga (yaani satelaiti za kuzunguka mwezi) ziliweza kutekeleza vipimo na kuleta data nyingi. Iliwezekana pia kurusha magari, jinsi walivyofanya Wachina. - Marekani waliona miaka iliyopita, hawawezi kupata faida wakituma watu mwezini, walipendelea kupeleka mitabu Mirihi na penginepo.
Maana kumtuma binadamu angani ni gharama mara nyingi kuliko kupeleka mashine au roboti.
Ila sasa wanaona gharama za kusafirisha mizigo angani zimepungua, hivyo wanaona warudi na watu ambao wanaweza kufanya utafiti mbalimbali; mashine inaweza kutekeleza tu yale yaliyopangwa, ila binadamu anaweza kuanza kitu kipya kisichopangwa mbeleni.
 
Hizi ni hoja za kichekesho mno ,kwamba Wamarekani wasingeweza kwenda na kupenya hilo eneo ila warusi waliwezaje?
Huu ni utoto mtupu
Hakuna nchi yoyote imefanikiwa kupitisha Chombo Kikiwa na binadamu Kwenye van allen belt .

Evidence nimekutumia 👆🏿
 
Hakuna nchi yoyote imefanikiwa kupitisha Chombo Kikiwa na binadamu Kwenye van allen belt .

Evidence nimekutumia 👆🏿
Hujaleta kitu chochote kwa sababu huelewi ile Van Allen belt ni kitu gani. Tazama nilichokuandikia #82. "There are two main Van Allen belts – the inner belt and the outer belt – and a transient third belt. The inner belt is the more dangerous one, containing energetic protons. The outer one has less-dangerous low-energy electrons (Beta particles). The Apollo spacecraft passed through the inner belt in a matter of minutes and the outer belt in about 1+1⁄2 hours. The astronauts were shielded from the ionizing radiation by the aluminum hulls of the spacecraft. Furthermore, the orbital transfer trajectory from Earth to the Moon through the belts was chosen to lessen radiation exposure. "
Tofauti ni: hao wa NASA wanaajiri watu wanaoelewa kazi hiyo; hawaajiri watu waliosoma kidogo wakiamini kuna "impenetrable barrier" (ambayo haipo).
Nimekuuliza: "Je, unaelewa vipimo vya "rem" na "mSv" vinavyotajwa katika matini ni ni ni? Unahitaji tafsir kwa Kiswahili?"
Basi hujajibu. Hujaonyesha chanzo kimoja, umeleta tu maneno uliyonakili mahali ambapo hutaki kuonyesha. Nimekupa maelezo ya wemyewe kuhusu utafiti wao kwenye Van-Allen-Belt.
Ukitaka kupinga, onyesha vyanzo!
 
Angalia tv program ya will Smith inaitwa one strange rock ujifunze

Kadri unavyoacha dunia dozi ya cosmic rays inazidi kuwa kubwa
Kuna milipuko mikubwa sana inaitwa supernova nyuklia haikamati kwa hatari yake

Hio mionzi Mpaka sasahivi wataalamu wanaichunguza nguvu zake katika kumdhuru kiumbe hai Lakini wamedhibitisha inakata genes za kiumbe na kupelekea kiumbe kubadilika (mutation ) kutoka aina moja kwenda nyingine Kwahio binadamu anaweza kuwa alien.

Anga za mbali sio mahali pa kuishi binadamu.

Mwana anga wa marekani aliishi Mwaka mmoja Kwenye Iss alivyorudi duniani alikuwa amebadilika kilichochangia ni kukosekana kabisa kwa nguvu ya uvutano, mionzi nk

iss haipo mbali Sana na dunia je huko anga za mbali itakuwaje ? Bado wanasayansi wana chunguza

Kama waliweza mbona imekuwa shida kurudia tena .

Program ya Space shuttle ilipofungwa imechukua muda mfupi kurudi Kwenye iss nini imeshindikana Kwenye mwezi ?
 
Angalia tv program ya will Smith inaitwa one strange rock ujifunze

Kadri unavyoacha dunia dozi ya cosmic rays inazidi kuwa kubwa
Kuna milipuko mikubwa sana inaitwa supernova nyuklia haikamati kwa hatari yake

Hio mionzi Mpaka sasahivi wataalamu wanaichunguza nguvu zake katika kumdhuru kiumbe hai Lakini wamedhibitisha inakata genes za kiumbe na kupelekea kiumbe kubadilika (mutation ) kutoka aina moja kwenda nyingine Kwahio binadamu anaweza kuwa alien.

Anga za mbali sio mahali pa kuishi binadamu.

Mwana anga wa marekani aliishi Mwaka mmoja Kwenye Iss alivyorudi duniani alikuwa amebadilika kilichochangia ni kukosekana kabisa kwa nguvu ya uvutano, mionzi nk

iss haipo mbali Sana na dunia je huko anga za mbali itakuwaje ? Bado wanasayansi wana chunguza

Unamaanisha Will Smith yule rapa? Nijifunze nini kwake kuhusu anga?
Mionzi haiongezeki kadri uanvyoenda mbali na Dunia.
1) mionzi ni kali katika kanda nyembamba inayoviringisha Dunia, kwa sababu ugasumaku wa Dunia unatukinga kwa kuelekeza upepo wa Jua (solar wind) kuzunguka Dunia.
2. Baada ya kupita kanda hiyo (=ukanda wa van Allen) ukali unapungua
3. Muda wote kuna mkondo wa chembe zenye chaji kutoka Jua; mara kwa mara kuna milipuko kwenye Jua inayorusha kiwango kikubwa angani; lakini mawingu hayo (coronal mass ejection) hayaelekei pande zote; ni kama wingu linalopita mara hapa mara huko. Hizo ni habari tunazoona wakati mwingine tukisikia kuhusu dhoruba ya Jua (solar storm) inayoweza kushinda ugasumaku na kuleta vurugu kwenye mitandao ya umeme. Mara nyingi zinapita mbali na Dunia.
4. Unayotaja kuhusu milipuko ya nyota (Nova, supanova) inaweza kuwa tatizo hata kwa uhai wote duniani ikitokea kwenye nyota ya karibu; kwa bahati nzuri imeshagunduliwa kwamba hatutapata nova karibu nasi kwa miaka ielfu mingi inayokuja.
5. Unachosema kuhusu matatizo ya kiafya ya wanaanga baada ya kukaa mwaka mmoja kwenye ISS, haina uhusiano na mnururisho wa anga. Hayo ni matatizo ya kukaa muda mrefu bila graviti. Hapo ni sababu kwamba wanaanga wote wana ratiba kali ya mazoezi kwa ajili ya musuli ya mwili. Pia imeshaeleweka tatizo lipo kwa hiyo kuna programu inayoandaliwa na ,madaktari kuwapokea na kuwasaidia kujenga musuli tena baada ya kurudi.
 
Will Smith anawashirikisha wanaanga wa nasa angalia kipindi kwanza usiongee kirahisi kama unatoka Dar kwenda moro.

Nani anaweza kutabiri mlipuko wa jua ili kuepuka?

Earth magnetic field inatuepushana na radiation particles hatari za milipuko mbalimbali ya anga za mbali

Hizi ni hoja za kichekesho mno ,kwamba Wamarekani wasingeweza kwenda na kupenya hilo eneo ila warusi waliwezaje?
Huu ni utoto mtupu
Mkuu huku hakuna siasa leta facts. Siasa peleka kwenye majukwaa ya siasa ndiyo maana unaona wenzako wanakuja na facts siyo blabla zako za siasa. Mambo mengine waachie wanaojua mkuu!
 
Duua.kwa Mimi ninavyofahamu ile mission ilikua faked hata ukiangalia much inaitwa interstellar wanaeleza kabisa kwamba misssion was faked
 
Nani anaweza kutabiri mlipuko wa jua ili kuepuka?

Earth magnetic field inatuepushana na radiation particles hatari za milipuko mbalimbali ya anga za mbali

Kaka,
1) Kila mwanafizikia anayejua muundo wa nyota kikemia (asilimia ya elementi zilizopo yaani hidrojeni, heliamu na nyingine), masi yake na mng'aro -ambayo yote hupimika- anaweza kukadiria muda unaobaki hadi akiba ya hidrojeni kwenye kiini imekwisha. Kinachofuata ni mlipuko. Kwa Jua letu ni miaka bilini 3 bado. Kwa nyota zilizo karibu makadirio yametekelezwa.
2) Unaleta ukurasa mzuri katika link pale juu lakini HUJAUSOMA!! Ukurasa ule wa mamlaka ya usafiri wa anga ya Kanada unaeleza vizuri sana hatari za mnururrisho wa angani. Unasema hali ya mwanaanga ni sawa na muuguzi anayeshughulika mitambo ya X-ray duniani. Kwa hiyo ni lazima kufuatilia kwa makini muda wa kuathiriwa na mionzi, maana mwili hutakiwi kuathiriwa zaidi ya kiwango fulani. Hii ni kazi wanayofanya wataalamu wengi katika taasisi za usafiri wa anga.
3) Kama ungesoma yale unayotaja, ungekuta pia ukurasa unaoeleza Kanada inajiandaa kumtuma mtu mwezini pamoja na safari ijayo ianyopangwa. Na wanaonyesha nyayo za hao Wamarekani mwezini.
1638513793074.png

16-24/julai/1969 Neil Armstrong,Buzz Adrin, na Mike Collins walisafiri hadi mwezini, hayo mengine kawafundishe washamba wa uko kwenu.
Tukio lilikuwa live mwanzo hadi mwisho(youtube video ipo)
Hoja ya tatu ni dhaifu sana kuliko zote ingawa zote ni dhaifu.
Wenzako mwezini wameenda zaidi ya mara tatu hata hao warusi unaowasema wameenda sana tu.
Wenzako wamejenga space station,na wanatuma vyombo sayari za mbali kuliko hapo mwezini.
Kuhusu bendera kupepea wakati hakuna upepo maelezo yake yapo wazi,NASA walijua kabisa mwezini hakuna upepo hivyo bendera isingepepea hivyo kipindi Adrin anapiga saluti mbele ya
bendera alivuta uzi (picha inaonyesha) uliofungwa kwa lengo la kuifanya ipepea ila ukiangalia picha ya mwisho kipindi wanaondoka bendera imesinyaa kabisa.
Kwa watu wanaojua teknolojia ya space shuttling hawawezi kuamini upuuzi wako.
Tembelea NASA na website ya SPACE upate maarifa kijana sio umekaa tu unamshangaa Amber ruty.
Nisamehe kwa reaction yangu huo ndio udhaifu wangu nikikutana na hoja za kipuuzi.
Mkuu usisubiri mpaka uaminishwe kuna muda lazima uitumie akili yako sio mpaka waanze kukuchambulia
Jiwe wanalo sema wametoka nalo mwezini si chochote bali lilichukuliwa kutoka Antarctica. Mkurugenzi wa NASA, Werner Von Braun, ambaye ni mmoja kati ya wanasayansi wa NAZI walioingizwa Marekani baada ya WWII kupitia mpango wa paper clip, jamaa huyu aliyepaswa kushtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uvunjaji wa haki za binaadam lakini alipewa ukuregenzi wa NASA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom