1968 Oscar Kambona interview

Kagera imevamiwa 1978 lakin siku ya Uzinduzi wa Bomba la Mafuta kule Horogoro Tanga, Museven alisema Horohoro inamkumbusha 1972 wakati akipitishiwa Silaha na Serikal ya Nyerere kwenda kushambulia Uganda kutokea Kagera

Bado unasubiri RTD sio TBC ikutangazie nani alikuwa Mgomvi?
Dogo ulitaka Mkoa wa Kagera ukaliwe na Majeshi ya Uganda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuweka record sawa, huyo jamaa (Rip) mwaka 1964 wakati JWTZ lilipoasi dhidi ya serikali ya Nyerere na yeye akiwa, nafikiri waziri wa ulinzi, ndiye aliyezima uasi huo.

Aliongea na wanajeshi waasi wa JWTZ waliotaka kuongea naye yeye kama waziri wa ulinzi na ndipo yeye Kambona akaongea na balozi wa Uingereza na Uingereza ikaleta vikosi vya makomandoo na kuutokomeza kabisa uasi huo.

Wakati hayo yote yakitokea Mwl. Nyerere alitoroshwa na huyu huyu Kambona na kwenda kumficha huko Mkuranga hadi hali ilipotengemaa ndipo Nyerere akarejeshwa tena Dar.

Baada ya matukio hayo inaonekana Nyerere hakumuamini tena Kambona na alihisi kutokuwa salama wakati huyo jamaa akiwa serikalini kwani Kambona alionekana kuaminiwa zaidi na mataifa ya magharibi kuliko yeye Nyerere aliyeonekana machoni mwa wazungu kama A Communist.

Tukubali tusikubali, huyu Kambona kama ndio angekuwa rais nchi hii leo ingekuwa inacheza ligi moja na Nigeria, South Africa, Egypt, Algeria na Morocco kiuchumi.

NB: Huyu jamaa kuna kipindi wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alimnasa Kawawa (Rip) kibau kwenye kikao kimoja na wakoloni baada ya Kawawa "Kubwabwaja" kitu alichoona ni cha hovyo, mwenye kumbukumbu atujuze zaidi.
 
Amino
Kagera imevamiwa 1978 lakin siku ya Uzinduzi wa Bomba la Mafuta kule Horogoro Tanga, Museven alisema Horohoro inamkumbusha 1972 wakati akipitishiwa Silaha na Serikal ya Nyerere kwenda kushambulia Uganda kutokea Kagera

Bado unasubiri RTD sio TBC ikutangazie nani alikuwa Mgomvi?

Sent using Jamii Forums mobile app
IDD Amini alikuwa ni hatari katika ustawi wa East Africa, hata Kenya mwanzoni Moi alimpa Support lakini baadaye alidai maeneo ya Western Kenya ni ya Uganda akajikuta anaingia mzozo
 
Ukipenda kuelewa vizuri mchango wa Oscar Kambona, soma kitabu hiki: THE MAKING OF TANGANYIKA byJudith Listowel. Published by Chatto and Wundus, 1965. Kitafute kwenye maktaba za Tanzania. I read it about 40 years ago, and it left a lingering impression on me.

Inawezekana Kambona alifanya makosa baada ya kufarakana na Mwalimu, makosa kama ya kushirikiana na Wareno waliokuwa Mozambique wakati ule. Inasemekana alikuwa anatumia ndege zao kudondosha vipeperushi Tanzania. Lakini hakuna mtu aliyeweza kuimarisha TANU miaka michache kabla na baada ya Uhuru kama Kambona.

Oscar Kambona anastahili kuwekwa kwenye orodha ya mashujaa wa Tanzania.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe..
 
Kuweka record sawa, huyo jamaa (Rip) mwaka 1964 wakati JWTZ lilipoasi dhidi ya serikali ya Nyerere na yeye akiwa, nafikiri waziri wa ulinzi, ndiye aliyezima uasi huo.

Aliongea na wanajeshi waasi wa JWTZ waliotaka kuongea naye yeye kama waziri wa ulinzi na ndipo yeye Kambona akaongea na balozi wa Uingereza na Uingereza ikaleta vikosi vya makomandoo na kuutokomeza kabisa uasi huo.

Wakati hayo yote yakitokea Mwl. Nyerere alitoroshwa na huyu huyu Kambona na kwenda kumficha huko Mkuranga hadi hali ilipotengemaa ndipo Nyerere akarejeshwa tena Dar.

Baada ya matukio hayo inaonekana Nyerere hakumuamini tena Kambona na alihisi kutokuwa salama wakati huyo jamaa akiwa serikalini kwani Kambona alionekana kuaminiwa zaidi na mataifa ya magharibi kuliko yeye Nyerere aliyeonekana machoni mwa wazungu kama A Communist.

Tukubali tusikubali, huyu Kambona kama ndio angekuwa rais nchi hii leo ingekuwa inacheza ligi moja na Nigeria, South Africa, Egypt, Algeria na Morocco kiuchumi.

NB: Huyu jamaa kuna kipindi wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alimnasa Kawawa (Rip) kibau kwenye kikao kimoja na wakoloni baada ya Kawawa "Kubwabwaja" kitu alichoona ni cha hovyo, mwenye kumbukumbu atujuze zaidi.
Huo ulikuwa mchezo wa waingereza kutaka kumdhoofisha Nyerere, na Mzee kifimbo pengine aliugundua mapema ndo Maana akamtuma Kambona akijua kabisa kuwa na yeye anamkono katika uhasi
 
Ni kweli Kambona alipoteza pale alipofanikiwa kuongea na kutuliza maasi kwa kipindi kabla ya Jeshi la Uingereza kutumwa kuwanyanganya silaha waasi. Inasemekana wakati wa mazungumzo na waasi walikuwa wamemwambia ajitangaze kama Rais na wao wangemlinda.

Kambona alijitoa sana katika kupambania Uhuru wa nchi hii. Kama Nyerere aliacha kazi ya mshahara akiwa mwalimu huko Dodoma na ndiye aliyetia hamasa katika kuipaisha TANU akiwa na Bibi Titi Muhamed.
Kuweka record sawa, huyo jamaa (Rip) mwaka 1964 wakati JWTZ lilipoasi dhidi ya serikali ya Nyerere na yeye akiwa, nafikiri waziri wa ulinzi, ndiye aliyezima uasi huo.

Aliongea na wanajeshi waasi wa JWTZ waliotaka kuongea naye yeye kama waziri wa ulinzi na ndipo yeye Kambona akaongea na balozi wa Uingereza na Uingereza ikaleta vikosi vya makomandoo na kuutokomeza kabisa uasi huo.

Wakati hayo yote yakitokea Mwl. Nyerere alitoroshwa na huyu huyu Kambona na kwenda kumficha huko Mkuranga hadi hali ilipotengemaa ndipo Nyerere akarejeshwa tena Dar.

Baada ya matukio hayo inaonekana Nyerere hakumuamini tena Kambona na alihisi kutokuwa salama wakati huyo jamaa akiwa serikalini kwani Kambona alionekana kuaminiwa zaidi na mataifa ya magharibi kuliko yeye Nyerere aliyeonekana machoni mwa wazungu kama A Communist.

Tukubali tusikubali, huyu Kambona kama ndio angekuwa rais nchi hii leo ingekuwa inacheza ligi moja na Nigeria, South Africa, Egypt, Algeria na Morocco kiuchumi.

NB: Huyu jamaa kuna kipindi wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alimnasa Kawawa (Rip) kibau kwenye kikao kimoja na wakoloni baada ya Kawawa "Kubwabwaja" kitu alichoona ni cha hovyo, mwenye kumbukumbu atujuze zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa elimu Tanzania tena professor hawezi kuongea sentence tatu za kiingereza hata magufuli mwenyewe hawezi kuongea hata sentence 2.
Sisi wabongo bado sana tofauti na wenzetu
Kwani kuongea kingereza ndiyo nini?
Unajua huu ujinga wa kujiona umeendelea kisa kujua hiyo lugha, hata wazungu wenyewe Wanatuona ni mandezi. Penda cha kwako kwanza, kama kuenea hiyo Lugha hadi huku ikafika ni wazungumzaji wake wa asili walianza kuipenda kisha wakajivunia kuongea popote. Ndiyo hadi huku wakaijua hao wengine, tuacheni fikra za kitumwa
 
Kwa mujibu wa video, mahojiano haya yalifanyika huko nchini Nigeria mnamo mwaka 1968. Mwaka mmoja baada ya Kambona kwenda ukimbizini huko nchini Uingereza.

siku wakoloni weusi ccm wakiondolewa itabidi tuunde tume ya kuandika upya historia ya Tanzania na kubadilisha mfumo mzima wa elimu maana historia na elimu tuliyo nayo sasa sio ya kumfanya mtazania ajitambuwe na awe na uwezo wa kumundu mazingira na kutatuwa matizo yanayo mzunguka. Historia iliyo na mfumo wa elimu iliyopo sasa ni ya kuwafanya watu wajinga kwa ajili ya manufaa ya wakoloni weusi ccm. ndio maana tuna ma PHD holders ambao hawana uwezo hata wa kujikimu kimaisha bila kujipendekeza kwa watawala. Tunahitaji kujenga system ambayo taaluma na welidi vinazingatiwa katika kufanya maamuzi na mipango ya kijamii.
 
Mwaka 1968 Kambona anasema kuna viashiria vya udikteta Tanzania. Mwaka 2020 kuna watu bado wanadai kuna viashiria vya udikteta. Maana yake yeyote anayesema haya aidha 1968 au 2020 is not smart at all.
 
Nyerere alijiepusha Kushiriki Msiba wa Kambona 1997 kama ambavyo Milton Obote (Rais wa Kwanza wa Uganda) alivyokataa kushiriki Msiba wa Nyerere hata kutoa pole japo Nyerere alituingiza Vitani 1978 ili amrejeshe Madarakani Shosti yake Obote

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee sikujua hili. Walitofautiana nini Obote na Mwalimu ilhali nchi yetu iliingia hasara kubwa kifedha na uhai wa watu wake katika vita ile ya kumtetea Obote?
 
Huo ulikuwa mchezo wa waingereza kutaka kumdhoofisha Nyerere, na Mzee kifimbo pengine aliugundua mapema ndo Maana akamtuma Kambona akijua kabisa kuwa na yeye anamkono katika uhasi
Waingereza wangekuwa na nia ya kumuondoa wangetumia hiyo fursa kwani Nyerere aliishapotea maboya na hao hao waingereza wakamrejesha tena madarakani.
 
Kipindi kile ilikua unachagua team ya ushindi Kwa level ya mwelekeo wa kidunia. Mwalm alichagu team ya ushindi ilio shindwa Kwa level ya kidunia.
Kambona alichagua team ya ushindi Kwa level ya kidunia lakin hakua na mamlaka ya kuelekeza taifa kwenye team hiyo. Laiti mwalm pamoja na influence aliokuanayo angechagua team ya kambona ....

Rejea CCM na kuvunja makundi, Kwa level hio (crude) then transform Kwa level ya world order.
Utaelewa nini kilikua kikiendea kipindi hicho muhimu kilicho leta Amani duniani kwa Ku promote capitalism na democracy.

My take, kamboan was in a right track, nyere was in the wrong track, but they all had a good intation for their people.
 
Heshima sana wanajamvi,Oscar Kambona alianza kutofautiana na Mwl Nyerere hasa kuhusu azimio la Arusha.

Mwl alipenda siasa za ujamaa hasa baada ya kufanya ziara nchini China wakati huo chini ya utawala wa Mao_Oscar akipendelea zaidi siasa za kibepari na pengine tungefuata siasa za ubepari tungekuwa mbali sana.

Oscar Kambona alipinga sana uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa kama kibbutz Israel lakini Kambona alitaka vianzishwe vijiji vya mfano kwanza kabla ya kunzisha nchi mzima ( pilot scheme).Nyerere akiungwa mkono na Kawawa walimshinda Kambona na vijiji vya ujamaa vikaanzishwa na matokeo yake kila mtu anajua.

Baada ya kadhia hiyo Kambona alikimbia nchi na Sisi tukabaki kukarishwa siasa za kipumbuvu “Kambona ameolewa huko Ulaya”
 
Thanks for this, hivi ni vitu adimu, jamaa was smart
P

Lakini baada ya Kambona kukimbia Nchi, tukawa tuna karirishwa kwamba Kambona ni msaliti,mpenda madaraka na kibaraka wa mabeberu! Tumeimba nyimbo za kumkashifu tangu tupo shule za msingi, O-level.A-level mpaka National Service - hakuna aliye amini kwamba Kambona ni smart upstairs - mimi ndio mara yangu ya kwanza kusikia sauti yake na anaonekana wazi wazi analytical mind yake ni moto wa kuotea mbali - mtu mu ona mbali kama huyo hasinge weza kupikwa chungu kimoja na Kambarage hasa hasa baada ya Kambarage kutaka kuingiza siasa za kisoshalisti alizo ibua huko Uchina, tuwe wakweli hapa idealogies za ki socialist zili cost our Nation an arm and leg - Kambona aliona mapema zaidi kwamba tunako kwenda kuna walakini - he was right.
 
Kuweka record sawa, huyo jamaa (Rip) mwaka 1964 wakati JWTZ lilipoasi dhidi ya serikali ya Nyerere na yeye akiwa, nafikiri waziri wa ulinzi, ndiye aliyezima uasi huo.

Aliongea na wanajeshi waasi wa JWTZ waliotaka kuongea naye yeye kama waziri wa ulinzi na ndipo yeye Kambona akaongea na balozi wa Uingereza na Uingereza ikaleta vikosi vya makomandoo na kuutokomeza kabisa uasi huo.

Wakati hayo yote yakitokea Mwl. Nyerere alitoroshwa na huyu huyu Kambona na kwenda kumficha huko Mkuranga hadi hali ilipotengemaa ndipo Nyerere akarejeshwa tena Dar.

Baada ya matukio hayo inaonekana Nyerere hakumuamini tena Kambona na alihisi kutokuwa salama wakati huyo jamaa akiwa serikalini kwani Kambona alionekana kuaminiwa zaidi na mataifa ya magharibi kuliko yeye Nyerere aliyeonekana machoni mwa wazungu kama A Communist.

Tukubali tusikubali, huyu Kambona kama ndio angekuwa rais nchi hii leo ingekuwa inacheza ligi moja na Nigeria, South Africa, Egypt, Algeria na Morocco kiuchumi.

NB: Huyu jamaa kuna kipindi wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alimnasa Kawawa (Rip) kibau kwenye kikao kimoja na wakoloni baada ya Kawawa "Kubwabwaja" kitu alichoona ni cha hovyo, mwenye kumbukumbu atujuze zaidi.

Wabaya wa Kambona walimgeuzia kibao na kudai eti Kambona ndiye alikuwa the brains behind ya uasi wa wanajeshi, kinachoshangaza zaidi Nyerere inaelekea alikubaliana na maoni yawafitini hao, kasahua kabisa kwamba kama Kambona angekuwa na nai ya kumpindua Nyerere hasinge mpeleka sehemu salama mafichoni, hasinge omba msaada wa jeshi la Uingereza kuzima uasi, angetumia majeshi hayo kumsimika kwenye kiti cha Urais lakini hakufanya hivyo.
 
Kipindi kile ilikua unachagua team ya ushindi Kwa level ya mwelekeo wa kidunia. Mwalm alichagu team ya ushindi ilio shindwa Kwa level ya kidunia.
Kambona alichagua team ya ushindi Kwa level ya kidunia lakin hakua na mamlaka ya kuelekeza taifa kwenye team hiyo. Laiti mwalm pamoja na influence aliokuanayo angechagua team ya kambona ....

Rejea CCM na kuvunja makundi, Kwa level hio (crude) then transform Kwa level ya world order.
Utaelewa nini kilikua kikiendea kipindi hicho muhimu kilicho leta Amani duniani kwa Ku promote capitalism na democracy.

My take, kamboan was in a right truck, nyere was in the wrong truck, but they all had a good intation for their people.
right truck! TRACK.
 
Back
Top Bottom