!?!?!?

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Mama kamkuta binti akiwa juu ya mti wa mwembe.MAMA;We binti kwanini unapanda juu ya mti wakati kuna wavulana hapa chini,hujui watakuchungulia nguo yako ya ndani? BINTI;Hahahaah! nilishawasoma kitambo na ndo maana kabla ya kupanda juu ya mti niliivua.
 
Mjukuu kamkuta bibi yake akianika ch*pi kwenye kamba,mjukuu akauliza;bibi hiyo nini?.Bibi akajibu;hii ni nguo yangu ya kujifutia mikono baada ya kula.Siku moja bibi aliitafuta sana nguo yake bila mafanikio,akamuuliza mjukuu wake kama ameiona nguo yake ya kujifutia mikono?Mjukuu akajibu;nimewapelekea wageni mezani ili wajifutie baada ya kula!
 
Mjamaica mmoja akiwa uingereza kwa mara yake ya kwanza alipanda double decked bus yenye upstairs na downstairs.Alipoingia ndani,siti za downstairs zilikuwa zimejaa hivyo akaambiwa aende upstairs.Alipofika upstairs mara ghafla akashuka downstairs huku akilalamika;we konda unafikiri mimi mjinga,kule upstairs hakuna driver!
 
Jamaa mmoja kwa sababu alikuwa na matatizo ya pressure,alishauriwa na doctor asitumie vitu vya mafuta,toka siku hiyo jamaa anaogopa kupanda hata magari kwa sababu yanatumia mafuta!
 
Babu mmoja alikuwa amekaa kibarazani na mjukuu wake aliyetoroka shule.Mara kwa mbali wakamuona mwalimu anakuja.Babu akamshauri mjukuu aingie ndani ajifiche,mjukuu akajibu;wewe ndo inabidi ujifiche kwa sababu shuleni nimeomba ruhusa kwa kuwadanganya wewe umekufa!
 
Asante sana mkuu umenifanya nicheke asubuhi hii...big up hahahahaha
 
Baunsa mmoja baada ya kutupwa jela,akaanza kuwapia mkwara wafungwa wenyeji;nasikia humu kuna watu wanajifanya vidume wa kuwageuza wenzao,sasa ole wake mtu aniguse atanitambua!kwa hasira akapiga kichwa ukuta kwa nguvu,akadondoka na kuzimia.Alipozinduka baadaye tayari alikuwa kalowana chapa chapa.
 
Dogo mmoja alipotoka shule alikuta kitu kama samaki kimebanikwa jikoni.Dogo akamchukua yule aliyeamini ni samaki akaenda kumla kwa ugali aliowekewa.Mara baada ya kula akamsikia bibi yake akilalamika kwamba hamuoni kinyonga wake wa dawa aliyembanika jikoni!
 
Babu mmoja alikuwa amekaa kibarazani na mjukuu wake aliyetoroka shule.Mara kwa mbali wakamuona mwalimu anakuja.Babu akamshauri mjukuu aingie ndani ajifiche,mjukuu akajibu;wewe ndo inabidi ujifiche kwa sababu shuleni nimeomba ruhusa kwa kuwadanganya wewe umekufa!
duh. Mkuu umenichekesha hapa balaa. Machozi yanantoka kwa kicheko ivoo!
 
Mjamaica mmoja akiwa uingereza kwa mara yake ya kwanza alipanda double decked bus yenye upstairs na downstairs.Alipoingia ndani,siti za downstairs zilikuwa zimejaa hivyo akaambiwa aende upstairs.Alipofika upstairs mara ghafla akashuka downstairs huku akilalamika;we konda unafikiri mimi mjinga,kule upstairs hakuna driver!

mamaaa mbavu zangu mie!!!
 
Mjukuu kamkuta bibi yake akianika ch*pi kwenye kamba,mjukuu akauliza;bibi hiyo nini?.Bibi akajibu;hii ni nguo yangu ya kujifutia mikono baada ya kula.Siku moja bibi aliitafuta sana nguo yake bila mafanikio,akamuuliza mjukuu wake kama ameiona nguo yake ya kujifutia mikono?Mjukuu akajibu;nimewapelekea wageni mezani ili wajifutie baada ya kula!

hahahah...napta 2 jaman..
 
Back
Top Bottom