18 wanaswa na Pembe za Ndovu 9 mkoani Morogoro

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu 18 kwa tuhuma za makosa mbalimbali, ikiwemo kupatikana na silaha ya kivita aina ya AK 47 na pembe za ndovu tisa, zenye thamani ya Sh milioni 210.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Wilbroad Mutafungwa alisema, watu wawili walikamatwa wakiwa na vipande vya pembe za ndovu hizo zenye uzito wa kilo 4. 30 vyenye thamani ya Sh milioni 35. 9.

Watuhumiwa hao ni Khalid Likoboko (24) mkazi wa Kisaki Stesheni na Msafiri Haji (31) mkazi wa kijiji cha Ndevu Kisaki na dereva wa pikipiki aina ya Houjio iliyobeba pembe hizo zilizohifadhiwa kwenye begi dogo. Watuhumiwa hao walikutwa na nyara za serikali Februari 13, mwaka huu majira ya saa mbili usiku maeneo ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Matinde Kijiji cha Mbwande Kata ya Bwalila Chini wilaya ya Morogoro.

Polisi wakiwa doria waliwakamata watu wawili wakiwa na vipande viwili wa pembe za ndovu. Kamanda huyo alitaja tukio jingine ni watu watatu kukamatwa na Polisi ambao ni Shomari Mponda (28) mkazi wa Nanungu na William Mgaya (32) mkazi wa Ifakara. Watu hao walikamatwa na pembe za ndovu tatu zenye uzito wa kilo 4.8 zenye thamani ya Sh milioni 104. 2.

Pembe hizo zilikuwa zimehifadhiwa chini ya matofali kwenye nyumba inayoendelea kujengwa pagale maeneo ya kijiji cha Mwaya wilaya ya Ulanga . Tukio hilo ni la Februari 9, mwaka huu majira ya saa mbili usiku Kijiji cha Bwawani Tarafa ya Kiberege wilaya ya Kilombero. Siku hiyo Polisi walimkamata Sefu Ngaoma (48), mkazi wa Kiberege akiwa na bunduki aina ya shotgun ambayo imefutwa namba zake, gololi 25 , vipande vya nondo viwili na maganda mawili ya shotgun.

Kwa mujibu wa Mutafungwa, kukamatwa kwa pembe za ndovu hizo ni baada ya kuhojiwa kwa Mponda, ambaye alimtaja Ngaoma kuwa huwa anawaazima silaha hiyo kwa ajili ya kwenda kuua tembo katika Pori la Akiba la Selous. Kamanda huyo pia alitaja tukio lingine kuwa ni la Februari 18, mwaka huu majira ya saa tisa usiku Kijiji cha Iputi wilaya ya Ulanga, ambapo watu wawili, Hassan Chikoko (23) na Sudi Salum (37), wakazi wa Iputi, walikamatwa na pembe za ndovu nne zenye uzito wa kilo 3.6 zenye thamani ya Sh milioni 69. 9 zikiwa zimefichwa kwenye tanuru la matofali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom