Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,565
Watu 17 wa Ukoo Mmoja wakiwemo watoto wadogo, wameuwawa kwa kucharangwa mapanga usiku wa manane wa kuamkia leo huko Musoma.
Kwa mujibu wa Radio One Breaking News asubuhi hii, mauaji hayo yanahusishwa na tukio la kulipiza kisasi lililohusisha watu wa koo moja dhidi ya nyingine!.
Marehemu watazikwa kesho!.
Very sad!.
Update 1
Watu 17 wauawa Musoma
Imeandikwa na Basil Msongo; Tarehe: 16th February 2010 @ 13:17 Imesomwa na watu: 419; Jumla ya maoni: 1
WATU 17 wakiwemo watoto wanane wameuawa usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Buhare, nje kidogo ya mji wa Musoma mkoani Mara.
Watu waliouawa ni wa familia tatu, wanane kati ya hao ni wa familia moja akiwemo mume, mke, na watu wengine sita.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Robert Boaz, amezitaja familia zilizokumbwa na maafa hayo kuwa ni za Kawawa Nyarukembe iliyopoteza watu wanane, Morice Mgaya imepoteza watu sita, na familia ya Mgaya Nyarukembe imepoteza watu watatu akiwemo mke wa mwenye nyumba.
Kamanda Boaz amesema, watu wasiofahamika walizivamia familia hizo saa sita usiku, wakavunja milango ya nyumba na kuwashambulia wanafamilia kwa silaha zenye ncha kali.
Miongoni mwa waliouawa ni wanawake 11, wanaume sita, watano kati ya marehemu ni watoto wa kike, na watatu ni watoto wa kiume.
Polisi wanahisi kuwa mauaji hayo yamesababishwa na kisasi.