11 akiwemo anayesaka ubunge Simanjiro wakamatwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali Mererani

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Katika hali isiyo ya kawaida wakazi 11 wa eneo la Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wamekamatwa kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali uliolenga kufanya kampeni za ubunge kinyume na utaratibu.

Watu hao wakiongozwa na kada wa Ccm anayetajwa kugombea ubunge katika jimbo la Simanjiro mkoani humo,Kiria Laiser walikamatwa ndani ya kitongoji cha tanesco na kisha kufikishwa mbele ya kituo cha polisi cha Mererani.

Mbali na kukamatwa watu hao walikuwa wamekusanyika kwa lengo la kufanya kampeni za kuwania ubunge wa jimbo la Simanjiro kimya kimya kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu za uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa kitongoji cha Tanesco ,Justin Sarakikya alisema kwamba watu hao walikamatwa kwa kosa la kuitisha mkusanyiko usio halali .

Mwenyekiti Huyo alisema kwamba watu hao wakiongozwa na Kiria walikamatwa juzi wakati serikali ikiwa tayari imeshapiga marufuku mikusanyiko kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa corona hapa nchini.

Sarakiya,alisema kwamba mara baada ya kupigiwa simu alifika eneo hilo na kuwakamata watu hao kwa msaada wa wananchi wa eneo hilo na kisha kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

"Hiki kipindi sio kipindi cha mikusanyiko lakini pia sio kipindi cha kampeni naomba hili lieleweke hili jimbo lina mbunge na muda wa kampeni bado" alisema Sarakikya

Mkazi wa eneo hilo,Sokota Mboya alisema kwamba baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakifanya kampeni za chini kwa chini kinyume na utaratibu na kukiomba chama tawala cha Ccm kuwachukulia hatua za kinidhamu.

"Hiki sio kipindi cha kufanya siasa kabisa muda wa kampeni bado haujafika tunaomba cha chetu kiwachukulie hatua za kinidhamu" alisema Mboya

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara,Zephaniah Chaula hakuweza kuthibitisha au kukanusha juu ya taarifa hizo lakini alikemea suala la baadhi ya watu kufanya mikusanyiko na kusisitiza ni marufuku.

Hatahivyo,alisema kwamba muda wa kampeni za uchaguzi bado na kuwasihi wanasiasa kuacha kupita katika baadhi ya maeneo kufanya kampeni za chini kwa chini.

MwishoView attachment 1427824
IMG_20200423_134855_557.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom