101 Motivational Quotes

Mheshimiwa Dr. W. Slaa,

Nimewahi kusema hapo nyuma kuwa katika mila na desturi zetu tulikuwa na vigezo viwili tu vya kumpata KIONGOZI. Either alirithi au alitia fora kwenye mapambano mpaka akakubalika. Lililotakiwa kwa hawa wote ni kuwa wawe shupavu na wasiwe waoga. Ukiacha Hayati Mwl. J. Nyerere hatujaweza kumpata kiongozi mwingine yeyote mwenye sifa kwa mojawapo ya vigezo nilivyovitaja.

JF ni uwanja wa majadiliano wa jinsi ya kulinda na kutetea maslahi ya Taifa letu bila kujali rangi, kabila, jinsia, chama wala elimu kwani kwa JF - ni nchi kwanza. Ukweli ni kwamba nchi iko njia panda na kiongozi shupavu anatakiwa. Tuungane tuiokoe Tanzania. Karibu Mheshimiwa.







.
 
Nakumbuka nilipoingia Bungeni Mshahara wa Rais bado haukuwa siri, sielewi ni kitu gani kimetokea.

...Waliobahatika kufika Zambia, Mauritius, India wanafahamu mfumo wa Bajet ulivyo 'simple' lakini very Transparent wenye kuruhusu Bunge kwa niaba ya Wananchi kusimamia.
Mathalan, Safari za Rais zinajulikana ni ngapi za mwaka, zikitokea za ziada, zinaelezwa ni zipi na kwanini ili kupata idhini ya Bunge kwa fedha zilizotumika ambazo hazikuidhinishwa na Bunge. Kwetu ukiomba hiyo ni sawa na uhaini.

...Watanzania tunahitaji kuwa macho katika kulinda rasilimali zetu. Fedha zinazoidhinishwa na hivyo kukusanywa kutoka kodi zetu ni nyingi sana. Ni lazima tuwe wakali katika kuzilinda ipasavyo, alimradi tunafuata taratibu za kawaida za Transparency. Tuko mbali sana na lengo hili. Kwamba hatukufika leo haina maana kuwa hatutafika na au tusipige hatua ya kwanza kuelekea huko. Inahitaji moyo.








.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom