100 days without Ben Saanane

Noel Shao

Member
Jan 19, 2017
89
185
Cheo ni Amana, na dunia ni sehemu tu ya matembezi kwa ajili ya binadamu.

Wako wapi wakina Mobutu Seseko Kuku Mbaga wa Zambega? Aliyekuwa mbabe pale Zaire, alikufa hata wacongo hawakutaka kuona hata mwili wake. Yu wapi Yule katili Nduli IDD Amini, alifia uarabuni na Waganda walikataa kuona hata mwili wake! Madikteta wote katili tulisha wazika! Na hao wakina Adolph Hitler, Mussolini, Bokasa n.k
Hesabu yetu itatolewa baada ya maisha ya hapa ulimwenguni! Kila mtu ataenda katika himaya yake baada ya kifo.

Tuishi vema na watu wote, chuki, visasi, husuda, ubwana, ufedhuli, n.k siyo vitu vya kutukuza.. Tuwe vielelezo kwa matendo yetu mema....

[HASHTAG]#100dayswithoutBen[/HASHTAG]
[HASHTAG]#siku100bilayaBen[/HASHTAG].
 
Kwa hiyo wanakufa madikteta tu?

Taja watakatifu wa zama za Hitler wanaoishi tuone.
 
Amepotezwa Kama Alphonce Mawazo,ukiwa ccm lazima uwe mchawi,hawa jamaa mikono Yao inanuka damu,wewe angalia wanavyomsotesha Lema ndani kisa alimtaja mungu wao abadilike imekuwa kosa,ccm ni janga !
 
Ni huzuni sana kwa familia yake pamoja na makamanda wote wa Chadema. Lkn ukweli tunakataa kuusema, kilichompoteza Ben ni hiki:

"........ hakiki PhD yako "

Lakini Mungu hapendi, na atamlipa kila mwanadamu kwa kadri ya matendo yake.
 
"Dunia imekua mahali hatari zaidi pa kuishi. Si kwa sababu ya kuwepo kwa watu waovu, ila kwa sababu wapo watu wema lakini hawachukui hatua zozote dhidi ya uovu"

100DaysWithoutBen
 
duniani kuna mambo yanashangaza sana hivi mtu mzima kama ben anawezaje potea miezi mitatu bila kuwa na taarifa yoyote kweli?.haiingi akilini hata kidogoo.

nikuombe muheshimiwa mwigulu ukiwa ndo waziri mwenyedhamana na ulituambia kwamba ben ni swahiba wako wa karibu angalau utupe mrejesho,maana ulituahidi hapa jukwaani kua unafuatilia kwa ukaribu swala la ben.mimi binafsi siamini kua vyomba vya usalama vimeshindwa kupata taarifa zozote juu ya ben.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom