Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,978
- 5,025
Nimerudi tena! Niliwahi omba ushauri wa mdogo anayetaka kusoma sua nikapewa. Nashukuru Mungu dogo naye kafanya mambo mazuri hivyo ushauri wenu utafanya kazi. Sasa hivi nina mwingine wa kike kapata moja ya point nane na siku zote anasema anapenda kusoma sheria. Atapata? Sijacheki matokeo shule zingine za art kulinganisha kama competition itakuwaje. Aanze na chuo gani kujaza ili apate? (naamini vyuo vyote siku hizi vimeingiliwa na siasa na ubora wa udsm wa enzi hizo wameshauua ndo maana siulizi chuo kipi bora). Nashukuru kwa ushauri wako.