1,000,000 >>>50MPs Zanzibar :40,000,000>>>>189MPs Bara

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wengi mno ukilinganisha na idadi ya watu katika kisiwa hicho.

1,000,000/50=20,000
40,000,000/189=211,640!

211,640/20,000=10.586. Ikiwa na maana kuwa wastani wa watu katika jimbo moja la Tanzania bara ni sawa na majimbo zaidi ya 10 ya Zanzibar.
 
Ulitaka iweje au hoja yako ya msingi hapa ni ipi?
 
Tulikwisha sema tangu zamani Zanzibar ni kisiwa cha Viongozi - ukitaka uongozi chap chap hamia Zenji
 
Hasara kwa taifa. Zanzibar wabunge 4 wangetosha: 1 pemba na 3 Unguja. Dawa kuchinja Muungano
 
Muungano ni vema uwepo lakini uwiano wa uwakilishi ndipo shida ilipo! Watanganyika tunatkiwa ku query hili
 
naona sasa watanganyika wameamka big up kwa mwanzisha mada wanavuna pasipo kupanda hawa na mbaya zaidi hawaendelezi kwao nilikwishasema zanzibar kuna siri iliyofichika kata za tanganyika zanzibar ni jimbo vigezo gani wametumia hawa mafisadi!
 
Wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wengi mno ukilinganisha na idadi ya watu katika kisiwa hicho.

1,000,000/50=20,000
40,000,000/189=211,640!

211,640/20,000=10.586. Ikiwa na maana kuwa wastani wa watu katika jimbo moja la Tanzania bara ni sawa na majimbo zaidi ya 10 ya Zanzibar.
Mkuu hata sikuelewi, Marekani ina watu zaidi ya millioni 250 unafikiri ilihitaji wabunge wangapi?
 
Sioni tatizo maana hata hawa wa bara hakuna la maana. Ni bora tu turudishe majimbo machache ya zamani
 
Mkuu hata sikuelewi, Marekani ina watu zaidi ya millioni 250 unafikiri ilihitaji wabunge wangapi?

Marekani watu 250 milioni china zaidi ya 1000milioni??????????????????????????
hapa tunaongelea Tanzania na mstakabali wa Tanganyika.
 
Hivi waliokwenda Zanzibar kubadili matokeo saa nane za usiku ni akina nani ,na walitaka watu wapigane wakatae matokeo lakini wapi,mipango ilikwisha onekana mapema ssana ,wamepigwa na chini ,na sasa watu hao wanaondoka kwa gear kubwa Maraisi watatu .:yield:
 
Hili suala ni zito na lina utata mkubwa sana hususani unapozungumzia maslahi ya taifa kwa ujumla. Haingii akilini pale penye mwakilishi kutoa pia mbunge, hali hii inaleta maswali mengi sana kuhusiana na aina ya kazi anazofanya mwakilishi na mbunge na pia uwezekano wa kuingiliana kazi.

Kuna baadhi ya wabunge wa Zanzibar wanaingina bungeni kwa kupigiwa kura na watu wasiozidi 2000 ilihali huku Bara hiyo ni idadi ya watu katika kijiji kimoja tu. Siwalaumu Wazanzibari kwa kupata uroda huu maana hakuna mwanadamu akataye ubwete

Lakini haya ndio matunda ya katiba mbovu na watawala ambao wako tayari kugawa "peremende" kwa yeyote yule ili mradi waweze kuendelea kutawala.

Ingefaa kama ni wabunge kila mkoa wa Zanzibar utoe mbunge mmoja tu.
 
Hii ni hoja na nilikwisha wahi kupambana na Prof. Ali Mazrui kupitia gazeti la Nation mwaka 1994. Hakuna sabsbu yoyote ile ya msingi kwa Zanzibar kuwa na wawakilishi wengi si tu katika bunge la muungano bali pia katika baraza la wawakilishi. Huu ni utapanyaji wa raslimali za nchi.

Hoja ya kuwa Zanzibar iwakilishwe kikamilifu katika bunge la muungano haiendani na kuwa na utitiri wa wabunge. Kwa kigezo kuwa mbunge wa kuchaguliwa awakilishe walau watu laki moja na nusu hadi mbili Zanzibar ilitakiwa iwe na wabunge sita. Ukilegeza kigezo hicho na kusema basi iwe na uwakilishi wa kutosha wabunge wake wasingezidi 20. Na kwa vile wanatokea katika sehemu moja ya muungano basi mamlaka yao kikatiba yangebakia yale yale kama yalivyoainishwa kwenye Katiba. Hivyo wanakuwa na uwakilishi unaofaa na nguvu kamili. Ikimaanisha kwamba kama muswada unatakiwa kupitishwa na idadi fulani ya wabunge kutoka Zanzibar basi idadi au asilimia hiyo inapatikana kutokana na wabunge hao wa Zanzibar. Sasa suala hili la kuwa na mbunge mmoja anawakilisha watu elfu nne ni kitu ambacho hakiingii akilini hata kidogo. Kama walitarajia kuwa Wazanzibar watanyamazishwa kwa kupendelewa na kuwa na watu wengi bungeni hilo wamenoa. Huwezi ukamnyamazisha watu kwa kuwapa upendeleo kwani kesho wale walioupata upendeleo huo wanaamini kabisa kuwa ule haukuwa upendeleo bali haki yao.

Kwa mfano hapo Marekani Jimbo dogo la Delaware lina mjumbe mmoja tu (idadi ya watu ni 885,000) katika Baraza la Wawakilishi. Na jimbo la Hawaii lina wawakilishi wawili wakiwawakilisha watu 1,295,000. Ni wazi kuwa kuna haja ya kupanga upya kabisa idadi ya wabunge kutoka Zanzibar. Vilevile kuna haja ya kuangalia majimbo mengine bara ambayo yalimegwa kwa ajili ya kuwalinda wanasiasa fulani na kukomoa vyama vya ushindani. Haya ni kama majimbo ya Hai na Sia pamoja na ya Singida Mashariki na Kaskazini. Ni lazima tuwe watu makini na tusitapanye pesa zetu kwa ajili ya kutaka kupata sifa au kuwatuliza watu fulani kwani kiu yao ya kupata zaidi haitakwisha.
 
Dawa ni kupunguza idadi ya majimbo ya zanzibar, wanakula kodi zetu hovyo.

kwa hiyo zanzibar wanatunyonya?kama wanatunyonya wanatunyonyaje hali ya kuwa wao wanategea TANZANIA na sisi ndo baba na mtoto humohumo
 
Hili suala ni zito na lina utata mkubwa sana hususani unapozungumzia maslahi ya taifa kwa ujumla. Haingii akilini pale penye mwakilishi kutoa pia mbunge, hali hii inaleta maswali mengi sana kuhusiana na aina ya kazi anazofanya mwakilishi na mbunge na pia uwezekano wa kuingiliana kazi.

Kuna baadhi ya wabunge wa Zanzibar wanaingina bungeni kwa kupigiwa kura na watu wasiozidi 2000 ilihali huku Bara hiyo ni idadi ya watu katika kijiji kimoja tu. Siwalaumu Wazanzibari kwa kupata uroda huu maana hakuna mwanadamu akataye ubwete

Lakini haya ndio matunda ya katiba mbovu na watawala ambao wako tayari kugawa "peremende" kwa yeyote yule ili mradi waweze kuendelea kutawala.

Ingefaa kama ni wabunge kila mkoa wa Zanzibar utoe mbunge mmoja tu.

Jamani msisahau kama Zanzibar ni nchi na hata kama wako 100,000 hili linabakia vile vile...Tuangalie kule UN kwanini zile nchi zenye idadi kubwa ya watu bado zina kiti kimaja kama nchi zenye idadi ya watu kidogo...
 
Back
Top Bottom