09 Dec, 2019: Maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

Siasa bhana.....! Nikikumbuka matusi, kejeli na dhihaka za wanaCcm kwa Edward kipindi kile nachoka kabisa! Wengine walimtabilia mpaka kifo! Kweli maendeleo hayana chama!
Na wale waliosema kwa miaka nane kuwa lowasa mwizi, fisadi, hana adabu, achomwe moto, azomewe, mvi zake zingekuwa na busara angemwambia mkwewe aache ushoga sababu alitoboa sikio, hafai kupewa hata ukatibu kata. Kisha wakampa tiketi ya urais na kumuombea kura unawazungumziaje?
 
Naangalia maadhimisho ya sherehe ya miaka 58 ya Uhuru, Kuna kikundi cha sungusungu kwa kweli wamevaa kichawi kabisa na matendo yao hata hayaeleweki.
Bila shaka hawa ndio wale elfu moja waliosema watamroga mtu yeyote atakayetaka kushindana na Magufuli.
Imagine 2019.
Halafu waku makofi kwah kwah kwah
 
Duuh labda Mulungu tu,kwa lugha ya Malawi ni Mungu, kwa Wandali wa Ileje hiyo ni surname ya watu (ukoo)...... kama ni matusi ubarikiwe sana
Nimekutakia mwisho mwema wa mwaka na Mungu akulinde ukipende kisukuma Mjomba, nahmala ni mjomba kwa kisukuma au unataka niwe bagheshi wako?
Bagheshi ni shemeji
 
Naangalia maadhimisho ya sherehe ya miaka 58 ya Uhuru, Kuna kikundi cha sungusungu kwa kweli wamevaa kichawi kabisa na matendo yao hata hayaeleweki.
Bila shaka hawa ndio wale elfu moja waliosema watamroga mtu yeyote atakayetaka kushindana na Magufuli.
Mbavu zangu jamani. Kilangila.
 
kila mwaka nasikia kauli mbiu yetu ni ileile ya miaka ya 1960... 70. ya "tutalinda muungano wetu"

Naamini kwa sasa tuko matured enough kuanza kuongelea "kulinda maslahi yetu kama Taifa".
 
Hazikuwa sherehe za uhuru bali zilikuwa mbinu za kumhakikishia jpm muhula wa pili!ndo mana kikwete hakuwepo MEMBE NDO IVO TENA BYE BYE!!!
 
Mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa wanaosamehewa. Amesema, kwenye mkoa huo amesamehe wafungwa 713, Dodoma wanasamehewa 385, Morogoro 365, Dar es Salaam 293, Mara 260, Mbeya 259, Kigoma 252, Tanga 245, Geita 230, Rukwa 214, Arusha 208, na Manyara 207.
Kilimanjaro karanga hawapo kwenye list! Kati ya magereza makubwa Tz hakuna!! Maana yake nini? Nijuzeni!
Kanda ya ziwa kote wamo!!??
 
stakehigh,
JESHI LA TANZANIA LILITAKIWA LIONYESHE MAMBO YALIYO KWENYE UWEZO WAO, HAWAJAWAHI KUMUOKOA MTU ALIYETEKWA NA GAIDI WANAWEZAJE KUSEMA NI RAHISI? UNAWEZAJE KUJUA KITU NI RAHISI KWA MAZOEZI TU? HUU NDIO UONGO USIOFAA. INGAWA HAKUNA UONGO UNAOFAA.
 
Jumla ya *Wafungwa 293* kutoka magereza Ya *Ukonga, Keko,Segerea na Wazo Hill* jijini Dar es salaam leo wameachiwa huru kwa *Msamaha wa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli* alietoa Msamaha kwa *Wafungwa 5,533* waliokuwa wakitumikia kifungo kwenye magereza mbalimbali Nchi nzima.

Wafungwa hao wameachiliwa huru leo Mbele ya *Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Abubakar Kunenge, Kamanda Wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam* ambapo Kwa pamoja wamewataka walioachiliwa huru kwa msamaha wa Rais kuhakikisha *hawarudii kufanya makosa.*

Kwa mujibu wa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam *Kamishina Msaidizi wa Magereza Julius Mtambala* amesema kati ya Wafungwa hao 293 walioachiliwa huru *130 wanatoka Gereza la Ukonga,54 Gereza la Keko, 74 Gereza la Segerea na 35 wanatoka Gereza la Wazo hill.*
 
Back
Top Bottom