09 Dec, 2019: Maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

1576044385413.png



KAMPUNI ya Ndege la Tanzania (ATCL) imenogesha maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, zilizofanyika jijini Mwanza, kwa kuhakikisha huduma ya usafi ri inapatikana hadi usiku. Aidha, ATCL imeongeza safari za ndege kwa mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro na Kagera, ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha abiria wanaokwenda maeneo hayo hawakosi usafiri wakati huu wa msimu wa sikukuu.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema katika sherehe za Uhuru wa Tanzania zilizofanywa jana mjini Mwanza, ATCL ilitoa huduma za usafiri wa abiria kwa kuongeza ndege moja ya ziada.

“Tunaongeza ndege kwenye ruti ya Mwanza, Bukoba na Kilimanjaro kwa sababu msimu huu ni wa abiria wengi hasa wanaokwenda makwao kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka, lakini pia jana kulikuwa na tukio kubwa la maadhimisho ya Uhuru, tuliongeza ndege moja ya ziada kwa ruti ya usiku jana (juzi) kutokana na uhitaji wake na leo (jana) usiku pia tumeongeza ruti nyingine ya kwenda na kurudi Dar,” alisema Kagirwa.

Akifafanua, Kagirwa alisema ruti ya kwenda Mwanza na Bukoba, ina ndege tatu kwa siku na kwamba kwenye sherehe za Uhuru, ruti zote zilijaa na ikaongezwa ndege nyingine ambayo ilisafiri usiku wa juzi. Alisema kwamba ATCL itaendelea kuangalia mahitaji ya wateja na kuongeza ndege pale inapobidi.

Akizungumzia mahitaji ya usafiri huo msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya, Kagirwa alisema kwa ruti ya kwenda Bukoba, abiria ni wengi, akitol mfano kuwa familia moja inaweza kuomba kuwekewa nafasi za watu 15. “Msimu huu wa sikukuu abiria ni wengi na sisi tumejipanga kuhakikisha wateja wetu hawakosi usafiri, tumeongeza ndege moja kwenye ruti ya kwenda Bukoba kwa ndege inayopita Mwanza kwa sababu familia moja inaomba kuwekewa nafasi hata 15, za kwenda Bukoba, sasa utaona mahitaji ni makubwa,” alisema Kagirwa.

Mbali na kuongeza ndege kwenye ruti ya Bukoba, pia kwenye ruti ya Mwanza inayofanya ruti tatu kwa siku, nayo imeongozwa ndege moja, na ruti ya Entebbe kupitia Kilimanjaro ina ndege tatu zinazoruka asubuhi, jioni na usiku. Alisema abiria wanaotumia usafiri huo wa ATCL wasiwe na wasiwasi, kwani huduma zimeboreshwa na hakutakuwa na shida ya usafiri, kwa sababu wamejipanga kutoa huduma kwa ruti zote kwa kuzingatia wingi wa watej
 
Huyu mtoa thread ni msemaji wa serikali sijui , jamaa inaonekana halali , usiku na mchana anapost mambo inayofanya serikali, huenda ametengewa fungu special Kwa ajili ya kutoa taarifa jamii forum
 
Huyu mtoa thead ni msemaji wa serikali sijui , jamaa inaonekana halali , usiku na mchana anapost mambo inayofanya serikali, huenda ametengewa fungu special Kwa ajili ya kutoa taarifa jamii forum
Wewe muache lakini pokea taarifa
 
Huyu mtoa thead ni msemaji wa serikali sijui , jamaa inaonekana halali , usiku na mchana anapost mambo inayofanya serikali, huenda ametengewa fungu special Kwa ajili ya kutoa taarifa jamii forum
Tatizo lako ni lipi sasa?
 
Tatizo lako ni lipi sasa?
Kwa hiyo wewe umesoma reply yangu huku lengo lako kuu ni kutaka kujua tatizo langu liko wapi , nakushaur rudia tena kusoma reply yangu bila kuwa na mlengo wowote , utanielewa nilimanisha nn
 
Kitu nimegundua Bukoba/ Kagera na Moshi/ Kilimanjaro ndiyo mikoa inayoongoza kuwa na wasafiri wengi/ wateja wengi wa usafiri wa ndege. Na pia ndo wanaongoza kwenda makwao elivina shambuni,
 
Ni mpango wa kishamba sana ! Halafu hawajifunzi tu , walipomtoa Babu Seya walidhani ingewabeba lakini matokeo yake ikawa sifuri
 
Tutaona mengi awamu hii.Wafungwa kwenye awamu zilizopota waliachiwa kwa kutangazwa idadi tu ,this time na sura zao zinaonyeshwa kupokelewa na ma DC au RC jamani Tanzania tutashangaa mengi
 
Siasa unazozioona zinafanywa na hao waliopewa msamaha wakisaidiana na ndugu na jamaa zao baada ya kuzidiwa na furaha.

Rais ametoa agizo la watu hao kuachiwa mapema na bila kubughudhiwa na mtekelezaji wa agizo Hilo moja kwa moja ni DC na RC na agizo Hilo lisipokelezwa kwa matakwa ya mtoa agizo ,ni ma-RC na ma-DC ndio wataulizwa

Hiyo ni kazi ya jeshi la magereza; uwepo wa dc, RC ndiyo siasa yenyewe. Hizi ndizo populist politics alizozungumzia Mzee Mkapa kwenye kitabu chake.
 
Back
Top Bottom