Tamko: CUF yaipa ZEC siku tatu kukamilisha mchakato wa uchaguzi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
attachment.php

attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • 12063529_1203947952965000_3104171369968466737_n.jpg
    12063529_1203947952965000_3104171369968466737_n.jpg
    74.3 KB · Views: 3,652
  • 10885198_1203948002964995_6517304857885241932_n.jpg
    10885198_1203948002964995_6517304857885241932_n.jpg
    69.3 KB · Views: 3,483
  • 12193546_1203948546298274_2285623473645913544_n.jpg
    12193546_1203948546298274_2285623473645913544_n.jpg
    46.4 KB · Views: 3,481
Hapa ccm hatuwezi kucomment kwani zanzibar najua maalimu aliishashinda. Tunasubiri kikwetwe atuokoe ccm upande wa zanziba ili maalimu asiapishwe
 
Ule usemi kuwa Zanzibar ilipatikana kwa damu na haiwezi kutolewa kwa karatasi nadhani sio muda wake. Tubadilike kifikra na tuangalie mustakbali wa Taifa letu. Nakupongeza Maalim Seif Sharifu Hamad kwa kutafuta haki kwa njia ya amani. Nikuombe pia kuwa usikate tamaa na kuwaachia wananchi watafute haki hiyo. Wewe ni muhimili mkuu katika utengamano wa kitaifa. Kampeni umefanya na Dr. shein pia kafanya. Tumewasikia. Huu sio muda wa kampeni. Ni muda wa kutafuta Muafaka. WAZUNGUMZAO HAWAGOMBANI. Kokote mtakapotupeleka tutaridhia ikiwa mna lengo zuri. Kuwa na subira na subira huleta haki. Wazinzibari wamechukizwa na Kufungwa kwa dhulma masheikh wao ndio maana wakaikataa CCM licha ya mazuri kufanyika. Anzieni hapo na muwatoe Masheikh ndipo muendeleze mazungumzo.
 
Hapa ccm hatuwezi kucomment kwani zanzibar najua maalimu aliishashinda. Tunasubiri kikwetwe atuokoe ccm upande wa zanziba ili maalimu asiapishwe


Mimi nakuona kama vile hujielewi.. sasa kama mtu ameshinda ya nini asitangazwe...yani unataka kuleta siasa za kibabe??
 
Haki haina mwenyewe,haki ni haki haina kabila dini au taifa Maalim kashinda kwa kishindo Zanzibar ishakuwa nongwa ZEC hawataki kumtangaza mshindi.

Siasa za Zanzibar wanazijua wazanzibar wenyewe!
 
Siasa za Zanzibar wanazijua wazanzibar wenyewe![/]

Hapana unakosea. Zikatae hizo fikra, usikubali zikutawale hasa wakati huu tulio nao ambao kudhulumiana haki imekuwa desturi na hakuna anayeshangaa. Wenye mamlaka wanajipa haki hata ambazo hawastahili wanaturudisha tulikotoka kwa speed ya supersonic, wanaturudisha enzi za ujima. wanajiona wana divine rights. Wamepotoka, wamepotoka kiasi kwamba wanaona ila hawajui kama wanaona. Lakini watambue siasa za wazanzibar kamwe hazitoachwa kwa wazanzibar peke yao. Kila kinachoendelea Zanzibar kinatuathiri moja kwa moja. Saa ya ukombozi yaja, yaja tena kwa kasi na hakika saa hiyo itakapofika wanyonge watajitwalia madaraka, watashika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii na hawa akina January makamba watagundua zama zao zimepita, watalia na kusaga meno, watatamani nyakati zirudi nyuma lakini hukumu itapita juu yao kwa maana hajutokuwa na namna nyingine.
 
Matamshi haya ni ya ajabu sana,"Kikwete awasidie Maalim aasiapishwe?"Hizi ni siasa za kibabe.Kwa hiyo CCM haijawahi kukubali multipartism kama ilivyojidhihirisha hata bara si ndiyo?Hipocrites.Time will tell what will become of Tanzania.

Yaani bila aibu Maalim ananyang'anywa ushindi wake hivi hivi.Mimi nadhani tuitishe kura ya maoni wananchi waamue wanataka mfumo upi,chama kimoja au vyama vingi.Kuendelea kinyemela namna hii haikubaliki.
Hapa ccm hatuwezi kucomment kwani zanzibar najua maalimu aliishashinda. Tunasubiri kikwetwe atuokoe ccm upande wa zanziba ili maalimu asiapishwe
 
Uhalali wa Tanzania kutatua migogoro nchi nyingine upo wapi wakati wanashawishi kitu wasichokiamini?umeshindwa kuruhusu demokrasia ya kweli halafu unataka mataifa yaige toka kwako,kweli wakongo watatushangaa na kagame atatuona mazuzu fulani.
 
Habari za ladies & gents,

Urais wa JMT ndio umekwisha na katiba hairuhusu matokeo kuhojiwa tena, kwa kifupi ukawa tumeshapoteza sasa ni kuganga yajayo. Nasikitika sana.

Lakini hayo yote yakitokea huku bara, kule znz hali ni tete baada ya maalim kuelekea ushindi na tume kusitisha utangazaji matokeo. Hali inauma sana hasa ukizingatia maalim kashinda chaguzi zote za nyuma na safari hii pia.

Kwa kuwa ukawa lengo ni kutawala znz na bara, nafikiri ni wakati sasa Mbowe na timu yake kuwekeza nguvu znz na kumsaidia Seif kupata haki yake, manake tangu mgogoro huu umeanza sijasikia Ukawa wakitoa tamko lenye nguvu kuhusu znz,.najua waliongea kwa uchache tu kuhusu uhalali wa kura za jmt zilizopigwa znz. Tuyaache hayo na sasa ukawa wapigane kutafuta haki ya Maalim.

Nawaomba Mbowe, Mbatia, Lowassa, na viongozi qoye waandamizi wakatie nanga znz kushinikiza kutangazwa mshindi.

Cheers.
 
CCM & co wameshajichanganya huko Zenji....

Subiri Nov 2 ndio utawajua Wazenji walivyo na uchungu na nchi yao sio kama manyumbu 'wadanganyika'
 
sakata la kufuta matokeo ya uchaguzi visiwani zanzibar limechukua sura mpya baada ya mgombea wa urais maalim seif sharrif hamad kusema hata kubali kuporwa ushindi.mgombea huyo ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais katika serikali ya umoja wa kitaifa visiwani zanzibar,pia ameitaka tume ya uchaguzi znz{ZEC)kuendelea kuhesabu matokeo katika majimbo yaliyobakia,kadhalika maalim ameonya kuwa kufikia kesho(nov 1)endapo mwenyekiti wa ZEC jecha.s.jecha ataendelea za msimamo wake wa kufuta uchaguzi na kupuuza msimamo wa wananchi kupitia sanduku la kura basi yeye na viongozi wenzake wa CUF na UKAWA kwa ujumla watajiweka kando katika kuwazuia wananchi na hatua yao ya kudai haki yao ya kidemokrasia,"chaguzi nne nimeibiwa matokeo kama shein ameamua kung'ang'ania madaraka safari hii sikubali,sikubali,sikubali"alisema maalim seif source:bongo blogs
 
Back
Top Bottom