Edward Lowassa aongea na vyombo vya habari, Amesema hatokubali matokeo ya uchaguzi mkuu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Mgombea Urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA, leo saa 4:30 asubuhi anazungumza na vyombo vya habari vya hapa nchini na vya kimataifa.


Katika mkutano huo anatarajia kutangaza maamuzi magumu kuhusu mchakato wa matokeo ya urais yanayoendelea sambamba na kile kinachotokea Zanzibar sasa.

Mkutano unafanyika Ngome.

attachment.php



Ndugu waandishi wa habari;


Tumewaita hapa kuwaomba muwaeleze Watanzania wenzetu, jumuiya ya kimataifa na marafiki zetu wengine ndani na nje, kwamba hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kote nchini.

Hii ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya wananchi.

Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli.

Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa.

Kwa mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na Mtambile, kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma, Same Mashariki, Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, siyo kura za uchaguzi mkuu wa rais. Tunaweza kuiita, ?mzimu wa uchaguzi.?

Ndugu waandishi wa habari;

Tangu kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ? mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya rais,Hata hivyo, Tume imeendelea kutangaza matokeo hayo, bila kujali kile ambacho tumekieleza na kukilalamikia, kana kwamba tunachokisema ni ujinga, uzushi na uwendawazimu. Hili halikubaliki.

Aidha, katika maeneo mengine, likiwamo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyoko mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi, yanatofautiana na yale ambayo yamekusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo.

Hali kama hiyo ipo pia katika majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA na wale wa vyama washirika vya CUF na NCCR ? Mageuzi, ama wamekuwa na nguvu kubwa au wameibuka washindi.

Upo ushahidi wa wazi ambao, ninyi waandishi mnaweza kwa kutumia uandishi wenu kuuthibitisha kwamba, katika majimbo yote ambako wagombea wa UKAWA wameshinda, TUME imechelea kutangaza matokeo ya urais kwa sababu zinazothibitisha kuwapo kwa mikakati ya hila.

Ikumbukwe kwamba matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada tu ya Jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabia kura na kuwakamata wataalam wetu waliokuwa wakipokea matokeo ya kura za rais nchi nzima ambayo hadi uvamizi huo ulipofanyika tulikuwa tukiongoza katika maeneo mbalimbali.

Ndugu waandishi wa habari;


Tunaamini kwa dhati kwamba, uvamizi huo ulifanyika mahususi kwa malengo ya kufanikisha uchakachuaji huo ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa sasa na NEC.

Wakati tukijua kwamba NEC ndiyo mamlaka pekee ya kisheria ya kutangaza matokeo ya urais, tunapenda kuwataarifu Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati uvamizi huo ulipofanyika kura zetu za urais tulizokuwa tumezikusanya zilikuwa zikionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60.

Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na watendaji wa NEC, mimi Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, tunautangazia umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC.

Ndugu waandishi wa habari;


Kutokana na makosa hayo makubwa, tunaitaka NEC kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo ya urais na kuanza upya kufanya uhakiki wa kile wanacholetewa na wasimamizi wa majimbo ambacho ushahidi unaonyesha kuwapo kwa vitendo vya hila ambavyo vinafanywa na NEC.

Ndugu wana habari


Kile kinachofanywa na NEC hapa ndiyo kile kile kinachoendelea kufanywa kule Zanzibar leo na ZEC ambako kunafanyika juhudi kubwa na za makusudi kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa wazi wa ushindi wa Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF anayeungwa mkono na UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad.

EDWARD LOWASSA
MGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokraisa na Maendeleo (CHADEMA) aitaka tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) asitishe zoezi la kutangaza matokeo ya Urais linaloendelea. Alisema hayo katika mkutano wake mfupi na waandishi wa habari na kuongea kwa niaba ya muungano wa vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba, UKAWA.

Una maoni gani juu ya kauli hii ya UKAWA?
 

Attachments

  • Lowassa.png
    Lowassa.png
    38.3 KB · Views: 7,340
Watanzania sisi ni mazuzu sana tunaishia kulalamikia kwenye key bord tu, upuuzi huu utanedela vizazi na vizazi, kama hatutabadilka tusitarajie nidhamu ya Tume ya Uchaguzi, Nchi kama Kenya wana tume ya Uchaguzi yenye nidhamu ya kipekee, tuache kulalamika kwenye key bord jamani
 
The history of man is defined by war, and war by the man who fight it.
Hakuna nchi imewahi kuongozwa kwa haki bila kutumia nguvu kulazimisha haki.
Taifa letu halina viongozi, lina watawala.
uongo siku zote unajitenga na ukweli.
kuhubiri amani na kuwa na amani ni vitu viwili tofauti.
Tanzania hakuna amani, kuna uvumilivu tu.
Nyuma ya uvumilivu kuna nidhamu ya woga.
 
Watanzania wameshaamua, hayo mengine ni hisia zake ambazo hazina uhalisia.
 
Huyu mtu ana matatizo...labda atangaze matokeo ya majimbo yote yaliyotangazwa ili tuone tofauti na uongo wa Tume...nje ha hapo bado Urais anaona ni wake..
mmh mwanakijiji hebu fafanua hapa ,kwa sababu zanzibar tumesikia matokeo yale hapa bado yanaendelea ,mh lowasa ameamua aongee kupitia media tatizo lake liko wapi
 
Back
Top Bottom