Mbowe: UKAWA haitambui matokeo ya Urais yanayotangazwa na NEC

dos santos

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
256
128
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA mh Freeman Mbowe amesema hawatambui matokeo ya urais yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa madai ya kuhujumiwa.

Mbowe alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa ngome Kawe.

Aidha amelalamikia kukamatwa kwa vijana wa IT pamoja na raia wa kigeni ambao amesema hawahusiani na CHADEMA.

Mbowe ametumia muda mrefu kulalamikia kuvurugwa mfumo wao wa vijana wa IT.
Amesema hata CCM wamekuwa na vijana kama wa namna hiyo ambao wanakusanya matokeo na kuchakachua.
Kesho amesema watakutana kamati kuu ya CHADEMA, na pia viongozi wanaouda UKAWA.

============================


Viongozi waandamizi wa UKAWA wamesema hawayatambui matokeo ya Urais yanayoendelea kutangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC kwa madai kuwa yamehujumiwa



Kauli hizo za kutoyatambua matokeo zimetolewa na Freeman Mbowe,Profesa Safari na James Mbatia wakati wakiongea na vyombo vya habari leo kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu.


Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe amesema serikali ya CCM imeamua kuwatumia wakurugenzi,NEC na jeshi la polisi kupindua maamuzi ya wananchi na kuamua kutangaza matokeo ya uongo.


Mbowe ametumia muda mwingi kulilaumu jeshi la polisi kuwakamata Ma IT wa Chadema waliokamatwa wakijumlisha matokeo ya Lowassa jijini Dar es Saalam, huku professa Safari akieleza jinsi NEC ilivyochakachua matokeo....

"Nimesikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa vijana wenzetu Wataalamu Wenzangu wa IT waliokuwa katika vituo vya majumuisho ya kura za mgombea Urais UKAWA.

"Huu ni UONEVU dhahiri kabisa. Inauma zaidi kwa wao kunyimwa kabisa dhamana.Hii si HAKI.

"Sitaki kuamini tumefikia hapa,sitaki kuamini uonevu wa kiasi hiki unatendeka kwa manufaa ya kisiasa."
Amesema Mbowe



Katika tamko lake, Profesa Safari ametolea mfano jimbo la tandahimba ambapo amesema, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo,Magufuli amepewa kura 49,098 huku Lowassa akiambulia 46,288


Kwa mujibu wa Profesa Safari, matokeo halisi waliyoyakusanya toka kwa mawakala wao yanaonyesha kuwa Magufuli ana kura 44,253 huku Lowassa akiwa na kura 44,537


Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia amesema NEC watachakachua matokeo lakini sio hisia za wananchi.


Viongozi hao wa UKAWA wamesema kesho Oktoba 28 watakutana kwa dharura na kutoa msimamo wao kwa wananchi juu ya mwenendo wa uchuguzi mkuu

Chanzo Mpekuzi blog



 
Safari hii hakuna kuitwa ikulu kunywa juice, akatae akubali magufuli rais tu, lini walikubali matokeo?

Kuna kusindwa kihalali hilo linakubalika!! si kwa kura hizi za tume zinazofiki 108.94%,
Numbers don't lie idadi ya wakiga kura inatofautiana na mchanganuo kwa kura 10,000?? Tume itoe maelezo
Mzee wasira analalamika mchezo mchafu jimboni kwake sielewi anamlalamikia nani mabox ya kura yanalala halmashauri - mkurugenzi wa halmashauri ni mteule wa ccm hatujui wanayafanya nini mabox..
 
hao raia wa kigeni walitaka kuhack system ya NEC EEEEEEEEEH?Mbowe mmekomeshwa mlitaka mshinde kiunjanja janja Mungu kawaumbua,kova shikiria hao ma hackers segerea na keko mpaka Rais apatikane ndo muwatoe
Baada ya akili kukurudi utaifikiria tena statement ya Mbowe na athari yake.
 
Victoire, you are unconsciously talking a such virus advice to the Mr. Kova as a general police. Can't you recognise what bankruptcy this country undergoes in?
 
hao raia wa kigeni walitaka kuhack system ya NEC EEEEEEEEEH?Mbowe mmekomeshwa mlitaka mshinde kiunjanja janja Mungu kawaumbua,kova shikiria hao ma hackers segerea na keko mpaka Rais apatikane ndo muwatoe

ni watanzania cyo wa kigeni
 
Hvi hawa c ndo walisemaga hawamtambui jk,mwisho wa siku wakajipendekeza kwenda kunywa juice ikulu?
 
Back
Top Bottom