Dokta mimi siumwi huko

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
8,758
8,631
"Ulikwenda hospitali mke wangu?" Masofa alimuuliza mke wake Sulee.
"Nilikwenda, lakini daktari kasema mimba nitapata tu ndani ya mwezi mmoja."
"Ndani ya mwezi mmoja utapata mimba? Inawezekana kweli? Hujamwambia kwamba tumehangaika kutafuta mtoto kwa miaka nane, sasa ndani ya mwezi mmoja mimba itapatikana vipi?"


"Mimi sijui Masofa."
"Mh! Haya, kwa sababu tumeambiwa na mtu tunayemwamini tuangalie, labda kweli daktari yule atatusaidia. Hakusema uende na mimi?"
"Hakusema Masofa, ila alisema kama naweza kesho na keshokutwa niende usiku saa moja ili anipime vizuri."
"Alikupa dawa?"


"Dawa atanipa kesho."
Masofa alichukua simu akampigia rafiki yake Miraji...
"Ee bwana Miraji, yule dokta uliyemsema kasema ‘waifu' aende kesho saa moja usiku, wewe si unamwamini?"
"Yule hana neno, aende tu. Bwana Masofa we hukumbuki jinsi mimi na shemeji yako tulivyohangaika kutafita mtoto?"
"Nakumbuka."


"Sasa kama si huyo daktari wa wanawake unadhani tungepata mtoto?"
"Oke, nimekuelewa bwana Miraji."
"Sawa Masofa."
Masofa alikata simu, akaendelea kukaa chumbani. Akili yake ilikuwa nzito sana kumruhusu mkewe arudi hospitali kesho yake, tena usiku wa saa moja...
"Sasa huyo daktari wa watoto ni kwa nini anataka mke wangu arudi usiku? Ni tiba gani hiyo ya usiku wa saa moja?"
***


Siku ya pili iliingia, saa moja jioni Sulee alikuwa kwa daktari wa wanawake anaitwa Dokta Kisarawe.
Dokta Kisarawe alikuwa amekaa ndani ya chumba cha utabibu kwenye zahanati yake huku akimwangalia Sulee kwa macho yenye huruma...
"Kwa hiyo tatizo kubwa ni mtoto tu anti yangu?"


"Ni mtoto tu."
"Miraji unamjua?"
"Ndiyo, ni rafiki wa mume wangu Masofa kwani vipi dokta, mbona umemtaja huyo?"

Kwa hisani ya Global publisher tupate uhondo huu............

Wembe ni ule ule: Michepuko sio dili na usitafute sababu ya kuchepuka, unaposema unampenda jinsi alivyo uwe unamaanisha.

Tuwemoo tuone mambo ya dokta.............
 
DOKTA SIUMWI HUKO-2

ILIPOISHIA…
"Kwa hiyo tatizo kubwa ni Mtoto tu anti yangu?"
"Ni mtoto tu."
"Miraji unamjua?"
"Ndiyo, ni rafiki wa mume wangu Masofa kwani vipi dokta, mbona umemtaja huyo?"
IDODOSE MWENYEWE…
"Ah! Nimeangalia kwenye maelezo yako, nikagundua kuwa mnatoka eneo moja kwa maana ya ubalozi…," Dokta Kisarawe alijibu huku akimuangalia Sulee kwa macho ya kumkagua f'lani hivi.
"Ooh…!, maana nilishangaa ni kwa nini umuulize huyo na umejuaje kama ninafahamiana naye…," Sulee alihoji huku akiyakimbiza macho yake pembeni baada ya kukutanisha na ya Dokta Kisarawe.
"Hata mkewe alikuwa na tatizo kama la kwako, lakini aliponea kupitia mikono hiihii…"
"Kweli dokta…?"
"Kweli nakuambia, niamini mimi."
"Mm!, sawa lakini nimesumbuka sana kwani naumia kukosa mtoto jamani…," alisema Sulee safari hii akionesha sura ya upole zaidi, hali iliyomfanya Dokta Kisarawe amkazie macho zaidi.
"Kwani mmehangaika kwa muda mrefu sana anti…?"
"Yaani wee acha tu dokta, ikishindikana na hapa itabidi niridhike tu kuwa sikupangiwa kuzaa kabisa…"
"Ndoa yenu ina muda gani sasa…?," Dokta Kisarawe alizidi kumdadisi Sulee huku muda nao ukizidi kuyoyoma na tayari saa iliyokuwa ukutani ilisomeka saa mbili na dakika nne.
"Miaka mitatu sasa dokta…"
"Mm..!"
"Mbona unaguna dokta jamani, au huamini?"
 
DOKTA SIUMWI HUKO-3

ILIPOISHIA:
"Kwani mmehangaika kwa muda mrefu sana anti…?"
"Yaani wee acha tu dokta, ikishindikana na hapa itabidi niridhike tu kuwa sikupangiwa kuzaa kabisa…"
"Ndoa yenu ina muda gani sasa…?," Dokta Kisarawe alizidi kumdadisi Sulee huku muda nao ukizidi kuyoyoma na tayari saa iliyokuwa ukutani ilisomeka saa mbili na dakika nne.

"Miaka mitatu sasa dokta…"
"Mm..!"
"Mbona unaguna dokta jamani, au huamini?"
MALIZANA NAYO…


"Hapana anti, naguna kwa kushangaa mwanamke mzuri kama wewe hujapata mtoto…!," alijibu Dokta Kisarawe huku akimkazia macho Sulee hasa maeneo ya kifuani na mapajani kutokana na sketi aliyokuwa amevaa kupanda hadi kuvuka juu ya magoti.
"Kwani mimi mzuri ja..ma..ni…?," aliuliza Sulee lakini safari hii kwa sauti iliyokatakata.


"Dah! Wewe ni mzuri sana anti, nashangaa hadi sasa hujapata mwanaume wa kukupa mimba…!"
Hapo Sulee hakusema neno zaidi ya kuendelea kumtumbulia macho Dokta Kisarawe aliyekuwa bize na kumungalia.
Alipoona Sulee yuko kimya, Dokta Kisarawe akazidi kumsifia huku akimhakikishia ni lazima atapata mimba.


"Yaani mwanamke umeumbika haswa, ona maeneo kama haya ya kifuani jamani…," Dokta Kisarawe aliendelea kumchombeza Sulee huku sasa akionesha kwa vitendo na kuyagusa maeneo ya kifuani ya mwanamke huyo mrembo wa sura na umbo achilia mbali rangi yake ya chokoleti.


"Kwe…kwe…lii dokta jamani…?," Sulee aliuliza kama kweli anaweza kuzaa lakini kwa sauti ya mkwamo kutokana na mkono wa dokta kugusa maeneo nyeti ya kifuani.
"Duh! yaani anti na nido nzuri kama hizi halafu huzai…!"
"Mm!," Sulee aliishia kuguna huku akijikunja kiaina kwani safari hii vidole vya dokta viligusa kisawasawa nido zake kutokana na blauzi nyepesi aliyoivaa mwanamke huyo.


"Hujapata tu mwanaume rijali…"
"Kwa nini unasema hivyo dokta jamani…," Sulee aliuliza katika hali ya kutojiweza, huku macho yake yakianza kubadilika rangi na kuwa mekundu kiasi.


"Mimi ni daktari si kwa matokeo ya mtihani bali kwa kukidhi vigezo, ina maana nina uwezo wa kujua tatizo la mgonjwa hata kwa saikolojia tu, yaani wewe unahitaji mwanaume rijali tu, kweli tena nakuambia," Dokta Kisarawe alizidi kutoa maelekezo kwa vitendo zaidi na safari hii mikono yake ikiparaza juu ya mapaja ya Sulee.
"Aah! Sasa huyo mwanaume rijali nitampata wapi jamani mbona haya ni majaribu sana dokta…?"


"Kha! Mbona wapo wengi sana, huko mitaani au hata mimi…"
"Mimi wa mitaani naogopa, mume wangu ni mkorofi sana…"
"Basi mimi…," Dokta Kisarawe alipasua ukweli wake huku mikono yake ikiwa na kazi ya kumpapasa na kumbinya kimtindo Sulee, kuanzia maeneo ya kifuani, mapajani hadi mgongoni na kumalizia kwenye kiuno kipana na cha mviringo cha mwanamke huyo.


Kutokana na joto la mikono ya dokta, Sulee alikuwa akipeleka upinzani hafifu na kuruhusu mikono hiyo izidi kutalii kadri iwezavyo na kumuacha akilalamika kimahaba huku akitamka maneno ya kukolea penzi.
"Aaah, jamani dokta lakini mimi siumwi huukooo…," Sulee alilalama huku akitoa ushirikiano kwa dokta.
Baada ya kuona amekolea, Dokta Kisarawe hakuwa na ajizi zaidi ya kumuandaa na kumsogeza hadi kwenye kitanda kilichotumika kwa wagonjwa kulazwa wakiwemo wale wa kujifungua.


Dakika chache kila mtu akawa ameiva na kuhitaji kukabiliwa na mwenzake, vilio na miguno ya kimahaba vikatawala ndani ya chumba hicho cha Dokta Kisarawe.
Haikuchukua muda mrefu, Sulee akatangaza kufika mwisho wa safari na dokta akimkaribisha kwa bashasha zote.
Baada ya shughuli pevu, dokta alimtaka Sulee arudi siku ya kesho kwa ajili ya vipimo zaidi kwa wakati huo, muda ulikuwa umekwenda.


"Ahsante sana dokta jamani, wewe ni tofauti sana…," alisema Sulee baada ya kuagana na dokta na kisha kuondoka huku akiangalia nyuma.
***
Masofa ambaye ni mume wa Sulee alikuwa sebuleni akimsubiri mkewe ambaye alichelewa sana kurudi kutoka kwa dokta.
"Ina maana huyu hadi sasa ni tiba gani hiyo…," alijiuliza Masofa akiwa na hasira.


Wakati akiwaza hayo, alisikia hodi na kwenda kufungua akakuta ni mkewe.
"Jamani mke wangu Sulee, hadi saa hizi ulikuwa kwa dokta tu…?"
"Sasa kumbe nilikuwa wapi tena jamani mume wangu…?," alijibu Sulee huku akitupia mkoba wake kwenye kochi.
"Dokta alikuwa na watu wengi, ndiyo maana nimechelewa kwani sasa hivi saa ngapi?"


"Angalia saa mwenyewe…"
"Mm! yaani saa tano kasoro mara hii…!"
"Haya, niambie huyo dokta amesema nini…?"
"Kwa leo amenipa ushauri tu wa kisaikolojia, amesema nirudi tena kesho muda kama wa leo…," alijibu Sulee.
"Mm!, ina maana leo amekupa ushauri tu…?"


"Ee mume wangu…"
"Inabidi kesho twende wote…," alisema Masofa na kumuacha Sulee ametumbua macho.
 
DOKTA MIMI SIUMWI HUKO-4

ILIPOISHIA:
"Mm! ina maana leo amekupa usahauri tu…?"
"Ee mume wangu…"
"Inabidi kesho twende wote…," alisema Masofa na kumuacha Sulee ametumbua macho.
GALAGALA NAYO SASA…


"Sasa mbona umekaa kimya, umenielewa…?" aliuliza tena Masofa akiwa amemkazia macho Sulee aliyekuwa bado amemtumbulia macho ya mshangao.
"Mm…!," aliguna Sulee kabla ya kukubaliana na uamuzi wa mumewe, hapo moyoni alibaki na maswali mengi juu ya hali itakavyokuwa baada ya kufika kwa dokta siku inayofuata.
"Sawa," aliitikia huku akitingisha miguu mahali alipokuwa amekaa.


"Sawa, ndiyo nini…?"
"Kha!, si nimekubaliana na ulichosema…!," alisema Sulee huku akimwangalia mumewa kwa jicho la ‘usinichoshe bwana'.
Masofa alibaki kimya kidogo, akaanza kuondoka kuingia chumbani huku akigeuka na kumwangalia Sulee.
Muda mfupi badaye, Sulee aliungana na mumewe chumbani ambapo bila hata kuvua nguo alijitupa kitandani.


"Aah, nianche bwana…," alikuwa ni Sulee akimjibu mumewe aliyekuwa bize kwa kumshika sehemu mbalimbali za mwili hasa maeneo ya nyuma akiomba kutafuna tunda.
"Sasa nikuacheje jamani mke wangu…?"
"Mimi nimechoka bwana…"
"Umechoka na nini…"


"Kha! si kazi jamani, au watu huchoka na nini…?"
Masofa hakujibu kitu zaidi ya kusitisha alichokuwa anakiomba.
Walipitiwa na usingizi hadi asubuhi ambapo Masofa alikuwa wa kwanza kuamka kabla ya Sulee aliyekuwa bado akiufaidi usingizi wa asubuhi uliokuwa ukisindikizwa na kibaridi cha alfajiri.
Masofa alijiandaa na kuelekea kazini, hakutaka kumsumbua Sulee akihofia mzozo usiokuwa na maana kwani aliyakumbuka vyema majibu yake ya jana.
***


Sulee aliendelea kulala hadi saa tatu na nusu aliposhituka ghafla. Akakurupuka na kukimbilia bafuni ambako alioga kabla ya kuanza kuandaa kinywaji.
Akiwa anakunywa chai, ghafla mazungumzo na majibizano yake ya jana na mumewe Masofa yakaanza kujirudia kichwani mwake.
"Haya, niambie huyo dokta
amesema nini…?"


"Kwa leo amenipa ushauri
tu wa kisaikolojia, amesema
nirudi kesho muda
kama wa leo…," .
"Mm!, ina maana leo
amekupa usahauri tu…?"


"Ee mume wangu…"
"Inabidi kesho twende…"
Kufika hapo, Sulee akaishiwa nguvu kimtindo.
"Sasa huyu naye anataka twende wote kwa dokta ili iweje?, wengine wanasumbuliwa na wivu, sasa kama yeye kazi hawezi si awaachie wenzake…", aliwaza Sulee.


Akaendelea na majukumu mengine kama mama wa nyumbani, huku moyoni akiombea mumewe apatwe na dharura yoyote ili asiende naye kwa Dokta Kisarawe!
Mawazo yakampeleka hadi kwa Dokta Kisarawe ambaye tayari hisia za mapenzi zilishaanza kuchipuka baada ya kupatiwa raha ya ajabu jana yake.


"Nakupenda, nakutaka, nakuhitajiiii….moyo wangu wakuwazaaa… mpenzi uko mbali namii….," Sulee alijikjuta akiimba wimbo huo wa Lady Jay Dee uitywao Distance baada ya hisia juu ya Dokta Kisarawe kuzidi kumuwaka vibaya…!"
Hatimaye muda wa mumewe kutoka kazini uliwadia, ambapo maandaliazi ya kwenda kwa dokta yakaanza.
Ilipotimu saa moja na nusu, Masofa akiwa na mkewe walikuwa njiani kuelekea kwa Dokta Kisarawe.


Wakamkuta dokta akiwa peke yake kwenye chumba chake akiwa bize na ukaguzi wa mafaili mbalimbali ya wagonjwa.
Dokta Kisarawe alipomuona Sulee, mapigo ya moyo wake yakaongezeka, ikabaki kidogo tu aropoke jambo ambalo lingeharibu kila kitu.
"Jamani hon…," alijikuta akikomea njiani japokuwa lile neon hon alitaka kutamka haoney, lakini akajikuta akibadili haraka baada ya machale kumcheza haraka.


"Hata haujachelewa, aisee unazingatia sana muda…"
"Kawaida tu dokta…," alijibu Sulee huku akijifanya kuvaa sura ya ubize kidogo.
"Ehee, naona umekuja na mgeni…"
"Siyo mgeni, huyu ndiye mume wangu…"
"Ooh, karibu sana…."


"Ahsante…,"aliitikia Masofa huku akimuangalia Dokta Kisarawe kwa jicho la "si utoe tiba tuondoke."
"Dokta Kisarawe naye akamwangali kama anayesema "Mbona umekaa kitemi sana."
"Ok, sasa sikiliza anti, nadhani jana uliyaelewa maelekezo yangu…"
"Ndiyo dokta…"
"Kuna dawa nitakupa kwa leo, ambazo utazitumia kwa siku tatu mfululizo kabla ya kurudi tena…"


"Sawa, dokta…".


Dokta Kisarawe akainama na kutoa kopo f'lani lililokuwa na dawa za vidonge, pamoja na zingine za maji!
"Hizi dawa ni muhimu sana, katumie kwa mtindo niliokuelekeza jana…"
"Sawa."
Baada ya maelekezo hayo, waliagana kwa kupeana mikono huku Dokta Kisarawe akimpa moyo Masofa kuwa mkewe atapona na kuondokana kabisa na tatizo la kutozaa.


"Usijali, mkeo atapona tu…"
"Ahsante sana dokta…," alisema Masofa huku akipeana mkono.
Wakaachiana mikono lakini Dokta Kisarawe akawa anamtupia jicho Sulee aliyekuwa kimya muda wote.


***
Toka siku hiyo, Dokta Kisarawe akawa anashinda akila karanga pamoja na kunywa mchuzi wa pweza kwa wingi, yote hiyo akiwa amempania Sulee atakapokuja siku ya tatu, kwani aliamini kwa vyovyote vile ni lazima aende peke yake.
 
DOKTA SIUMWI HUKO-5


ILIPOISHIA
Toka siku hiyo, Dokta Kisarawe akawa anashinda akila karanga pamoja na kunywa mchuzi wa pweza kwa wingi, yote hiyo akiwa amempania Sulee atakapokuja siku ya tatu, kwani aliamini kwa vyovyote vile ni lazima aende peke yake.
OGELEA NAYO SASA…


Kila mara Dokta Kisarawe hakuacha kumkumbuka Sulee…!
"Dah, yule ni mwanamke bwana…," aliwaza Dokta Kisarawe jioni moja akiwa amejipumzisha.
"Halafu, si nilimwambia aje baada ya siku tatu…?," aliendelea kujiuliza maswali mengi.
"Eeh bwana…Ina maana kesho yupo hapa…Afadhali, kesho nitabimbilika naye tena…," akaendelea kujikumbusha mwenyewe ndani ya chumba hicho.


"Twende mbele, turudi nyuma, aisee yule ni demu…Na hata muumba aliposema nitakufanyia msaidizi, alimaanisha yule…Kweli tena, fuatilia sana…," Dokta Kisarawe akazidi kuzama kwenye mawazo hayo ya kujibizana na nafsi yake.
Dozi kali ya mchuzi wa pweza na karanga mbichi kwa wingi alizokuwa akizitumia Dokta Kisarawe, ziliendelea kumuweka sawa kwa ajili ya mechi kali ya kukata na shoka siku atakapokutana na Sulee.
"Mume wangu si unakumbuka dokta alisema nirudi baada ya siku mbili…?," Sulee alimuuliza mumewe baada ya siku hiyo kufika.


"Kha!, sasa mimi na wewe nani anapaswa akumbuke…?," Masofa alimjibu kwa mkato na sauti ya kishari.
"Wote…," Sulee naye akajibu kishari huku akimtupia jicho."Halafu wewe siku hizi mtata sana…"
"Nakumbuka basi, unasemaje…?"
"Basi ni leo…"
"Sasa ulikuwa unauliza au kunitaarifu…?," Masofa alijibu lakini safari hii akiwa ‘siriasi' zaidi.
Maisha ya Sulee na Masofa ndani ya ndoa yao, yalikuwa yameshaanza kuingia dosari.


Hii ni kutokana na hali ya Sulee kutopata ujauzito.
Sulee alinyamaza na kuendelea na shughuli zake. Masofa naye akaondoka kwenda kwenye mihangaiko yake ya kila siku.
Jioni ilipofika, Sulee alijiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na Dokta Kisarawe, moyoni akiwa amepania sana kupata tiba ya uhakika.
Akaianza safari ya kuelelekea kwenye zahanati ya daktari huyo. Alipofika alimkuta akiwa na mwanamke mwingine ndani, ikabidi asubiri nje.


Dakika moja baadaye, yule mwanamke aliondoka na kumpa nafasi Sulee kumuona Dokta Kisarawe…
"Niambie jamani…," alisema Sulee huku akipanua mikono yake ili kumruhusu Dokta Kisarawe amkumbatie.
"Safi tu, mbona una furaha sana…?"
"Aah!, si nimefurahi kukuona jamani, au hupendi…?," Alijibu Sulee wakiwa bado wanaendelea kukumbatiana.
"Sijasema hivyo, vipi kwema lakini…?"


"Kwema tu, naona ulikuwa na mwanamke humu, naye ana tatizo kama la kwangu…?"
"Hapana, kuna dawa nilikuwa namuelekeza, vipi mume mwenzangu mzima…?," Alijibu Dokta Kiasarawe lakini mikono yake ikianza kukosa utulivu mwilini mwa Sulee.
"Aah!, jamani sa…saaa…," Sulee alijaribu kuuliza lakini tayari joto la miili yao lilikuwa likimuendea ndivyo sivyo.
"Sasa kwani nini tena jamani…?," Dokta Kisarawe aliuliza huku mikono ikiendelea kuutalii kwa utundu wa hali ya juu sana mwili wa Sulee.


"Aaa….h, mmh…," Sulee alishindwa kuvumilia utundu wa mikono ya Dokta Kisarawe ambaye sasa alikuwa amemsogeza karibu kabisa na kifua chake kuliko hapo awali.
Mikono ikashuka hadi kwenye kiuno cha Sulee kilichobinuka vyema na kujitenga kwa juu.
Akawa kama anakibinya kimtindo, hali iliyomfanya Sulee apige ukelele wa kuashiria kuguswa yalipo maruhani yake.
Dokta Kisarawe hakuishia hapo, sasa akawa anaparaza kifuani na kuzigusa nido kimtindo…


Sulee akawa anajinyonga huku naye akirudisha mashambulizi kwa kummiliki Dokta Kisarawe.
Ikafika wakati kila wakishikana, wanakuwa wanalegezana nguo taratibu, baadaye kila mmoja alijikuta akiwa kama alivyokuja duniani.
Dokta Kisarawe akamuweka sawa Sulee kwa chini na kuanza kuchimba chumvi kisimani hali iliyozidisha uraha wa ajabu kwa Sulee.


"Yes, yesiii..yee..eee…siiiiii…..," Sulee alizidi kuitikia kila alichoulizwa na Dokta Kisarawe.
Wakati akichimba chumvi, mikono ya Dokta Kisarawe ikawa bize na kifua cha Sulee, alizishika nido na kuzizungusha, Sulee akawa hana cha kufanya, akatoa macho yake meupe na kuyazungusha huku na kule.
Sulee aliposhindwa na uzalendo, akamgeuza Dokta Kisarawe na kuikimbilia maiki yake, akaishika vyema na kuanza kuimba nyimbo mbalimbali tamu.


Dokta Kisarawe akawa anasikilizia utamu wa mashairi ya Sulee kwa kufuatisha alivyokuwa akiimba.
Muda wa sebene ukawadia, kila mmoja akamuweka sawa mwenzake. Mechi kali ikaanza.
 
DOKTA SIUMWI HUKO-6


ILIPOISHIA
Dokta Kisarewa akawa anasikilizia utamu wa mashairi ya Sulee kwa kufuatisha alivyokuwa akiimba.
Muda wa sebene ukawadia, kila mmoja akamuweka sawa mwenzake, mechi kali ikaanza.
SASA ENDELEA…


ILIKUWA ni furaha ya aina yake kwa Dokta Kisarawe japo kwa Sulee ilitegemea na biti kwani wakati mwingine aliisikia sauti ikimwambia…
"Lakini wewe ni mke wa mtu, unalijua hilo?"


Sulee alishindana na akili zake kuhusu hilo, lakini sasa mapigo ya Dokta Kisarawe yalimfanya asitishe kwa muda kuwaza mambo hayo na kumpa ushirikiano mzuri…
"Dokta," aliita Sulee lakini hakuitikiwa kwani dokta alijitahidi ili amalize haraka na kuwahudumia wagonjwa wengine.


Hivyo alijitahidi kupiga mipira ya karibu. Sulee alikuwa hoi, kwa sababu alisimama, miguu iligoma kufanya kazi, akataka kukaa kwenye kiti lakini nafasi hiyo haikupatikana kwa Dokta Kisarawe.
Ni Sulee huyohuyo ndiye aliyeanza kutangaza hali ya hatari golini kwake, dokta akambana vizuri zaidi ili kumkinga na anguko lolote…


"Dokta…dokta nipe mtoto basi," alisema Sulee akitaka kujitoa kwa dokta baada ya kupasua dafu lake lakini dokta ambaye alihamasishwa na lugha hiyo alimzuia na yeye akatangaza kushuka chini ya mnazi na kuvunja dafu lake, wote wakavunja madafu yao.


Mlio wa pangaboi ndani ya chumba hicho cha dokta ndiyo uliosikika pekee huku kila mmoja akiwa hana la kumwambia mwenzake. Sulee alikaa kwenye kiti na kuinamia meza, dokta alisimama, mkono mmoja ulishika sehemu ya juu ya suruali yake akiiziba njia.


"Wewe Sulee wewe, hivi kweli umekuja kutibiwa au kutibua?" Sulee alisikia sauti ikimwambia hivyo…
"Nimekuja kutibiwa," eti Sulee aliijibu ile sauti kwa kujiamini.
Sasa alikaa vizuri, dokta naye alikuwa kwenye eneo lake la kiti akimwangalia mwanamke huyo, aliyeumbika sawa na mapenzi ya muumba.


Wote walijikuta wakicheka, lakini Sulee akakatisha kicheko kwa swali…
"Hivi mfano dokta…"
"Ee…"
"Ikitokea nimepata mimba mtoto wa nani?"
"Si wa kwako!"


"Hutamtaka?"
"Ha! Nimtakie nini wakati mimi nina mke wangu na watoto watatu, nimtake mtoto wako sijitaki kwangu?"
"Kwa hiyo unaniahidi?"
"Nakuahidi Sulee wala usiwe na wasiwasi."


Siku hiyo Dokta Kisarawe hakumpa dawa yoyote Sulee, akamwambia akaishi kwa siku thelathini kamili halafu arudi tena…
"Noo dokta, mume wagu ataniuliza dawa ziko wapi?"


"Oke…oke, basi chukua hizi, akikuuliza muoneshe..." Dokta Kisarawe alimpa Sulee vidonge vya kutibu mifupa, maarufu kwa jina la ‘indosidi'.
"Hapo sawa."
Sulee aliondoka akiwa mwepesi sana, alitembea kwa madaha kurudi nyumbani kwake.


***
Usiku wakiwa kitandani, mume wake alimuuliza…
"Vipi hospitali?"
"Nilikwenda."
"Walikupa dawa?"
"Ndiyo."
"Dawa gani?"


"Mi sizijui, sijui zinaitwaje!"
"Ziko wapi?"
"Sulee alitoka kitandani kwenda kuzichukua, akampa mumewe…
"Hizi siyo za kuongeza damu?"
"Mi sijui, alisema niwe nameza vidonge viwili kwa siku mpaka mwezi mmoja uishe halafu niende tena."
"Sawa. Tutaona, kama hakuna matumaini itabidi tuachane naye," alisema mwanaume huyo akiwa amelala anaangalia juu.


***
Mwezi mmoja na siku mbili, siku hiyo Sulee alijiandaa vilivyo, si kama anakwenda kwa daktari kupata tiba ili anakwenda kwa mpenzi wake. Kama mumewe angekuwepo nyumbani angemzuia kuvaa alivyovaa…
"Hapa niko sawa, mwenyewe akiniona atajua mimi ni mwanamke wa nguvu. Lakini Dokta Kisarawe naye, mh! Sijui alikwenda chuoni!"


Sulee alikuta wagonjwa wengine, akapanga foleni akiwa ni mtu wa kumi na saba mpaka kuingia chumba cha daktari. Alipita nesi…
"Samahani anti, mwambie Dokta Kisarawe nipo hapa nje."
"Mh! Unadhani ataweza kuwaacha wenzako wote hawa akakuwahi wewe tu?" alihoji yule nesi.
"Sijasema awaache, nimekwambia mwambie nipo hapa nje."


"Umesema nani vile?"
"Sulee."
"Haya, subiri."
Nesi aliingia kwa dokta, aliweka cha kuweka kabla hajatoka akamwambia…
"Kuna dada anaitwa Sulee, anasema amefika."
"Kwa hiyo?"


"Kasema nikwambie."
"Oke, mwambie umeshaniambia, asubiri. Yeye anadhani ni wa maana kuliko wenzako siyo?"
Nesi alitoka akafunga mlango huku macho yake yakikutana na macho ya Sulee…
"Nimemwambia anti, lakini hajanijibu kitu."
Sulee kuna kitu kiligonga kichwani mwake…


"Au wanawake wote hawa ni wake, kwa hiyo kila mmoja ana umuhimu kwake? Maana kama mimi tu ndiyo mtu wake angetoa jibu lolote lile, isitoshe hatujaonana siku nyingi, mwezi na kitu sasa."
"Aingie mwingine," alisema Dokta Kisarawe akiwa amesimama mlangoni, alikutana macho na Sulee lakini hakuonesha uchangamfu wowote ule.
Dakika tano baada ya huyo mwanamke kuingia, vicheko na kugongeana mikono kulisikika kutoka kule ndani.
 
DOKTA SIUMWI HUKO-7


ILIPOISHIA
"Aingie mwingine," alisema Dokta Kisarawe akiwa amesimama mlangoni, alikutana macho kwa macho na Sulee lakini hakuonesha uchangamfu wowote ule.
Dakika tano baada ya huyo mwanamke kuingia, vicheko na kugongeana mikono vilisikika kutoka kule ndani.
TIRIRIKA NAYO SASA...


Sulee akaamua kunyanyuka mahali alipokuwa amekaa na kusogea karibu kabisa na mlango.
Akawa anategesha sikio kusikia zaidi kinachoendelea ndani ya chumba cha Dokta Kisarawe.
Vicheko viliendelea kusikika, kugongeana mikono kukazidi kuchukua nafasi kubwa....!


Sulee alirudi hadi alipokuwa ameketi awali, nakuanza kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
"Hivi, wanaweza kuwa wanafahamiana kweli...?"
"Kha, lakini nami bwana, sasa kama hawafahamiana wanawezaje kucheka na kugongesheana mikono namna hiyo...?"


"Kwa vyovyote vile watakuwa wanafahamiana tu, ngoja nifuatilie sana...!
"Sasa kama wanafahamiana, kuna uwezekano huyu dokta kuwa anatuchanganya...?"
"Yawezekana..."


"Lakini ni sisi wanawake yawezekana ndiyo tunajichanganya...," Sulee aliendelea kujisemea juu ya hali aliyoiona kwa siku hiyo.
"Ina maana kila mwanamke mwenye ugonjwa kama wangu, ni lazima atembee na huyu dokta ndiyo apone...?"


"Sasa kama ni hivyo atakuwa ametembea na wangapi?"
"Kama ndiyo mtindo wake, kwa nini sisi wanawake tusishituke ?"
"Kuna uwezekano wanawake wengi wanajua, lakini nani wa kuvujisha siri kama anapokea dozi ya maana ya Dokta Kisarawe...? Halafu sasa unakuta wengi wao ni wake za watu, lakini sisi wanawake bwana...!


"Sisi wanawake siyo, wewe tufuatilie sana, siyo kwa sababu haiwezekani wote hawa tutembee na mtu mmoja na siri isijulikane...," maswali yakazidi kumchanganya Sulee mahali alipokuwa amekaa.
Lakini kwa wakati wote huo akiwa amekaa kwenye ile foleni, macho yake hayakuwa yanabanduka kwenye mlango wa ofisi ya Dokta Kisarawe...


"Lakini mimi naye bwana, sasa nimethibitishaje kuwa ni wapenzi labda huenda wanafahamiana tu na umepita muda mrefu bila kuonana?"
"Lakini, kufahamiana gani huko wanacheka hadi kugonganisha mikono kwa sana...?"
"Sasa kwani kugongeana mikono kuna maanisha nini...?," Sulee akazidi kujihoji na kujijibu mwenyewe, hali ilishaanza kuwa tete ndani yake. Moyo haukuwa na amani tena na kidonda cha wivu kilishaanza kumnyemelea.


"Yaani kweli mambo anayonifanyia Dokta Kisarawe, anaweza kumfanyia mwanamke mwingine kweli?"
"Eee, inawezekana kwani kama aliweza kwako ni kivipi asiwafanyie wengine...," ilisikika sauti ikimjibu kutoka upande wa pili wa moyo wake.
"Ila kweli, hilo nalo neno."


Sulee aliendelea kujihoji na kujijibu mwenyewe. Hali haikuwa hali. Dokta Kisarawe alikuwa amemuingia moyoni mwake, sasa alikuwa haambiliki wala kusikia chochote juu yake.
"Haya mapenzi bwanaaa, hayana maana....," wimbo wa Diamond ulisikika masikioni mwake baada ya kushindwa kuhimili vishindo vya maumivu ya wivu wa mapenzi.


Muda mfupi baadaye, Sulee aliamua kusogea tena karibu kabisa na mlango wa ofisi ya Dokta Kisarawe. Lengo la safari hii ni kusikia nini kilikuwa kikiendelea ofisini humo.
Sulee alishituka baada ya kusikia sauti za kunong'ona kwa chini sana tofauti na awali ambapo Dokta Kisarawe na mteja wake walikuwa wakizungumza kwa sauti ya juu.
Safari hii alisikia watu wakibusiana, moyo ukazidi kumuuma...


Akajishika kifuani kwa upande wa kushoto ulipo moyo, mapigo yakazidi kumuenda mbio.
Dakika mbili baadaye, alianza kusikia miguno na sauti ya meza na kiti vikisogea...Moyo ukazidi kumuuma kuliko kawaida.
"Kuchiii.....kwaguuu...vegeeee....vegeeee.....vigi...vigiiiii....," milio ya kiti na meza viliendelea kusikika na kuzidi kumpa maswali mengi sana Sulee...


Mbali na milio ya samani hizo, miguno na mihemo ya chini ikazidi kusikika, kila dalili ya watu kula mua ikawa inajionesha wazi...
Sulee akashindwa kuvumilia, akarudi kwenye kiti. Dakika tano baadaye yule mwanamke akatoka. Dokta Kisarawe naye akatoka nje na kumuita mwanamke mwingine. Lakini wakati akimuita mtu mwingine, macho yake na ya Sulee yalikutana lakini hakuonesha dalili yoyote ya kumchangamkia (Sulee). Hali hiyo ikazidi kumchanganya kabisa Sulee.


Kuna kipindi akataka kuondoka lakini akazidi kujipa moyo na kuendelea kusubiri aone hatma ya mchezo wa siku hiyo.
"Kha, au kuna kitu nimemkosea ndiyo maana kachukia namna hii, au niondoke? Lakini nikiondoka wakati nimeshafika hapa itakuwa si busara. Ngoja niangalie mwisho wa hii sinema...," akawaza moyoni Sulee.


Hatimaye wote wakaisha na kubaki kwenye benchi peke yake. Akadhani sasa zamu yake imewadia. Lakini alishangaa kumuona Dokta Kisarawe akitoka huku akifunga mlango wa ofisi yake kwa ufunguo.
Kuona hivyo, Sulee akahamaki na kumuuliza kulikoni iwe hivyo na vipi kuhusu tiba yake kwa siku hiyo?
"Haa, sasa Dokta mbona unaondoka vipi kuhusu mimi jamani...?
"Kuhusu wewe nini tena..."


"Si tiba yangu..."
"Ipi..."
"Ya siku zote, ina maana umesahau kabisa...?"
"Hebu acha maneno yako wewe...," alijibu Dokta Kisarawe huku akimalizia kufunga kufuli la mlango.
 
DOKTA SIUMWI HUKO-8


ILIPOISHIA:
"Hebu acha maneno yako wewe…," alijibu Dokta Kisarawe huku akimalizia kufunga kufuli la mlango.
YUMBAYUMBA NAYO SASA…
"Kha, dokta mbona sikuelewi…?"
"Hunielewi kivipi wewe….?"
"Si hivyo, ina maana kweli hujui kilichonileta…?"


"Sasa kama ningekuwa sijui si ningekuuliza…?"
Sulee alibaki kimya. Akawa hana cha kujibu wala kuongezea kwa hapo. Majibu ya mkato ya Dokta Kisarawe yalikuwa yamemuumiza na kumvunja moyo vibaya mno.
"Unajua Sulee mimi nakushangaa sana…," Dokta Kisarawe alifungua tena uwanja wa mazungumzo baada ya Sulee kubaki kimya.


"Wewe unanishangaa mimi, au mimi ndiyo nakushangaa wewe…?"
"Kwani, hebu ngoja nikuulize, hivi inawezekana kweli nikawa nawaita wagonjwa wengine, hadi nafunga mlango halafu nisijue kilichokuleta, inawezekana kweli?"
Sulee alibaki kimya tena, akawa anamwangalia Dokta Kisarawe kwa macho ya ‘unataka kusema nini sasa?'


"Sikiliza, nina mazungumzo na wewe nje ya mazingira haya ya kazi, ndiyo maana sikutaka kukuita toka mwanzo," alisema Dokta Kisarawe na kumfanya Sulee aachie tabasamu kwa mbali.
"Hapo sawa, kwa hiyo tunaelekea wapi…?"
"Wewe tulia, si uko na mimi sasa wasiwasi wako nini…?"
"Mmh…!", Sulee aliishia kuguna.


Dokta Kisarawe akanyanyua simu na kupiga upande wa pili, ambapo ndani ya dakika kumi na tano, ilikuja teksi na kusimama karibu kabisa na walipokuwa.
Sulee akaelewa kuwa kumbe ile simu ilikuwa ni wito wa teksi. Kwa tahadhari kubwa sana, Dokta Kisarawe akampa ishara Sulee ya kumtaka akae siti ya nyuma.


Yeye akakaa mbele na dereva. Safari ikaanza huku Sulee asijue walipokuwa wakielekea.
Akataka kuuliza lakini dhamira ikamsuta na kubaki na maswali yasiyokuwa na majibu.
"Sijui tunaelekea wapi jamani…?"
"Lakini namie bwana, si nimeambiwa nitulie kwa kuwa niko naye…!"


"Lakini hata kama, sasa ndiyo napelekwa pelekwa tu kama mbuzi…!," alizidi kuwaza lakini wakati akiendelea na mawazo hayo, ghafla mazungumzo yake na Dokta Kisarawe yakajirudia kichwani kwa kasi ya ajabu.
"Haa, sasa Dokta mbona unaondoka vipi kuhusu mimi jamani…?"
"Kuhusu wewe nini tena…"
"Si tiba yangu…"


"Ipi…?"
"Ya siku zote, ina maana umesahau kabisa…?"
"Hebu acha maneno yako wewe…,"
"Kha, dokta mbona sikuelewi…?"
"Hunielewi kivipi wewe….?"
"Si hivyo, ina maana kweli juhui kilichonileta…?"


"Sasa kama ningekuwa sijui si ningekuuliza…?"
"Sikiliza, nina mazungumzo na wewe nje ya mazingira haya ya kazi, ndiyo maaana sikutaka kukuita toka mwanzo.
"Hapo sawa, kwa hiyo tunaelekea wapi…?"
"Wewe tulia, si uko na mimi sasa wasiwasi wako nini…?
Ikabidi atulie.


"ngoja nione mwisho wa safari hii…," akawaza moyoni huku akiegemea kwa nyuma.
Safari ikaendelea, mbele kidogo dereva alianza kupunguza mwendo, Sulee alipochungulia kupitia kioo, akasoma bango lililoandikwa Utulivu Gest House.
Moyo ukamlipuka, akajua nikilichokuwa kinaendelea.


Baada ya kuteremka, dokta alimlipa dereva pesa yake na kumruhusu aondoke zake lakini akamwambia angempigia simu baaadaye kwa ajili ya kwenda kuwapokea. Alionekana kuwa ni mtu wake wa karibu sana, ndiyo maana Dokta Kisarawe alikuwa anamuamini kwa kiasi kikubwa namna hiyo.
Wakazama hadi mapokezi ambapo baada ya kukamilisha taratibu zote, wakapewa chumba.
Walipoingia tu, Dokta akaanzisha mazungumzo.


"Umeona mwisho wa safari yetu…?"
"Nimeona, umeshinda bwana…"
"Ulikuw ana wasiwasiii….?"
"Mmh…"


Dokta Kisarawe alimwambia Sulee kuwa alikuwa mjamzito jambo lililomshangaza sana Sulee.
"Unasema kweli dokta…?"
"Wewe niamini mimi…"
"Kweli…?"


"Ili uhakikishe, naomba kesho ukapime kwa daktari mwingine halafu uje uniambie."
Waliongea mengi lakini mwisho wa siku wakaelekea kwenye uwanja wa fundi seremala ambapo shughuli ilikuwa pevu, Sulee alijiachia na kutamka maneno yote aliyoyajua. Hatimaye walifika pamoja mwisho wa safari yao.


Baada ya shughuli hiyo, Sulee aliingia bafuni kujiweka sawa, na kisha kutoka ambapo alichukua usafiri hadi nyumbani kwake.
"Mbona leo umechelewa sana kurudi…?," Mumewe Sulee, Masofa alimuuliza akiwa amekunja ndita.
Ilikuwa ni kama saa mbili na dakika kumi usiku kwa wakati huo.
"Watu walikuwa wengi sana, halafu nina habari njema sana mume wangu…"


"Habari gani hiyo…?"
"Nina mimba…"
"Amekupima…?"
"Sasa asingenipima ningejuaje…?"
"Ok, mimi siamini labda twende kwa daktari mwingine…"


"Sawa…"
Waliongoz
ana hadi kwenye zahanati ya jirani, na kumkuta daktari akiwa peke yake.
"Karibuni jamani"
"Ahsante…"
Walieleza shida zao, taratibu zikafanyika na baada ya dakika ishirini, waliitwa na daktari huyo.
 
DOKTA SIUMWI HUKO-9


ILIPOISHIA:
"Karibuni jamani."
"Ahsante…"
Walieleza shida zao, taratibu zikafanyika na baada ya dakika ishirini, waliitwa na daktari huyo.
ZUNGUSHANA NAYO SASA…


Jamani sasa naomba muwe tayari kwa ajili ya kupata majibu yenu…," yule daktari akafungua uwanja wa mazungumzo.
"Sawa daktari, tuko tayari…," mumewe Sulee Mr. Masofa alijibu kwa sauti ya unyenyekevu na wasiwasi mkubwa.
"Hongereni sana…"


Aliposema maneno hayo, akatulia na kuwaangalia kwa zamu.
"Mkeo ana ujauzito wa mwezi mmoja, hongereni sana…," yule daktari alirudia tena na kuwapa mikono ya furaha kwa pamoja.
"Jamani mke wangu, kumbe ni kweli, hongera sana…," Masofa alisema huku akimkumbatia kwa furaha kubwa mkewe.


"Ahsante sana mume wangu, hata mimi sikuamini nilipojua…"
Waliendelea kufurahia kwa muda mrefu kabla ya kuagana na daktari.
Walipofika nyumbani, furaha iliendelea, kila mmoja wao akijitahidi kuonesha upendo wa hali ya juu kwa mwenziye.
"Mume wangu Mungu ni mkubwa sana…"


"Kweli kabisa mke wangu…"
"Kwa jinsi tulivyohangaika kutafuta mtoto, hakika Mungu yupo mume wangu…"
"Uko sahihi kabisa mke wangu, tumshukuru kwa pamoja."
Furaha iliendelea kati ya Sulee na mumewe Masofa. Usiku mzima waliendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale ili mradi tu kukamilisha furaha hiyo.


Siku iliyofuata, mumewe Sulee alidamka mapema na kuwahi kibaruani akiwa mwenye furaha tele.
Sulee aliendelea kuchapa usingizi huku akimfikiria sana Dokta Kisarawe. Mapenzi yake juu ya dokata huyo yaliendelea kushamiri hasa kwa kitendo cha yeye kunasa ujauzito.


"Ina maana hapa mwenye matatizo ya uzazi ni huyu mume wangu Masofa…," Sulee alianza kujisemea muda mfupi baada ya kuamka na kuketi kitandani.
"Kweli kabisa, ni lazima atakuwa ni huyuhuyu, kwa sababu kama ningekuwa ni mimi nisingeweza kunasa hii mimba," mawazo hayo yakaendelea kujirudia kila mara akilini mwake.


Aliamka na kuanza kufanya usafi wa ndani baadaye akaenda kuoga. Alipomaliza akabandika chai jikoni huku akiendelea na ufuaji wa nguo chache zilizokuwa chafu.
Akamaliza kazi zote na kuanza kunywa chai huku akiwa ndani ya khanga moja iliyolichora thabiti umbo lake la namba nane.


Baada ya kunywa chai, aliingia ndani na kubadili nguo ambapo alivaa viwalo vikali vilivyomtoa sana.
Akaamua kwenda kwa rafiki yake mmoja aitwaye Monica aliyekuwa na tatizo la kutozaa kama alilokuwa nalo yeye.


"Hodi jamani hapa, hodi jamani…," Sulee alibisha hodi kwa mbwembwe na uchangamfu wa hali ya juu.
"Mm! Karibu sana jamani…," aliitikia Monicha huku akimshangaa Sulee kwa jinsi alivyokuwa amechangamka.
"Mzima shoga yangu…?"
"Mzima sijui wewe…?"


"Salama…"
"Karibu, naona una furaha kubwa kulikoni…?"
"Tayari shoga yangu, tayariii…"
"Tayari nini tena, mbona sikuelewi…!"
"Nimenasa…"


"Umenasa…?"
"Eee, nimenasa…"
"Umenasa nini Sulee, mbona sikuelewi?"
"Mwenzio nina mimba Monica…"
"Hamna, acha utani wako bwana…"


"Siyo utani Monica, nina mimba…"
Waliendelea kuzungumza mengi huku Monica akishangaa ni kwa namna gani ameweza kupata ujauzito wakati wote kwa pamoja walisumbuliwa na tatizo moja la kutopata ujauzito. Kwa upande wa Monica tayari alikuwa amekata tamaa.
"Umepata wapi hiyo tiba mwenzangu…?"


"Kuna daktari mmoja mtaalamu sana, yaani ameponesha wengi."
Sulee aliendelea kummwagia sifa Dokta Kisarawe.
Kwa muonekano, Monica alikuwa mwanamke mrembo mno kupita Sulee. Alikuwa mweupe, mrefu mnene kiasi huku nyuma akiwa ‘amejazia mzigo wa maana.'


Mwili wake ulinakishiwa kwa vinyweleo nadhifu vilivyolala, pua nyembamba ndefu wastani huku maeneo ya kifuani yakiwa yamepambwa kwa ‘nido' ndogo kiasi zilizochongoka.
Mara nyingi alipendelea sana kuvaa nguo za kubana na kusababisha mateso makubwa kwa wanaume wakware.


Miguu yake minene wastani, kila alipokuwa akikanyaga hatua moja, mzigo wa nyuma ulitingishika kiaina.
"Sasa na mimi utanipeleka lini nikamuone huyo daktari…?"
"Wewe unapenda twende lini…," Sulee alimuuliza Monica huku akiwa amemkazia macho.
"Hata sasa hivi, au unasemaje…?"


"Kwa leo itakuwa ngumu, maana inahitaji maandalizi…"
"Maandalizi gani Sulee jamani mimi nina shida, kama ni fedha ipo bwana…," Monica alizungumza huku akizidi kuliangalia kwa umakini sana tumbo la Sulee.


"Kesho uje unipitie nyumbani jioni ya saa moja na nusu, sawa…?"
"Saa moja na nusu…?," Monica alihoji kwa mshangao mkubwa.
 


***
Toka siku hiyo, Dokta Kisarawe akawa anashinda akila karanga pamoja na kunywa mchuzi wa pweza kwa wingi, yote hiyo akiwa amempania Sulee atakapokuja siku ya tatu, kwani aliamini kwa vyovyote vile ni lazima aende peke yake.


Hahaha hizi story za vijiweni vinapotosha na kuchekesha.
 
Back
Top Bottom