"Square Peg In A Round Hole"-ELIMU NI NINI?

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,967
22,476
Nitakwenda na kuileta ile hotuba ya Mbeki pale mlimani alipoweka wazi kuwa matatizo ya Afrika yanasababishwa na wale wenye ELIMU!

Kauli ya MBEKI ni NZITO na ya kutafakari kwani alipoitowa pale mlimani kwa masaa mawili mfululizo bila kupumzika alionyesha kukerwa sana na mikataba ambayo tumeingia na MAKABURU wa nchini mwake ambao hata sisi tuliwasaidia kumpinga na kumwondoa madarakani.

NI WAZI KUWA MADAI YAKE NI YA WAZI KUWA UMASIKINI WETU NA UFUKARA,MAGONJWA NA NJAA VIMESABABISHWA NA WENYE ELIMU.

Sasa naomba tuanze na mjadala huu...JE ELIMU NI NINI?
 
Hotuba hiyo hapo chini ni ya MBEKI kwa wasomi kabla hata sisi hatujajuwa vizuri kuhusu kashfa za UFISADI!
Ni wazi yeye alikuwa na data zaidi yetu na ndio maana alikuwa na MACHUNGU MWANA HUYU WA AFRIKA ALIYEMSHINDA JK NA MAMLUKI WENGINEO WA MZUNGU NA MWARABU!
Swali linabaki pale pale...ELIMU NI NINI?
Naomba mchangiaji usioigope kutowa jibu...Towa jibu based on your understanding..Ni swali linaloweza kuwapa hata maprofessa shida...Ila hapa jf hatuogopi kutowa mawazo yetu kwa UHURU...
Kutokana na ukweli kuwa mafisadi almost all of them are EDUCATED...THE....What is EDUCATION?

Mbeki: Afrika imeangushwa na wasomi

na Ratifa Baranyikwa

RAIS wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, amesema wasomi barani Afrika, hawatakiwi kulalamikia matatizo yaliyopo, kwani wao ndio chachu ya suluhisho ya matatizo hayo.

Akizungumza katika mdahalo uliofanyika juzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mbeki aliwapa changamoto wasomi nchini, nao kuacha kulalamika na badala yake watoe mchango wao katika kushughulikia matatizo.

Alisema wasomi nchini ndio wana jibu sahihi kuhusu matatizo yanayotokana na umaskini. Alisema thamani ya vyuo ni kutoa fikra zitakazowezesha kuchangia shughuli za maendeleo na kuwataka wasomi hao kufanya tafiti kuhusu hali za nchi zao katika kushughulikia matatizo ambayo yanazikabili.

Mbeki alisema Tanzania na Afrika Kusini wanaweza kukaa pamoja na kutafuta suluhisho kuhusu tatizo la umaskini na matatizo mengine ambayo yanakwamisha maendeleo ya kiuchumi iwapo wasomi watafanya ipasavyo yale wanayopaswa kuyafanya.

“Nchi zetu zina maliasili nyingi za kutosha kama maji, madini na kadhalika, sasa tunazitumiaje maliasili zetu katika kuzungumzia umaskini, ndilo jambo ambalo wasomi wanatakiwa kutoa mchango wao. “Tumekuja kwa wasomi kusema nini tufanye kuhusu maliasili zilizopo Tanzania, hii ni changamoto, nyinyi kama wasomi kushirikiana na serikali zenu,” alisema Mbeki.

Alisema kama nchi za Afrika ziliweza kuwaondoa wakoloni, sasa ni wakati wa kuondoa umaskini kwa kutumia maliasili zilizopo, lakini pia kwa mchango wa watu wenye ujuzi ambao ni wasomi.

Mbeki alisema hivi sasa nchi hizo mbili zimeanzisha ushirikiano ambao una lengo la kuleta maendeleo na kusema kuwa, katika mkutano wake na Rais Kikwete (uliofanyika juzi kabla ya kuhutubia wanafunzi wa chuo hicho), nchi hizo zilikubaliana kuanzisha Tume ya Maendeleo ili kupambana na umaskini.

Mbeki ambaye aliingia katika ukumbi wa chuo hicho wa Nkuruma majira ya saa 9 alasiri, alihutubia kwa muda wa saa mbili bila kupumzika mbele ya umati wa wanafunzi waliojaa kupita kiasi na kuwalazimisha baadhi yao kusikiliza mdahalo huo wakiwa nje ya ukumbi.

Alisema: “Hatuhitaji watu wengine kutoka nje kuwa waangalizi katika mambo yetu ya kimaendeleo, Waafrika wenyewe tunapaswa kuwa waangalizi wa masuala yanayohusu nchi zetu.”

Aidha, Rais Mbeki alisema kati ya matatizo ya kiuchumi ambayo viongozi wa Kiafrika wanatakiwa kuyavalia njuga, ni biashara. Akita mfano, alisema kiasi cha dola za Kimarekani milioni 500 zilipaswa kukusanywa kutokana na mauzo ya Tanzania nje ya nchi, lakini takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa kiasi kilichokusanywa ni dola milioni nane tu.

Alisema hii inatokana na uchimbaji na usafirishaji wa madini hayo, ambao si halali na kutokuwa na uhalali wa kuuza madini hayo nje. Alisema kwa mantiki hiyo, mchango wa wasomi hasa wa kifikra, ni muhimu sana kwa serikali zao kwa kushauri nini kifanyike kutokana na nchi zao kuwa na maliasili nyingi ambazo hazitumiki ipasavyo.

Mbeki alikuwa ameambatana na balozi wa Afrika Kusini nchini, pamoja na mawaziri kadhaa wa Afrika Kusini akiwemo Waziri wa Viwanda, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mambo ya Nje na mshauri wake wa mambo ya sheria.

Wenyeji wake aliokuwa ameongozana nao ni Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msola pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Basil Mramba.

Akimkaribisha Rais Mbeki awali, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alimshukuru Rais Mbeki kwa kutenga muda wake na kukutana na wanafunzi hao na kutambua mchango wa wasomi.

Wakizungumza na gazeti hili baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wanafunzi walisema kuwa, alichokisema rais huyo ni changamoto kwa serikali, pia kuhakikisha kuwa inaboresha elimu nchini.


Tanzania Daima: 7 Aprili 2007
__________________
 
Na kwa kuanzia mimi mwenyewe binafsi..Kabla sijaelezea maana halisi ya square peg in a round hole...Mimi naona nitowe kile ambacho nimejifunza kwamba elimu ni nini... na pia naomba nikosolewe kwani mjadala huu ni MUHIMU SANA....

BINAFSI NASEMA ELIMU NI MWENDELEZO WA KIJAPI.
 
Hapa nimeona kimya...Ina maana hakuna mwenye definition yake ya kuwa elimu ni nini?
Je kati ya kipaji na elimu...Kipi hutangulia?
Na kipi hutoa mwongozo pale inapokuja kwenye uamuzi wa direction ya future yako?
Kama kuna mwenye maoni...
 
Mwalimu alitufundisha kuwa..ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA...Je kama tukiamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha yetu sisi kama watu binafsi..Ni kivipi tutaweza kuamini kuwa elimu hiyo hiyo ni ufunguo wa maisha ya kila mtu bila kujali utofauti wao wa kabila,dini na hata rangi?
Je...Elimu ni nini?
 
Inawezekana hoja yangu kuwa elimu ni mwendelezo wa kijapaji imekubalika na wengi.

Na kwasababu hiyo basi...Naomba niwaase wazazi na vijana jambo moja...Kuwa kabla huja amuwa kuwa ni mchepuo gani wa elimu wa kuchukuwa...Jaribu kufanya utafiti kuhusu kipaji chako...Kwani wakati huu vipaji ndio hulipa watu...Mfano ni michezo,biashara,udokta,siasa nk.

Kama jamii yetu ikijipanga upya kwa kuzingatia hayo...Basi tutaepuka ile dhana ya square peg in a round hole...Kwa maana square haiwezi kufiti kwenye tundu la mduara...Ni vitu viwili tofauti...Utakuta watu wana vipaji vya tofauti lakini wanakwenda kusomea mambo ya tofauti kwasababu tu anachosomea ndio kina lipa kwa kupata kazi kiurahisi.

Na hapo ukiangalia kwa makini wenye uwezo wa kusoma ni wachache...Wengi wao wazazi wao ni matajiri ama viongozi wa nchi.

Vipaji Tanzani na Afrika vimezikwa moja kwa moja kwa sababu hiyo hapo juu.

Kwasababu tukijiuliza swali la msingi tutakuja kugunduwa kuwa kipaji cha wafanya biashara kilianza kabla hata ya slylabus ya bishara.

Mfano halisi ni Batter trade...Utakuta kuwa watu walikuwa wakifanya mambo base on specialization.

Hatuwezi kui apply dhana ya specialization kwenye karne hii ya 21...Lakini tunaweza kujifunza yale positive ya kimsingi...Kwamba kipaji mtu huzaliwa nacho...Na mtu anaweza kutumia elimu kukiendeleza kipaji chake badala ya kwenda na kusomea yale asiyokuwa na kipaji nacho....

To be continued...
 
Elimu ni ile uliyoipata inayokuwezesha kuwa raia bora wa dunia.
kujali maumbile uliyoyakuta na utakayoyaacha.
kujua nafasi na wajibu wako ktk ulimwengu.
inayokuwezesha kuyapa umuhimu hahitaji yako na ya walimwengu wengine.
inajifunzwa tangu unapozaliwa mpaka unapokufa.
Mbeki alimaanisha tumewapa nchi watu wasio na elimu, bali wenye nafasi na pesa za kudanganya watanzania,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom