Ndege ya idara ya wanyama pori yapotea

Power to the People

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
1,198
892
Ndege ndogo ya idara ya wanyama pori inasemekana imepotea na haijaonekana tangu ilipoondoka uwanja mdogo wa ndege wa Arusha kuelekea Loliondo.

Inasemekana ndege hiyo ilikuwa imebeba vigogo wa idara hiyo wakielekea Loliondo na leo longido kukutana na mafisa wa maeneo hayo.

Mwenye habari kamili atuambie
 
brothers and sisters

NIMEPATA HABARI KWAMBA KUNA NDEGE NDOGO ILIPOTEA JANA NA LEO IMEOKOTWA IMEANGUKA PORINI (MONDULI KAMA SIKOSEI) NA WATU WOTE WATATU WALIOKUA HUMO WAMEFARIKI

NADHANI HABARI ZAIDI MUWASILIANE NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
 
Ndege hiyo mali ya Wizara ya Maliasili na Utalii, imeangukia mlimani wilayani Monduli ikiwa njiani Kwenda Loliondo, ndio wahusika wamepaki magari hivi sasa wanapanda mlimani kuangalia ilipo. Ndege ilikua na biria watatu na rubani wake Pius Ngwalali. Miongoni mwa waliokuwamo ni Naibu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Miriam Zachariah na Ofisa wanyamapori Stephen Mahinya.

Ndege iliondoka Dar Julai 3 saa 2.30 asubuhi na kutua Arusha airport saa 4.00asubuhi na kuruka hapo Arusha uwanja mdogo saa 5.00 asubuhi kuelekea Loliondo, na baada ya hapo haijaonekana tena.
 
Last edited:
Mode badili si tetesi tena ni habari za uhakika. Ila vifo tutajua muda si mrefu baada ya polisi, maofisa wanyamapori na maofisa wa Usalama wa Anga wakifika ilipo ndege hiyo. Uwezekano wa kupona kwao ni mdogo sana kwa sasa.
 
Lo!hizi ndege ndogo na helcopta zetiu mbona zinapata masahibu hivi?
Mungu nusuru maisha ya watanzania.
 
Lo!hizi ndege ndogo na helcopta zetiu mbona zinapata masahibu hivi?
Mungu nusuru maisha ya watanzania.

SingleD kuna jambo. Tena Arusha!??? Lakini inawezekana kuna tatizo la hali ya hewa maeneo hayo, lakini kwa suala la helikopta ni dhahiri Vithlani na mwenzake Tanil Somaiya wa Shivacom wanatakiwa wakamatwe na watueleze
 
Lo!hizi ndege ndogo na helcopta zetiu mbona zinapata masahibu hivi?
Mungu nusuru maisha ya watanzania.

Mungu aweze roho zao mahali pema peponi, AMEN!

Binafsi nimeguswa sana na hii habari maana hao vigogo baadhi yao nawafahamu binafsi,,,,its so sad!
 
NakuliliaTanzania, bado hawajathibitishwa kufa, japo kupona ni bahati

Mkuu kuthibitishwa nadhani ni suala la protokali tu, lakini vyanzo vyangu vya KUAMINIKA vimeshaniambia hatunao tena

Kumbuka nimesema ni watu wangu wa karibu (walikuwa) kikazi japokuwa sio kipindi cha karibuni. I feel so sad mkuu lakini ndo ivo tena kazi ya Mungu!
 
Ndege hiyo mali ya Wizara ya Maliasili na Utalii, imeangukia mlimani wilayani Monduli ikiwa njiani Kwenda Loliondo, ndio wahusika wamepaki magari hivi sasa wanapanda mlimani kuangalia ilipo. Ndege ilikua na biria watatu na rubani wake Pius Ngwalali. Miongoni mwa waliokuwamo ni Naibu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Miriam Zachariah na Ofisa wanyamapori Stephen Mahinya.
Ndege iliondoka Dar Julai 3 saa 2.30 asubuhi na kutua Arusha airport saa 4.00asubuhi na kuruka hapo Arusha uwanja mdogo saa 5.00 asubuhi kuelekea Loliondo, na baada ya hapo haijaonekana tena.

Duh mbona hatari jamani,hili jina kama la jamaa wa Songea alikuwa SUA miaka ya 90 akibukua hiyo shahada ya wanyama.
Huko kwenye wanyama Arusha kuna nini?
 
Mtangazaji wa Taarifa ya Habari ya Tanzania Broadcsting Corp. ya saa 2 usiku EAT, July 4, 2008, amesema mara tatu, "Watumishi watatu wa Wizara ya Maliasili wamekufa papo hapo baada ya ndege kuanguka..."

Sasa, hii ndege ilipotea kwanza, na hakuna aliyeshuhudia wanakufa papo hapo.

Hako katofauti kana umuhimu gani?

Inawezekana Marehemu walighalaghala porini dakika, hata masaa kadhaa, bila msaada ambao ungeweza kuwaokoa. Hujui walikufa hapo hapo.

Katika nchi zilizoendelea, kushindwa kusaidia walioofikwa na maafa kama wangeweza kuokolewa ni skandali kubwa. Tanzania hatujafika kuwa na uwezo wa kufikia kwa haraka kwenye kila pori kuokoa watu.

Lakini usisema kwamba walikufa papo hapo. Hujui.

Sasa hii taarifa ndio Watanzania millioni 40 wamesomewa jioni ya leo!

Cheesy press!
 
Back
Top Bottom