Huoni kama kule Dodoma walimwaga ugali na yeye anamwaga mboga? Pengine (pengine kwa sababu sina hakika), kimya cha miaka minane yote hiyo kilikuwa ni katika juhudi za kuwakingia kifua wale "waliomkata". Baada ya kuona kuwa hawabebeki, hawafadhiliki, ndio hivi karibuni akaanza kutapika. Na kama...
Nape akisema 10 usishike hata moja. Huyu siye aliyekuja na kauli mbiu ya "Kujivua Gamba"? Nani alijivua? Badala yake watu "Wakavaa Ngao" na "kuwaesrow" Watanzania.
Langu Jicho.
Mzee Kingunge anajamini kwa sababu ni Mtanganyika (ukipenda ita Mtanzania) na kama angekuwa Mzanzibari, tayari angekwishaundiwa zengwe. Amuulize Mzee Moya.
Wengi wao ni wasindikizaji tu. Hawa hatimaye watajitoa na kuja kujiunga na makundi ya wagombea wenye mwelekeo ili mwisho wa shughuli yote, mshindi awaone kwa jicho la huruma.
DK Salim hapiti NG'O. Kwanza yeye mwenyewe alishajiweka pembeni na kukataa kutogombea akiamini kwamba hatapitishwa na wale waliomtimua Mzee Jumbe, wakamweka ndani Maalim Seif, wakaja kuwafukuza akina Othman Massoud, Mansour na hivi karibuni Mzee Moyo. Chezea CCM Zanzibar wewe!
Kwa maelezo yako, anayetoka chama kimoja na kuhamia chama chengine ikiwemo Chadema, si msaliti. Lakini akihama Chadema kwenda chama chengine, hasa ACT, ni msaliti. Nimekuelewa!
Muchas gracias.
Aqui esta parte del Himno del Real Madrid en espanyol:
¡Hala Madrid!, Hala Madrid!, Hala Madrid!
Enemigo en la contienda,
cuando pierde da la mano
sin envidias ni rencores,
como bueno y fiel hermano.
Tafsiri yake jwa kikwetu ni:
¡Hala Madrid!, Hala Madrid!, Hala Madrid...
Hili nina wasiwasi nalo. "Kijana" "mwanamume" wa kweli hajifichi uso, hujitokeza hadharani kudai matakwa yake au kutekeleza dhamira zake Hawa kwa wingi ni wahuni wa vijiweni (wanaotumiwa, pengine) kupandikiza mbeguza chuki kwa maslahi ya kisiasa. Tusisahngae kuona video kutoka madhahebu nyengine.
Hapa nimeona manyoya, hivyo sina haja ya kuuliza kuku kenda wapi. Rushwa na Ubadhirifu vinanukia. Takukuru iingilie kati mapema kabla ya "Escrow Part II" haijatinga bungeni.
Nchi ina laana hii!!!!!!. Lini tutajifunza?????
Ninakubaliana na wewe kabisa mkuu. Kabla ya kusoma bandiko lako nilikuwa nilieleze hilo. Ya Ngoswe aachiwe Ngoswe, Profesa Muhongo hakupaswa kukubali uteuzi wa kisiasa. Kwenye siasa kuna mitego, kuna ulaghai, kuna maadui. Kwenye taaluma hasa ya sayansi, hoja za kule ni utafiti na theories...
Polisi wetu na vyombo vyetu vya usalama, badala ya kuwa "Walinzi wa raia na mali zao", wao wamekuwa maadui nambari moja wa wananchi na mali zao. Jamani, hii nchi inapelekwa wapi?
Hivi ukisamehe ni lazima usahau? Kwa uoniwangu tu, ni kuwa kama wasingesamehe, wangebaki na kisasi na pengine siku moja kupanga kulipa kisasi hicho, lakini kwa kutosahau kwao ndio maana wanawakumbuka wahanga wao kila mwaka.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.