barabara hii mnayoiona kutoka Same kwenda milimani Chome ilichimbwa na wananchi wa wilaya ya Same kwa utaratibu wa kujitolea. utaratibu huo wa kazi za maendeleo za kujitolea unaitwa "msaragambo."
serikali ya mwalimu nyerere ilikuja kuwapa sapoti wananchi kwa kutoa baruti za kupasua muamba...
unajua mambo mengi ya wapare huamuliwa kwa mashauriano. na mashauriano hayo mara nyingi huwa marefu sana mpaka watu wafikie muafaka. na mara nyingi muafaka ukishafikiwa wote walioshiriki ktk shauri hilo hufungwa na maamuzi hayo.
mimi nimeshuhudia hata suala la ndoa za kipare; majadiliano ya...
kitu ambacho sijaona wapare wanafanya ni wachungaji wahubiri hawa wanaojiita manabii. lakini wapare wapo ktk kila nyanja, kuanzia wasomi mabingwa, wafanya biashara wakubwa, machinga, polisi, wanajeshi, mpaka kuna magaidi wapare.
Nyerere aliwakuta Wapare wanachimba barabara kwa njia ya kujitolea inaitwa "msaragambo." Moyo huo wa kujitolea na uchapakazi wa Wapare ulimfanya Nyerere atamke kwamba, " Wapare ni Wachina wa Tanzania. " Mpare ni mchapakazi na haogopi ushindani, ndio maana anaishi popote pale Moshi, Iringa...
wapare wanawapenda sana jirani na watani zao wachaga. mimi wazee wangu walinihusia kwamba mahali ambapo hakuna mpare,mchaga, au msomali, hakuna pesa kwa hiyo niepuke kuishi hapo.🤣
mpare anaweza kuishi katika jamii ya wachaga na ku'survive. jamii zingine zinawaogopa wachaga na kuwaona wabaguzi kwamba hakuna uwezekano wa mhamiaji kufanikiwa kibiashara au kimaisha ktk ardhi ya wachaga. mpare yeye anahamia popote pale moshi, arusha, tanga, d'salaam, morogoro,
ni utamaduni wetu toka kwa mababu kuamua migogoro, au mambo ya kijamii, kwa njia ya mashauriano. hata wakoloni walipofika ktk ardhi ya Wapare kitu kimoja kilichowashangaza ni huo utamaduni unaofanana na mahakama wa kuamua masuala mbalimbali yanayoihusu jamii. kwa kawaida na kwa asili yetu Wapare...
maelezo yako sio ya kweli. kabla ya uhuru wilaya ya Pare [ Same + Mwanga] ilikuwa sehemu ya Tanga Province. Majimbo yalipovunjwa na mikoa kuanzishwa ndipo wilaya ya Pare ikakatwa na kupelekwa kuanzisha mkoa wa Kilimanjaro. Pia hakuna Mangi aliyedai nchi au taifa la Wachaga. Madai hayo ni fitina...
kabila letu ni Vaathu/ Vaasu, au Vamp'hare; lugha ni Chasu / Chathu. pia kabla ya kuwa jamii iliyounganika kama kabila, Wapare walikuwa jamii ndogondogo zenye asili ya makabila mengi kama Wakamba, Wataita, Wazigua, Wagweno, Wachaga, n.k.
Hakuna jamii / koo ya Wapare ambao waliwahi kupigana...
kuna wakamba wana majina sawa na wapare na huo ni uthibitisho kwamba kuna muingiliano. wataita pia wana muingiliano na wapare na lugha zao zinafanana.
kama kuna mchanganyiko kati ya wapare na wachaga basi ni kwa kiwango kidogo sana. je, unafahamu kama kuna muingiliano wowote ule wa lugha kati...
hizo sio taarifa za kweli. Wapare ni mkusanyiko wa watu wa makabila mbalimbali kama Wataita, Wakamba, Wazigua, Wasambaa, Wachaga, Wagweno, ambao walihamia eneo linaloitwa Upare sasa hivi. Ukichunguza majina ya Wapare utayakuta ktk jamii hizo nilizozitaja hapo juu.
maeneo ya tambarare au chini...
wapare ni mkusanyiko wa koo toka makabila ya wachagga, wazigua, kwa upande wa Tanzania, na wataita, na wakamba, kwa upande wa kenya. kwa mfano, jina minja liko uchagani na upareni. jina kilonzo liko kwa wapare na wakamba. pia huyo mfumwa sabuni asili yake ni mbaga sio usangi alipokuwa mfumwa!!
Na wapare wa mwaka 1945 walikuwa na muamko wa kutetea haki zao kuliko wa sasa hivi. mwaka 1943-44 serikali ya mkoloni ilianzisha utaratibu wa kodi ya kichwa ktk wilaya ya pare. ilipofika januari 1945 wananchi wa upare waliamua kufanya maandamano na kukusanyika ktk makao makuu ya wilaya same...
Wilaya ya Same ina shule nyingi na zinafanya vibaya. Katika matokeo ya mitihani ya kitaifa wilaya ya Same imekuwa ikishika mkia ktk mkoa wa Kilimanjaro. Data kwamba wilaya ya Same inashika mkia kielimu mkoa mzima zipo ukizitafuta utazipata...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.