Nimemsikia mgombea urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli, kwenye kampeni zake zinazoendelea huku kanda ya ziwa, amekua akitumia kisukuma mara kwa mara.
Hatukuwahi kusikia Rais yoyote waliotangulia wajifanya kama anavyofanya magu.
Najiuliza tu, wagombea wengine wa vyama CHADEMA, ACT Wazalendo, CUF...
Naishauri serikali, kuwepo na gates kwa ajili ya kupima wasafiri waingiao na watokao katika mikoa hiyo. Mfano Dar, gate za upimaji abiria wote ziwekwe kwenye njia zote za mabasi yaingiayo na kutoka Dar, hali kadhalika kwa mikoa yote, hii itasaidia kufanya mass testing na kuzuia uenezi kwenye...
Wakuu,
Leo wakati mkuu wa nchi anakagua pale Ubungo interchange, ni dhahiri kabisa mkuu kuna kitu kimemuudhi, yule hisia zake hazifichiki, nadhani kuna kitu Mfugale amemkwaza Mh Rais.
Mimi binafsi sikupenda Mfugale alipokuwa anatoa maelezo kwa kutumia lile lifimbo lake la kutembelea kila mara...
Kuna baadhi ya wanafunzi nawafahamu wametoka miongoni mwa shule hizi zinazoongoza kitaifa/form 4, wanapokuwa A level au hata chuo ukweli ni tofauti kabisa na ufaulu wao wa O level.
Hebu Wizara husika chukueni jukumu la kuwaita hao wanafunzi wa St. Francis wote na kisha just tafuteni utaratibu...
Wale ma superstar ambao kila kukicha mumekua na tabia ya kuishambulia hii treni, eti watu wa kaskazini hawatapanda, napenda kuwataarifu kua treni inajaa kila siku, na imeongeza idadi ya safari kwa wiki kutokana na demand kua juu, naomba msiwe mnapinga juhudi za serikali inapowaletea wananchi...
Huwa nawaona nazo walinzi wa viongozi mbalimbali, almost dunia nzima type ni ileile, je kwa mwenye ufahamu ni miwani za kawaida au ni special na zina nguvu /ufanisi wa ziada, kwa anaefahamu please
Nalizungumza hili nikiwa nimekumbana nalo mara kadhaa ninapokwenda TRA kulipa kodi, misururu ni mirefu na wafanyakazi wa TRA kumsikiliza mteja ni changamoto hasa ukizingatia umati unaomsubiri, athari za foleni hizi ni nyingi, ila kubwa ni kushuka kwa mapato. Uongozi wa TRA ni jukumu lenu...
Kwa hali ilivyo, kuwa watu fulani watatumia gharama na rasilimali zao ili mtu wao ashinde uchaguzi, je kuna sababu ya kupanga foleni kupigwa na jua ilhali unajua matakwa ya chama tawala ? Mifano ni mingi, mimi binafsi nimeapa sintakaa nipige kura labda utaratibu unadilishwe, eboo, huku ni...
Hivi karibuni tumesikia toka kwa waziri wa nishati, ambaye pia ni mbunge wa chato, kuwa serikali imedhamiria kujenga uwanja mkubwa wa mpira ambao utakuwa wa pili baada ya ule wa dar es salaam. Nimekua na maswali mengi pasi na majibu. Na kama kweli serikali imedhamiria kufanya hivyo naomba...
Naandika kwa masikitiko, ninaposoma magazeti, maandiko mbalimbali nk kwenye mitandao, au hata kusikiliza mazungumzo ya vijana wetu wa leo nagundua kuna shida kubwa sana kwenye lugha yetu, herufi "h" imepotea kabisa, mfano ni maneno yanayohitaji" H" yanapewa "a, e, i,o,u" mfano akuna, ata kidogo...
Naandika nikiwa na uchungu sana, hoja nyingi za hapa JFzinaonyesha ni jinsi gani ndugu zangu watanzania tusivyokuwa wazalendo mwendo uliopo ni kutukana Serikali hata ambapo haistahili, najaribu kupitia threads za JF za wenzetu nchi za jirani, wao wana support kubwa sana kwa nchi zao, regardless...
Mimi ni mpenzi wa kipindi cha jahazi ila ukweli hiki kipindi bila kibonde (RIP) kimepwaya, Captain na George Bantu nawaomba msikate tamaa hizi ni changamoto za maisha
Ni katika kujua tu, kwa anae fahamu naomba anijibu, Serikali ya Morocco ni tajiri kiasi gani hadi watujengee uwanja, je kwao ki miundo mbinu kama hiyo wako vizuri sana ? Je kuna malipo yoyote/faida toka kwetu, mwenye jibu la uhakika naomba anielimishe, tafadhali kama huna jibu ni bora ukae kimya
Hili suala linazidi kunishangaza, kila kona, mji mzima utawakuta kuanzia 6-10 wakiwa na vidubwana vyao vya kutolea risiti, ole wako ukutane nae, atatafuta kila sababu ili tu ulipishwe faini ya 30,000/= sio siri hii pesa hua inauma sana hasa ukizingatia hawa jamaa ni kama wametumwa wakusanye...
Kila kukicha tunaambiwa makundi ya vijana/kina mama wanatakiwa kupewa mikopo, kutoka katika makusanyo ya halmashauri husika, jamani hiki kitu kipo kweli? Nimekua nikimsikia naibu waziri wa ajira, vijana ... mikakati mbalimbali kuhusu vijana hususan kuwezeshwa kibiashara nk, hivi vitu vipo ...
Huyu ni raia wa Saudi Arabia ambae ameajiriwa na serikali ya nchi hiyo hususan katika hukumu za kunyonga kwa kuchinja watu, na anakiri kuwahi kuchinja hadi watu 3 kwa siku, na anapinga kuwa kuchinja binadamu sio ukatili, msikilize hapa
Ni ukweli usiopingika, kwamba hii vita ni ngumu. Tuhuma zote sasa zinamuendea mtu mmoja na ukiangalia kwa undani kwa namna moja ama nyingine wote wanaopeleka mashambulizi kwa huyo mtu ni kwamba kama hajaguswa yy basi ni mtu wa karibu yake. Imefika mahali sasa mjadala umehamia kwenye maisha yake...
Ni kijana wa takriban miaka 8 amefariki dunia kwa kung`atwa na mbwa ambae anasadikiwa kuwa na kichaa. Mtoto wa kiume wa rais mteule wa Gambia, Adama Barrow amefariki akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuumwa na mbwa.
Habibou Barrow alifariki Jumapili baada ya kukumbwa na mkasa huo katika...
Ndugu zangu, katika harakati za kutafuta mkate wa kila siku nimezunguka baadhi ya mikoa, ila ki ukweli hali inatisha na kusikitisha, juzi nilikua Arusha, mji umeharibika, maeneo karibu na soko kuu machinga wanapanga bidhaa mpaka barabarani, jana asubuhi nawahi stendi ili nisafiri kurudi kwenye...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.