Sidhani kama nchi za kigeni zinaruhusu watu wa nchi nyingine (wageni) wafanye shughulu zao za kisiasa nchini mwao. Kwa mfano siamini kuwa Tanzania itaruhusu watu wa Rwanda, Burundi, DR congo, Kenya, Zambia, Uganda na kwingineko, waje wafungue matawi ya vyama vyao mabali mbali vya kisiasa. Huo...
Nafikiri sababu kubwa ni hii posho/ruzuku. Chama kinachokuwa na wabunge wengi ndicho kinachopata ruzuku nono. Kwa hivi vyama havina njia nyingine ya mapato ya kukidhi, kila chama kinawania kupata wawakilishi/wabunge wengi iwezekanavyo. Wanachama michango yao ni ya kusuasua. Mara nyingi hawatoi...
Kila nchi katika dunia ina matatizo yake. Tusiwasahau wenzetu wa Tarime wanaochinjana kila kukicha ndani ya nchi yetu. Na bado nasi tunazungumzia hiyo hiyo E.A.Federation ambayo Makao Makuu yake tunayo Arusha.
Nyerere, Mroman Catholic, Rais wa Kwanza wa Tanzania, alipotambua kujitenga kwa wa Ibo, Waroman Catholic wa Biafra ya Nigeria hiyo hiyo, huku akitaka muungano wa Afrika, alikuwa shujaa.
Gadhafi, Muislamu, Rais wa kudumu wa Libya, anapotaka kujitenga kwa Waislamu na Wakristo wa Nigeria, huku...
Kwa masikitiko makuu na hudhuni nyingi naipokea taarifa hii. Nilimfahamu Daudi tangu siku za ujana wake akiwa TANU mpaka katika uzee akiwa UN. Alikuwa mchapa kazi mahiri sana, mcheshi na mkarimu.
Mungu ampe makazi mema yanayomstahili na awape nguvu wafiwa ya kustahimili msiba huu mkubwa. Ameen!
Ule msemo wa kisheria unaodai kuwa "mtuhumiwa hana hatia, mpaka pale mahakama itapomtia hatiani" unahitajika hapa.
Tuwaonee huruma waliotapeliwa kwa kiwango kile kile tunachohitajika kumwonea huruma aliyetuhumiwa.
Kwa hakika Ali Abeid Amani Karume, bila ya kujali jina lake, anayo haki ya msingi ya kikatiba, kugombea nafasi yoyote katika nchi yake ya Tanzania kama alivyo na haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi yeyote anayemtaka. Ni unyanyashaji na ubaguzi wa hali ya juu sana kumnyima haki yake hiyo...
Usijute kuzaliwa Tanzania. Jilaumu kwa kukaa pembeni ya ulingo na kulalamika. Mvunja nchi ni mwananchi. Nini mchango wako katika kuirekebisha nchi yako? Viongozi wa nchi wanatokana na wananchi wake. Viongozi wabovu wa wananchi wanapatikana miongoni mwa wananchi wabovu. Ukweli unauma.
Wananchi,
Kabla hatujalinganisha ufanisi wa miaka 15 ya Chadema na ile miaka 50 ya TANU/ASP/CCM, inatubidi, ili kupata usahihi wa jawabu, inatupasa kwanza tuviweke vyama hivi vyote viwili katika mizani moja na uwanja tambarare wa ushindani.
Tumejiuliza?
Kwani TANU au ASP ilifanya kitu...
Unapowalinganisha Waalimu ni lazima pia uwalinganishe na wanafunzi wao. Huwezi kusema Mwalimu fulani hodari kuliko mwenzake, eti kwa kuwa wanafunzi wake wengi wamefaulu. Je, wanafunzi waliofeli kule kwa mwenzake wakoje? Kuna wanafunzi wasioweza kufundishika hata wakipewa mwalimu gani. Pamoja...
Tukiirudia historia ya Muungano wa Tanganyika kimakini, tutagundua kuwa huu muungano haufanani na muungano wowote uliowahi kutokea kabla yake. Na hicho ndio kiini cha kero zote za muungano tulizonazo na tunazokabiliana nazo. Kusema kweli hatuna muungano wa nchi wala serkali zetu. Muungano huu...
Katika vitu vibovu ambavyo tumerithi kutoka TANU/CCM ni ujinga na uwoga. Ujinga wenyewe si wa kusoma shule ni ule wa kutotambua haki zetu na tunapozitambua hatujui jinsi ya kuzipata na tunapozipata hatujui kuzidumisha wala kuzistawisha. Uwoga ni ule wa kutokuwa na ujasiri wa kuthubutu.
Ndani...
Maalim Seif Shariff Hamad na Ibrahim Lipumba maadamu wanakubaliwa kugombea Urais wa Zanzibar na Tanzania na wanachama wao wa CUF kwa mujibu wa katiba ya chama chao,
wana haki ya msingi ya kugombea nafasi hiyo kwa miaka 26 na zaidi. Haki hii hata Julius Nyerere alikuwa nayo katika TANU na CCM pia.
Waungwana,
Mtu jina lake ndilo linalomtambulisha yeye mmoja pekee katika kundi. Mathalan, mtu akisema jina lake John au Kidawa au Ali anakuwa hajajitambulisha kikakamilifu kwa kuwa ametumia jina la kawaida. Kuna akina John au Kidawa au Ali kibao. Na akitumia jina la ukoo pekee, kwa mfano...
Waungwana,
Kama viongozi wa CUF - Mwenyekiti Lipumba na Katibu wake Hamadi wanatuhumiwa kung'ang'ania viti vyao, basi nafikiri na huyu ndugu yetu ni mng'ang'anizi wa cheo chake. Yale yale ya Tambwe Hiza. Viongozi wote wa Tanzania ndivyo walivyo. Pakiwa na mtetereko wowote katika nyadhifa zao...
Waungwana,
Kujibu swali ni kulielewa swali. Kipi Kiswahili sahihi? Hapakutajwa dini kwenye swali? Jinsi gani sahihi katika utamaduni wa Kiswahili? sio utamaduni wa kidini!
Mama katika Kiswahili sanifu ni yule mzazi, awe mzaa mtoto au mzaa chema. Lakini, katika utamaduni wa Kiswahili, jina...
Tukiangalia bila kupenda sana, mwenye kupenda sana, chongo huita kengeza. Tanganyika kabla ya uhuru wake, ilitawaliwa na Mwingereza na Zanzbar ilitawaliwa na Sultani Jamshidi ambaye utawala wake ulilindwa na Uingereza.
Utawala wa Mwingereza uliondoa utawala wake Tanganyika kwa maana ya...
Hatua ya kwanza ya kujibu swali lolote ni kulielewa swali lenyewe. Nimesoma majibu mengi humu yanayoonyesha wanaojibu wanatoa maelezo mengi na mazuri, lakini hawajibu swali.
Usemi kuwa "anayejuwa baba wa mtoto ni mama" una ukweli wenye uzito mkubwa sana. Lakini, ukweli huu si ukweli mtupu...
Unahangaika bure, huyo mtoto ni wa mumeo. Kuzaa hata kuku anazaa. Baba ni kulea na upendo wa dhati. Siamini kuwa mama ndiye mwenye kujua ameshika mimba ya nani kwa uthabiti. DNA imeshawaibisha akina mama wengi wanaodai kuwa mtoto wao ni wa fulani.
Ungekuwa unampenda kweli mumeo, usingekaa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.