Prof naye anatuchanganya kweli!!!!! Hivi siku zote alikuwa wapi kusema hayo aliyosema leo, je hayo makubaliano yaliyokiukwa ni yapi na kwa nini asingesema mapema? Kitu gani kimemtokea? Sasa tuelewe kipi mara inasemekana tatizo lipo kwenye uongozi wa chama chake leo anasema tatizo ni ukawa. Kwa...
Daaaaaa! Ametuacha katika sintofahamu kubwa maana wakati huu tunaoelekea kwenye mabadiliko makubwa ya kiuongozi katika taifa letu mchango wake ulihitajika sana akiwa katika nafasi ya mwenyekiti wa chama na si mwanachama wa kawaida.
Nape ameamua kusema chama kimehujumiwa, baada ya kukosa maneno ya kusema. Hivi awali alipotamba kuwa chama chake tayari kimeshashinda katika uchaguzi huo hata kabla ya siku ya uchaguzi hakujua kama wananchi ndio wanaoamua nani awe mbunge wao?. Au alifikiri yeye ndo kila kitu.
Mh.Sitta anatakiwa akubali bila kushinikizwa kuwa chama chake hakina sera, wala asijaribu kumtaja mgombea kuwa ndiye sababu ya kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi wa Arumeru
Hakuna hujuma wala mtoto wa hujuma, CCM ilishapoteza dira toka siku nyingi tu, hicho tulichokiona Arumeru ndo matokeo yenyewe, hata kama wangehutubia wananchi hadi wakawapigia magoti,na kulia sana bado wasingeshinda.
Nape alitamba kuwa chama chake kitashinda kwa kura nyingi kuliko kilizopata Igunga, yako wapi aliyosema kama siyo aibu tupu. Hongera CHADEMA kwa kuongeza idadi ya makamanda wa kupinga ufisadi
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.