Search results

  1. Mystery

    Ni kwanini kushambuliwa Kwa risasi Mbunge Sendeka, kushughulikiwe Kwa haraka na Polisi, wakati lile la Tundu Lissu halishughulikiwi kabisa?

    Tukio la kushambuliwa Kwa risasi gari alilokuwemo Mbunge Ole Sendeka, ni baya mno na linafaa Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi ili kuwabaini waliotenda uovu huo. Hata hivyo Kwa taarifa zilizotufikia zinasema kuwa tayari hivi sasa, kuna timu ya wataalamu, kutoka Jeshi la Polisi, limetumwa...
  2. Mystery

    Benki ya Dunia imefichua ukweli kuwa lindi la umasikini linaongezeka kwa watanzania!

    Tofauti na propaganda za serikali ya wanaccm za kila mwaka, kuwa uchumi wa watanzania unakuwa kwa asilimia kubwa kila mwaka, benki ya Dunia imewashushua waendesha propaganda hizo kwa kueleza ukweli kuwa hali ya maisha ya watanzania walio wengi, hususani wale wa hali ya chini, inazidi kudorora...
  3. Mystery

    Fred Lowassa kumshukuru Rais Samia pekee kwa matibabu ya Baba yake, atakuwa amekosea

    Nilimsikia Fred Lowassa katika salaam zake za rambirambi pale Karimjee Hall, akitoa shukurani zake za dhati Kwa Rais Samia Kwa matibabu ya Baba yake, Hayati Edward Lowassa na kwenda mbali zaidi Kwa kutamka kuwa kama siyo Kwa msaada mkubwa aliotoa Rais Samia, baba yake asingeweza kufikia majuzi...
  4. Mystery

    Makonda amesema kweli; wengi wa viongozi wa Serikali hii ya CCM wanafanya usanii kumpa sifa Rais Samia, lakini kivitendo wanamhujumu

    Pengine mtu mbaye anabeba vichwa vya habari kwa sasa kuliko mtu mwingine yoyote hapa nchini kwa sasa ni Paul Makonda aka Bashite. Watu wanajiuliza maswali mengi, iweje mtu huyu huyu, kwenye utawala wa awamu ya 5, chini ya Mwendazake, alionekana kuwa ni mhalifu mkubwa, leo hii kwenye utawala wa...
  5. Mystery

    TANESCO wanalazimika kubeba hasara kubwa tunazopata wananchi, kutokana na mgao wao wa umeme, usio na ratiba maalum

    Hivi sasa siyo tena habari, kuona maeneo kadhaa ya nchi, yakiwa yako gizani, kutokana na mgao wa umeme, ambao ni "endless" bila ya TANESCO kutoa taarifa za mapema, kuwa kutakuwa na mgao wa umeme katika maeneo hayo husika! Nyinyi watu wa TANESCO hebu jaribuni kufikiria, hizo hasara kubwa...
  6. Mystery

    Ni kwanini wabunge wa CCM waendelee kung'ang'ania wakurugenzi wa miji wawe wasimamizi wa uchaguzi, licha ya hao wakurugenzi kukosa sifa?

    Moja ya malalamiko makubwa kabisa ya chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema na wananchi walio wengi nchini, ni kukosoa suala la wakurugenzi wa miji kuwa wasimamizi wa uchaguzi Mkuu. Ni jambo lililo wazi kuwa katika suala zito sana la uchaguzi Mkuu, ni lazima wanaopangwa kusimamia uchaguzi...
  7. Mystery

    Hivi vile vyama 13 vya upinzani, vilivyoamua kuungana na CCM, kuwapinga Chadema, wanajisikiaje hivi sasa baada ya kuona maandamano hayo yamefanikiwa?

    Baada ya Mwenyekiti wa Chadema kuutangazia Umma kuwa chama chake kinategemea kufanya maandamano ya amani jijini Dar tarehe 24 mwezi huu, kama kawaida viliibuka baadhi ya vyama, wakiongozwa na CCM kuyapinga maandamano hayo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, maandamano hayo ya amani...
  8. Mystery

    Kuruhusu maandamano ya amani ya Chadema, je Rais Samia ameshawachoka wahafidhina wa CCM wasiotaka mabadiliko nchini?

    Kwa kweli leo tarehe 24, inabidi iingie katika historia kwa nchi hii, kwa kuwa ni kwa mara ya kwanza, tokea tupate uhuru kwa serikali yetu kuruhusu maandamano ya amani ya chama cha upinzani! Ingawa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) na 18(2)...
  9. Mystery

    Rais hana Imani na wananchi wake hadi aingie kwenye nyumba za ibada na walinzi wake?

    Kwa kweli huwa najiuliza, lakini nakosa majibu, hivi inakuwaje Kwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, aingie na walinzi wake na huku akichukua hadi kiti chake Cha Ikulu, ili akalie kwenye nyumba za ibada, Huku akilindwa na walinzi wake zaidi ya wawili? Hivi hatuoni kuwa hatuishi na maneno...
  10. Mystery

    Mgao mkali unaoendelea hapa nchini, unatokana na ilani ya CCM ya kutaka "sifa" ya kusambaza umeme katika Kila Kijiji!

    Kwenye biashara kuna kitu kinachoitwa "demand and supply principle" Unapoona mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wako wa kuhudumia, kinachotokea baada ya hapo ni upungufu mkubwa wa huduma hiyo, ambayo inaweza kusababisha kitu tunachokiita "chaos" Niseme wazi kuwa kutokana na mgao mkali sana...
  11. Mystery

    Ni kauli ya "kishamba" mno aliyotoa Chalamila, kuwa tarehe 24, majeshi yetu yote yatakuwa yanafanya usafi jijini!

    Nimestuka sana nilipoisikia kauli aliyotoa mkuu wetu wa mkoa wa Dar tena kanisani, kuwa tarehe 24, "anawaagiza" askari Polisi 5,000 na askari wa JWTZ 8,000 wajitokeze mitaani Dar, ili wafanye usafi! Kustuka kwangu ni kuona Mkuu wa Mkoa, asivyoelewa majukumu ya Hawa walinxi wetu, Kwa kuwa Jeshi...
  12. Mystery

    Kuzidi kushuka Kwa bei ya mafuta, LATRA iitishe kikao Cha dharura, ili kushusha bei ya usafiri

    Bei ya mafuta ya petroli nchini imezidi kushuka. Katika bei zilizoanza Leo, mafuta ya petroli yameshuka bei hadi shilingi 3,040 Kwa Lita moja, kwa Jiji la Dar, kutoka bei ya mwezi uliopita ya shilingi 3,158 Nawaomba sana LATRA waitishe kikao Cha dharura, ili kupokea maoni ya wananchi, ili...
  13. Mystery

    Tunawataka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhi (LATRA) wasitishe mara moja, tangazo lao la kupandisha nauli za mabasi

    Sisi wananchi wa nchi hii tunawataka, mamlaka ya Udhibiti usafiri wa Ardhi (LATRA) wasitishe mara moja, tangazo lao la kupandisha nauli, ambalo wao walisema zitaanza rasmi kesho kutwa, terehe 8 mwezi huu Nimesema sisi watanzania, tunawataka hao LATRA wasitishe mara moja, tangazo lao, Kwa kuwa...
  14. Mystery

    Watawala kutumia mbinu ya kutaka kutoa elimu ya Katiba Kwa miaka 3, wanataka KUTULAZIMISHA tuendelee kutumia milele Katiba tuliyonayo sasa!

    Baada ya kauli ya aliyekuwa waziri wa Katiba, Dkt Ndumbalo kusema kuwa watatoa elimu ya Katiba Kwa miaka 3, nilidhani kuwa huo ulikuwa ni mtazamo wake na siyo wa chama chake. Hata kuondolewa kwake kwenye wizara hiyo na kupelekwa kwenye wizara ya michezo, niliamini kuwa ilitokana na kauli yake...
  15. Mystery

    Kama waziri Mwigulu anakataa kuwa pesa hazijaibiwa serikalini, ina maana kuwa anapingana na ripoti ya CAG?

    Wakati akifunga mjadala wa bajeti ya wizara ya Fedha ya mwaka 2023/2024 waziri Mwigulu alinukuliwa akiwaambia wabunge kuwa, kama ripoti ya CAG inadai kuwa pesa nyingi zimeibiwa serikalini, je pesa yote anayoitoa Rais Samia kwenye miradi mbalimbali nchini, angezitoa wapi, iwapo pesa nyingi...
  16. Mystery

    Kuna "jam" ya kufa mtu hapa Maseyu-Morogoro!

    Tumekuwa kwenye foleni ya magari toka Saa 7 mchana, Hadi muda huu wa saa 11 jioni, ndiyo foleni hiyo ya magari imeanza kufunguka. Tunaomba watu wa "traffic Police" watueleze tatizo lilikuwa nini? Kwa kuwa watu wengi wameathirika Sana Kwa kuchelewa kufika makwao Kwa zaidi ya massa 3
  17. Mystery

    Waliotuibia mabilioni ya shilingi za pesa za Umma, kama wamegona kutupisha, ni kwanini Rais aliyewateua, anashikwa na "kigugumizi" kuwafukuza kazi?

    Hilo ndilo swali kubwa ninalojiuliza, ni kwanini hao watendaji wetu wa Serikali, ambao wanafahamika hata Kwa majina, waliotajwa kwenye ripoti ya CAG, kuwa wamefisadi mabilioni ya shilingi za Umma, ni kwanini Rais Samia Suluhu Hassan, hawatengui kwenye nafasi zao, wakati ni yeye mwenyewe ndiye...
  18. Mystery

    Tumsaidie Rais wetu kwa kuwazomea hawa wezi wa Mali ya Umma bila kuchoka

    Tumesikia madudu ya kutisha, kama yalivyobainishwa na CAG, namna watanzania wenzetu, wasio na uzalendo hata kidogo, namna wanavyotafuna fedha zetu za Umma bila woga, Kwa kutuibia mabilioni ya pesa. Hivi Hawa watumishi wachache wa Umma, wanatuona watanzania wote kuwa ni wajinga? Hivi hizi...
  19. Mystery

    Ugonjwa unaodaiwa na Wizara ya Afya, ulioua watu 5, unaweza kuwa ni Ebola?

    Imetolewa taarifa na wizara ya Afya na Profesa Tumaini Nagu kuwa huko Bukoba vijijini, katika Kata ya Maruku na Kanyangereko, kumetokea ugonjwa usiojulikana, ambao dalili zake ni kutoka damu mfululizo, kwenye sehemu mbalimbali, ikiwemo puani, hadi Figo zinazshindwa kufanya kazi, uliosababisha...
  20. Mystery

    Je, Rais Samia kutoa kauli ya "Mwanaume ni yule anayejiamini" ni kijembe Kwa Hayati Magufuli?

    Rais Samia ametoa kauli yenye utata mkubwa, wakati wa ziara yake huko Usa River, Arusha, hapo majuzi. Wakati akitoka kwenye semina elekezi ya viongozi waandamizi huko Arusha, alitoa kauli hii wakati anazungumzia ujio wa Godbless Lema, hapa nchini, kuwa "Mwanaume ni yule anayejiamini" na...
Back
Top Bottom