Huyu Sabaya japo siujui uovu wake kiundani sana, lakini ninachofahamu ni kuwa alikuwa akiwapigania watawala sana.
Huenda ilikuwa ni ajira yake, lakini alikuwa hodari sana wa kuitetea serikali na kuipigania.
Alishiriki kuwakakandamiza wapinzani kwa namna moja ama nyingine ili kulinda maslahi ya...
Sijui tu hii dhana watu waliitoa wapi!
Kwamba eti ili mwanaume awe rijali lazima afundishwe na aelekezwe, ikiwemo na pamoja na kuoneshwa hulka za kiume ili aziige.
Wengine wakasema kwamba, sababu mojawapo ya watoto wa kiume kuwa mashoga ni ukosefu wa malezi ya baba. Eti hawakuwa na 'role...
Haya mabarakoa yamejaa usanii mtupu.
Ukiingia ofisi ya umma unalivaa. Ukitoka unalivua.
Hata mama yetu akiwa ughaibuni analivaa. Akishuka uwanja wa ndege analivua anaendelea kupuyanga.
Mabarakoa yamekuwa kama fasheni ya kubandika na kubandua. Unaangalia tu mazingira muafaka.
Barakoa...
Hakuna mahali popote katika historia ya nchi hii, kabla ya ukoloni, kwamba palikuwa na machifu.
Machifu ni watawala wa mkoloni waliosimikwa kwa ajili ya kazi ya mkoloni. Divide and Rule tactics. Hawa ndio waliohusika kuwauza wenzao utumwani.
Neno lenyewe ni la Kiingereza "CHEIF".
Baada ya...
Hii tamaduni ya marais wa nchi kugangamara kwa kila jambo hauna afya kwa taifa.
Umeelekezwa, sikiliza. Rais sio Mungu, lazima ukosolewe ikibidi.
Lazima nchi ijifunze kujitegemea. Huwezi kuwa taifa la kuomba omba kila siku. Ni kujilemaza.
Ni kweli, inawezekana kujitegemea kiuchumi ni jambo...
Mpendwa Mama Samia,
Nchi hii haiwezi kujengwa kwa kuomba omba. Nchi inajengwa kwa kazi, bidii, na nidhamu ya utumishi wa umma.
Nchi yetu imebarikiwa kila aina ya rasilimali: Maji, Mito, Mabwawa makubwa, maziwa, madini ya kila aina, gesi, mafuta, chakula, nishati, ardhi kubwa yenye rutuba...
Kwa jinsi ambavyo hii nchi ilikuwa inaendeshwa na genge la mafisadi chini ya utawala wa awamu ya nne, ni wazi kwamba bila Magufuli, CCM ingeshakuwa imejifia kabla ya 2015.
Uzembe, udhaifu, wizi, ubadhirifu, ulegevu na mauchafu ya kila aina yaliyoratibiwa na Rais wa awamu ile, yalifanya wananchi...
Kwanini huyu mama yetu mpendwa samia analalamika tu bila kuchukua hatua?
Wananchi wanapenda kuona Rais mwenye uwezo wa kutumia Mamlaka tuliyompa.
Yaani watu milioni sitini wa nchi hii, wote kwa pamoja tumekukabidhi wewe mamlaka yote lakini bado unalia lia tu kama mtu mwingine wa kawaida...
Nawasalimu kwa Jina la Mungu muumba wa mbingu na ardhi.
Jamani, kusafiri ni jambo jema katika kujenga diplomasia na mahusiano ya nchi na nchi. Haipingwi wala haina neno.
Lakini hii kutwa mama wa nchi kukimbizana angani kila wiki inakuaje?
Leo yuko Scotland, kesho Cairo, kesho kutwa Ubelgiji...
Kuna mzee mmoja ana umri wa miaka 70 hivi. Ni mstaafu wa Idara ya usalama wa Taifa.
Mimi sifahamu vitengo vilivyo ndani ya idara hii, kwahiyo sijui ni kitengo gani ndani ya idara alichokuwa anafanya kazi lakini alikuwa humo.
Alikuwa ni Land lord wangu miaka kama minne iliyopita. Ni mzee lakini...
Cc: Andiko hili liwafikie wanasheria na wote wenye kuhusika.
Nchi yetu ina Katiba, sheria, kanuni, miongozo na taratibu — za ndani na za kimataifa.
Katiba yetu inatambua haki ya kuishi, kulindiwa afya, kuwa na maamuzi sahihi na taarifa sahihi juu ya yote yahusuyo mustakabali wa maisha yetu...
Huu uharamia wa kodi mpya za miamala ya simu unapaswa kusimama.
Wanasheria wetu mtusaidie hili. Hakuna kitu kinachoitwa sijui "kodi ya uzalendo" — Lazima Mahakama iweke ZUIO la hizi kodi za kitapeli.
Hauwezi ukakata kodi mara tatu kwenye muamala mmoja. Huo ni uhuni na wizi.
Hizi ndizo kodi za...
Huyu anayeitwa Anthony Mtaka ni muda sasa nimeanza kumsikia lakini sikumtilia maanani kivile. Hata wakati wa Magufuli nilikuwa namsikia sikia tu kwamba ati ni Mkuu wa Mkoa bora. Akapewa sijui na tuzo!
Binafsi sikuwahi kumfuatilia kwa sababu sikuwahi kuvutika nae. Nilikuwa namsikia sikia tu kwa...
Ukisikia "kizungu-chefu chefu" ndio cha huyu Bwana mdogo nguli wa bongo fleva.
Huyu Bwana mdogo wa Tandale sijui katoa wapi hii kizungu ya kimarekani? Sijui ndio kuwa NIGGA? — Bado sijamuelewa vizuri.
You garrah gooh... i garrah duuh, i garrah fyoko, yoooo ma nigga, i garrah nyokooh...
Hey,
Nawasalimu kwa Jina la Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Hivi majuzi juzi tumesikia taarifa lukuki kuhusu corona. Wengine nimesikia wanasema kwa sasa hili ni wimbi la tatu — Wengine wanaita sijui DELTA kitu gani gani??
Majina yamekuwa mengi kidogo. Kuna DELTA na kuna wimbi.
Kiuhalisia...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.