Kwa sababu unaona wamevaa gwanda wanafanana na wale walinzi wa Security za mtaani.. nyamaza tu kama hujui uangalie michango ya watu labda utaelimika kuliko kuita watu wajinga.
Huko jeshini kuna kozi nyingi sana wanapitia mpaka kufika hapo.
Unazani ni rahisi tu mpaka kuwa mlinzi wa Rais.
Ndugu ukoloni haukuishia tulipopewa bendera ila tuna njia ndefu mpaka kufikia Uhuru wa kiuchumi.
Tulitawaliwa kisiasa na Kiuchumi kisiasa tuliachiwa kupandisha bendera zetu ila bado wanacontrol kila kitu bado tumejiingiza kwenye mikataba ya kimataifa ambapo inatubidi kufuata wanavyotaka...
Hukunielewa sibishani na kazi kubwa alizofanya kama Rais wa Marekani.
Obama anaondoka kama Rais kipenzi cha wamarekani wengi, mwanasiasa na mwanadiplomasia mzuri.
Ila kwa upande wa kutetea haki za watu weusi wa Marekani na ndugu zake wa Africa huku tunatafuta legacy yake kwa tochi.
Ni kweli kwa kiasi flani ila takwimu zinafikirisha na kuonesha kuwa wanalengwa na system. Kuna idadi kubwa wanaouwawa bila hata kuwa na silaha, vijana wengi weusi wamekua wakipikiwa kesi na mahakama kuendelea na kesi za hizo zisizo na mashiko na mengine mengi
SIJAKURUPUKA kila mmoja anapimwa kutokana na nafasi aliyoipata kwenye jamii, waliokuja kumtetea Obama wamezungumzia Obamacare ambayo naona ndicho hicho tu atakachokumbukwa.
Sasa kama Obamacare is his only legacy huoni kama amefanya chini ya matarajio ya wengi.
Mugabe alipowagusa settlers kule Zimbabwe alipigwa vikwazo mpaka leo hii wakati mpaka sasa wengi wa wale masettlers ni wazaliwa wa Zimbabwe... kama hatutaangaliana kama ndugu tutashindwa kwenye hii vita
Hatuhitaji Misaada zaidi ila kwa position aliyonayo hata kukemea hayo maovu yanayoonekana.
Hauachi mambo yakaenda hovyo kwa kisingizio cha viongozi wa Afrika hawajitambui..sasa kama hao ndio viongozi wa Afrika hao wananchi huko chini hali ikoje?
Kwa watu wanaofuatilia mwenendo wa vuguvugu la BLM utagundua wengi bado wanalalamikia sheria nyingi kandamizi dhidi ya mtu Mweusi wa Marekani.
Hata kama huku kwetu Afrika tutakua tukimtwisha mzigo mzito sisi tutajipambania wenyewe.
Ila swali la msingi linabaki kuwa amewafanyia nini wamarekani...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.