Umekasirika sana!
Samahani sana kwa kukukosea, ni aula sana kufanya mijadala na watu waliokuwa na busara na hekima kubwa kama wewe. Nilidhani kuwa Kuna kundi ambalo limependelewa na wengine wakaachwa kulingana na maelezo yako ya awali na hata haya.Kumbe si hivyo nimekosea nisamehe bure maana...
Mjadala unaonesha jinsi watu walivyo watupu katika kuchambua vitu vidogo sana kwa mantiki.Hivi unapozungumzia kufunga ni sawa kwa Muislam na mkristo? Je mkristo anafunga kwa ajili gani, wakati gani, anafunga mambo gani nk.Ukimaliza hapo uliza Muislamu anafunga kwa sababu zipi? wakati gani?Je...
Kwani sasa hivi hayo masomo ya dini yanafundishwaje?.Maana wanafunzi wanafanya mitihani na wanaofaulu wanafaulu na wanaofeli wanafeli. Kwakuwa hakuna atakaye lazimishwa kusoma tahasusi yenye Somo la dini wanaotaka wasome wapewe nafasi.
Suala hapa siyo Kodi,mtoa mada uwe wazi unahofu na Hilo box.Nami nimekuelewa hapo kuwa unahofu na matokeo ya wale watakao fundishwa hasa upande Wa pili.Usipige chenga kusingizia Kodi kwani hao wengine hawalipi Kodi. Masomo ya dini zote yanafundishwa acha watoto wanaotaka wasome.Wengine hawana...
Bado Sijapata mantiki ya hoja ya kupinga tahasusi mpya.Ina maana mwanafunzi anaposoma Somo la dini na masomo mengine mawili tena Kwa hiyari yake ni madhara gani hutokea?.Mbona wanapoenda vyuo vikuu zipo shahada zinazohusu dini.Nilidhani labda watakosa maarifa ya awali wanapoanza shahada zao...
Nimepeleka cheti wakati anaanza darasa la kwanza na mwezi Wa January akiwa darasa la nne nilipigiwa simu nipeleke majina nikaenda na cheti kwamba wanasajiliwa.Hata hivyo majina yaliyokosewakwenye hii ilikuwa ni zaidi ya watoto kumi mbona ikaisha baada ya watu kulalamika?Uzembe upo.
Anayesajili ni nani kwenye huo mfumo? Kama walimu wakuu hawasajili kwenye mfumo liwe wazi maana kunakutupiana mpira .Sisi ni Watanzania na wadau Wa elimu tungependa watu waliopewa dhamana na taifa watutendee haki kwa mujibu Wa majukumu yao.Mpaka hapa naona Kuna walakini.
Mwalimu inabidi utuelimishe taratibu.Wengine tunafuatilia jambo hili kwa ukaribu kwa kuwa limetuathiri.Mimi nimefika Hadi shuleni kupeleka nyaraka za mtoto wangu kwa maelezo kuwa usajili unafanyika.Baada ya kufikisha nakala ya cheti ninapaswa kufanya Nini zaidi ya hapo?.Matokeo yanatoka jina...
Mwalimu umeghadhibika.Maneno yako yanakuondolea Haiba ya kiualimu.Kukiri kosa siyo udhaifu,unajirekebisha mambo mengine yanaendelea.Hata walimu wanaofanya kazi kizembe siyo wote ni baadhi tu.
Tatizo siyo dogo baadhi ya walimu hawapo makini.Watoto wangu wawili pia wamepata shida kama hiyo.Vyeti niliwakabidhi, wanavyo na baadhi ya walimu nimeshawahi kufanya nao kazi wananifahamu na watoto pia.Nilipojaribu kufuatilia eti mkuu naye anashangaa.Ila maelezo ambayo Afisa Taaluma alinipa...
Answar mtume wao nani?,kitabu Chao kipi?hawaswali swala Tano?.Hitilafu za maulamaa ni hekma.Tuungane pamoja katika tusiyo pishana.Pia tuwe na viongozi wenye hofu ya Mungu na wenye maono.Huwezi ukamchagua imamu mpiga ramli ukakubali kuswalishwa naye lazima mpotee wote.Tufuate Quran na Hadith...
Na wasiokuwa waislam wanaipenda sana Bakwata.Hata masheikh wengi huingia katika misukosuko kwa kuongea ukweli juu ya Bakwata.Kiukweli hii taasisi inaudumaza uislam nchini kwakuwa Ina mipango duni isiyotekelezeka.
Sidhani kama wewe ni muislamu mwenye uelewa kuhusu BAKWATA.Hii ni taasisi ya kusimamia waislamu siyo dhehebu.Shida viongozi wanaingiza umadhehebu kwenye taasisi inayotakiwa kusimamia waislamu wote kama ilivyokuwa EAMWS.Taasisi ndogo zinafanya vizuri katika nyanja ya maendeleo ya kijamii lakini...
Sheikh Kishk ni Sheikh anayeona mbali.Wangekuwepo mashekh wengine kama yeye Jamii ya kiislam ingebadilika.Tatizo wapi wachache Wa aina yake na hawapewi nafasi kuongoza Jamii ya waislamu Wa Tanzania.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.