Mkuu, ili kuonesha kuwa unajali na ni mkweli ungetuwekea bandiko la hiyo hotuba ya Mhe. waziri, kipengele cha tozo la kila mwezi la sh. 1,000 ambacho Mhe. Zitto anasema kakikuwepo nawe wasema kilikuwepo.
Comments zingine huwa zinachekesha sana. Mkuu, kama hayo uliyoyasema ni ya kweli, inakuwaje serikali yenye vyombo madhubuti vya ulinzi na usalama ya Tz imeshindwa kuwachukulia hatua za kisheria hao wahusika uliowatuhumu kwa uchafu na makosa hayo uliyayataja???!!!!
Mkuu, pamoja na msimamo wako "ulio thabiti" kwa hoja hii, ni ukweli ulio wazi kwa wanaoamini uwepo wa Mungu kwamba yupo upande wao CDM. Hii ni kutokana na kuweza kuruka vihunzi na mikwamo mingi iliyopata kuwekwa juu yao. Kama hayo ni ya kweli kwa nini wasiamini kwamba Mungu yu upande wao?
Mkuu, naomba nikuunge mkono, aidha huyo askofu anataka kuuambia umma wa wa-TZ kwamba huko Israel hakuna watu wanaoishi bila kufunga ndoa? Ninamhurumia kwa kujiingiza katika ushabiki wa kisiasa.
Mkuu, umeeleza mengi kuhalalisha mawazo yako kuhusu kinachosemekana kuwepo kwa kutokuelewana kwa mhe. JMK, Rais wa TZ na Kiongozi wa Rwanda mhe. Kagame.
Binafsi siamini kwamba viongozi hawa wawili hawaelewani, kwa sababu ushauri alioutoa mhe. JMK kuhusu kufanyika kwa mazungumzo ya amani na...
Mkuu, kiingeredha chako kigumu!! hadi nimetoka kapa, ni cha wilaya gani ya TZ. Kwa nini usingeandika lugha ya Kiswahili ukaeleweka vizuri kuliko hicho ulichokiandika, ni aibu, sijui ni cha wapi?
Mkuu, pole sana. Unadhani wewe ndiwe uliye sahihi katika Kiswahili? Hapana. Hilo neno "ndio" katika Kiswahili fasaha hutumika kamaanisha kundi au makundi. Hapa ulitakiwa utumie neno "ndiyo nini"?
Mkuu, mleta mada ameleta kiushabiki. Kwa bahati mbaya sina huo ushabiki wa vyama. Ila nina kumbu kumbu ya rais wa awamu fulani ambaye alipata kukutana na waziri mkuu mstaafu wa Malaysia (Dr.....). Alipomwuliza kuhusu mbinu walizotumia kupata maendeleo ya kiwango kile akamjibu. Ili muendelee...
Mkuu, samahani hicho kiinglishi kimenipita mbali kwa sana, si unazijua Kayumba Skuli?
Lakini ngoja nijaribu kidogo yawezekana Kiswahili hukijui kabisa.
Are you a stranger in Tanzanian politics? Haven't recently ever heard about the release of a draft for the new constitution of Tanzania...
Mkuu, mambo mengine ambayo huwa unayaandika huwa yanajikanganya yenyewe.
Unasema kushabikia kiingereza ni ulimbukeni, mbona nawe umeandika kichwa cha habari cha uzi wako kwa lugha hiyo hiyo ya kilimbukeni (tena kwa makosa)???!!! Lakini maelezo ya ndani kwa Kiswahili, je kulikuwepo na hiyo haja?
Mkuu, ningekuona wewe kuwa ni GT wa JF iwapo uzi wako ungeambatana na mifano halisi ya "wabunge na wagombea urais wa kudumu" wa hicho chama CHADEMA waliopo. Weka mkazo katika "wa kudumu". Hapo ndipo mantiki ilipo.
Mkuu, naomba nikukumbushe kitu. Muungano wa Tanzania unafanana na iliyokuwa Soviet Union (USSR).Kipindi kile Sovereign republics zote zilizokuwa zinaunda Soviet Union zilikuwa na viongozi wa juu na katiba zao isipokuwa Russia. Sababu ilikuwa kwamba Russia ndiye aliyekuwa mhimili ya Soviet Union...
Mkuu, pamoja na ushabiki wa kivyama, ni ukweli usiopingika kuwa, CCM kama chama tawala kimekuwa mstari wa mbele kupinga wagombea binafsi. Rejea kesi ya Mch. Mtikila dhidi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ya TZ, na hukumu yake na nini kilifuatia kuhusu utekelezaji wa hukumu hiyo? Ndiyo maana huyu...
Mkuu, tangu mwanzo wa uzi huu umekuwa ukimshambulia mleta mada. Ni dhahiri kabisa una chuki za kitoto na huyu bwana. Katika kuchangia mada si muhimu kujua nani kaileta, bali inahusu nini. Au ni kanuni ipi ya JF inayosema ili u-post mada ndani yake ni lazima uwe mwandishi wa habari...
Mkuu, hakika ukipenda chongo utaita kengeza!
Kweli kwa profesa wa sayansi ya miamba, ambaye vipimo vya urefu ndiyo lugha yake asijue sentimeta ni kitu gani hadi akichukulie kama kipimo cha ukuaji wa uchumi halafu useme eti ulimi umetereza bila kutilia shaka???!!! Hakika TZ haiishi vituko...
Mkuu, hongera kwa kutujuza na hongera kwa kuandika ukweli kwa kujiamini.
Sasa na sisi tusioelewa ninaomba utusaidie.
Hivi balozi wa TZ, sijui ni nchini au jijini Roma anaitwa Kardinali nani?
Ahsante mkuu kwa kunifumbua macho, nilikuwa sijui kuwa Kiingereza ni lugha mahsusi ya TZ.
Hata hivyo ninakuomba, ili kunipa uelewa zaidi nielekeze ni wapi pameandikwa na kusisitizwa kama ulivyoandika hapo juu kwenye wekundu. Ni katika katiba ya TZ au ni pahala gani? Tafadhali nielimishe.
Ahsante mkuu kwa kunifumbua macho. Nilikuwa sijui kwamba Kiingeeza ni lugha mahsusi ya TZ.
Ili kunifumbua zaidi mkuu, ninaomba unielekeze ni wapi pameandikwa hivyo kama ulivyosema hapo kwenye wekundu? Ni katika katiba ya TZ au wapi?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.