Ni ajabu na kweli kwamba lile jina lililokuwa linawanyima usingizi mashabiki na wapenzi wa Young African sasa limejifia lenyewe by "Natural Death" huku wenzao wakipokea shurba hiyo kwa jina lao la "Makolo" kuibuka na kujipatia umaarufu mkubwa.
Kweli kutesa kwa zamu.
Tafuta hela heshima...
Mwaka 2017 nikiwa chuoni niliamua kuacha kunywa soda na soft drinks zote baada ya kupima sukari na kukuta ikiwa juu kiasi.
Sasa imetimia miaka 4 bila kunywa na nimezoea kabisa. Najihisi kuwa na afya njema sana na wala sitamani zaidi ya kuwaonea huruma wanaotumia. Asante Mungu!
Enzi hizo miaka ya 1993, 1994, 1995 ikifika saa 11 kasoro jioni kale ka mlio ka ndege kanaanza kulia. Ikifuatiwa na muziki mzuri wa reggae hasa Luck Dube. Those days were so beautiful and astonishing.
Mimi namkumbuka sana mtangazaji wa kike nadhani kwa sasa ni marehemu "Jane Zondo"
Nimetumiwa sms na mkuu wa idara ukiagiza kutoa mchango wa Tsh.5000 kwa kila mtumishi kwa ajili ya mwenge. Imenifikirisha sana sijui tunaenda wapi? Huku mchango wa mwenge kule kodi ya kizalendo kwenye miamala ya simu. Ng'ombe anakamuliwa mpaka atoe damu badala ya maziwa.
Natazama mechi ya ligi kuu kati ya Gwambina vs Jk Tanzania. Kwakweli huu uwanja wa Gwambina Complex Pitch imechoka na ni dhahiri uwanja umekosa hadhi ya kutumiwa kwa michezo ya ligi kuu kwa sasa. Pitch ina vinundu vya manyasi na vipara vingi, hali inayosababisha mpira wa chini kushindwa...
Toka sekeseke la kuvurugika kwa mchezo wa watani wa Jadi,Wizara ya michezo imekuwa bubu licha ya TFF kueleza kuwa ilipokea maelekezo ya kubadilisha muda toka Wizarani. Kuna usemi kwamba "If you hide the truth people will create their truth". Sasa kuna uvumi mwingi na kila mtu anaongea lake...
Ni kiu yangu kuona uwanja wa Uhuru ukiwa na taa km ilivyo uwanja wa Mkapa, au Azam Complex.Lengo baadhi ya mechi zinazopangwa kuchezwa pale uhuru saa 8 mchana basi zichezwa usiku. Kucheza mechi kwenye " Artificial Pitch" saa 8 au hata saa 10 jioni ni mateso kwa wachezaji.
Asilani abadani Magufuli asingeweza kuvumilia huu upuuzi uliotokea leo uwanja wa Mkapa. Kesho asubuhi mapemaaa! kuna mtu angetumbuliwa. Huu si uzembe tu bali dharau iliyopindukia kwa familia ya wanamichezo.
Kiungwana tu Waziri wa michezo atoke hadharani kutuomba msamaha. Na namshauri Mh. Rais...
Ukikiongea Kiswahili cha Kenya hadharani ukiwa Tanzania unaweza jikuta umeshushiwa kipigo heavy.
Hii lugha inawapiga chenga sana. Tuendelee kuwasaidia ipo siku wataelewa.
Kuna watu wamechachawa na mechi ijayo ya watani ya tarehe 8 May, presha juu hawalali. Simba na Yanga wamecheza dabi toka miaka ya 30s hadi leo, na wataendelea kukutana miaka mingi ijayo labda hadi mwisho wa dunia.
Ukitaka kufurahia Simba na Yanga usiwe na presha. Kuwa tayari kwa matokeo yoyote...
Unabii ni moja ya huduma 5 za Mungu za kuliongoza kanisa, iliyo muhimu sana kulingana na Biblia. Ukisoma vizuri maandiko utaona kuna tofauti kubwa iliyopo kati ya manabii wa sasa na wale wa zamani. Hizi baadhi ya tofauti:-
1. Nabii wa zamani mara nyingi walitabiri kuhusu mambo makubwa...
Niseme tu kwa mara ya kwanza nimemuona Carlinhos akichezeshwa nafasi sahihi anayoimudu na aliitendea haki haswaa! Nadhani makocha waliopita hawakuliona hilo na hii ndio faida na hasara ya kubadilisha makocha. Kuna wa kunufaika na wa kuumia. Kufa kufaana.
Yanga ina mapungufu mengi lakini kukosa...
Bila kuchelewesha mada zifuatazo ni faida na hasara za kuoa mke kutoka familia yenye uwezo kifedha.
A) faida
1.Kupata zawadi nyingi wakati wa harusi.Mnaweza pewa zawadi ya fedha, vitu vyote vya ndani, nyumba, magari,nk.Kwa hiyo kiuchumi inalipa.
2.Kiasi fulani inaweza kukupa heshima mtaani...
Nyanya ni zao ambalo hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu msimu wa mvua nyingi na msimu wa baridi kali. Hali hiyo husababisha bei ya nyanya kupanda sana kipindi hicho na wale wanaobahatika kuwa na nyanya vipindi hivyo huuza kwa bei nzuri.
Naomba kujua ni aina gani ya nyanya inayofanya vizuri...
Msimu huu pekee Yanga wamebadilisha makocha zaidi ya 3 lakini timu bado haina matokeo mazuri.Kitendo cha kubadili badili makocha ni dalili tosha kuwa timu ina matatizo ndani ya uwanja.Nimekuwa nikiifuatilia Yanga inapocheza kwa makini sana. Yanga wanatatizo kila idara,na sina hakika km wanajua...
Ukitazama mpaka wa Tanzania na Kenya ni dhahiri Kenya wana haki ya kutetea eneo la bahari ambalo Somalia wanadai kuwa ni lao. Kama madai ya Somalia ni halali basi hata Kenya wangeweza kuibuka na madai kama hayo dhidi ya Tanzania. Madai kama haya nayafananisha na yale ya Malawi dhidi ya Tanzania...
Nakumbuka wakati Kaze anatajwa kutakiwa na Yanga, kuna mwandishi mmoja wa Burudani/ Rwanda Kama sikosei alisema Kaze hana uwezo wa kufundisha timu kubwa kama Yanga. Akatoa sababu kadhaa ikiwepo ya kukosa uzoefu wa kutofundisha timu kubwa na zenye presha.
Leo nimeamini hiyo kauli na nakiri...
Kuna watu wanaishi kwa kuamini kila taarifa.Kwa ujumla ulimwengu wa leo unaendeshwa na habari za uzushi na uongo.Unaposikia au kuambiwa jambo lolote lazima ulichekeche. Ndio maana tukaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Kuhusu chanjo ya Covid-19, kuna watu tena viongozi wakubwa wa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.