Wakuu mimi sina mambo mengi sana hapa najaribu kufikiria, hivi Mh. Shabiby aliwaza kweli kuwa kuna watu ambao wao wanakatwa bima moja kwa moja kwenye mishahara yao?
Hawa wataondolewaje kwenye huo mfumo aliopendekeza sababu na wao ni wamiliki wa simu watakaokatwa bima mara mbili.
Labda...
Salamu Wakuu,
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza. Binafsi nadhani serikali au viongozi husika wameshindwa kabisa kujua ni namna gani mechi za week end hii za Yanga na Simba zitusaidie kiuchumi kama taifa.
Nimesikia baadhi ya viongozi na wadau wa michezo wakiongelea uzalendo na kutaka watu...
Salamu waungwana.
Nisiwe na maneno mengi mimi nina swali hili kwa wataalamu wa afya na wizara ya afya kwa ujumla.
Je, mtindo wa watu kuoga maji baridi ili kupooza joto la miili yao ni salama kwa afya?
Kama sio salama kwanini wizara na wataalamu wa afya hamlizungumzii hili suala hata kutoa...
Hapa nimeshangazwa na ujasiri wa Dj aliye zamu leo RFA maana anapiga nyimbo za mixtape za Anti Virus live live ni matusi matusi tu.
Kama hamtaamka na barua ya TCRA asubuhi Mungu yupo nanyi.
Nimekumbuka ile barua ya onyo waliyopewa miaka mingi nyuma kisa kupiga nyimbo ya Kaka Suma by Nash MC...
Habari Wakuu,
Kama mada hapo juu inavyosema.
Mhusika ambaye ni Mzee MICHAEL ELICHILIA UISO nasema mzee sababu kwa makadirio kwa sasa atakuwa na miaka isiyopungua 72
HISTORIA FUPI NIIJUAYO
Mzee MICHAEL ELICHILIA UISO alisoma nchini Urusi masuala ya kilimo, na baadae aliporudi nchini Tanzania...
Habari wana JF
Nianze kwa ufafanuzi mfupi wenye maslahi kwa watu wengi.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mwanasheria na Wakili. Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Mwanasheria ni mtu mwenye digrii ya sheria. Hivyo mtu mwenye diploma ya sheria au elimu chini ya hapo sio Mwanasheria, bali ni...
Salamu wana JF,
Katika kuweka mizani ya utawala na utendaji wa haki nchini sawa tumeona Rais akiunda na kuituma kazi Tume ya kupitia utendaji wa taasisi za haki jinai, hili ni jambo zuti hasa tukiangalia Tume hii imeundwa kwa wingi na watu waliofanyakazi katika mfumo wa haki jinai, ingawa wapo...
Habari wana JF
Leo naomba nigusie maswala machache yanayohusu sheria na utendaji wa makampuni binafsi.
Naamini umewahi kusikia juu ya wito wa kurasimisha biashara na makampuni. Wapo viongozi wa kiserikali na hata binafsi wamekuwa wakihamasisha wafanyabiashara kurasimisha mifumo yao ya biashara...
Habari wana JF
Leo naomba kuongelea au kuliwekea ufafanuzi jambo moja ambalo limekuwa likielezwa vibaya au kimakosa na watu wengi wengine wakiwa ni viongozi hadi wa kiserikali.
Suala hilo ni swala la je, ni ndoa kiserikali baada ya kuishi na mwanamke au mwanaume nyumba moja kama wapenzi?
Hili...
Habari wana JF.
Huu mwaka nimedhamiria angalau kwa kila wiki niwe naweka uzi mmoja unaohusu swala la kisheria.
Nimeamua hivyo baada ya kuona changamoto nyingi sana za kisheria zinazoikumba jamii yetu, sio rahisi kufikia kila mtu lakini bora kidogo kuliko kukosa kabisa, basi nitatumia zaidi JF...
Habari Wakuu.
Leo nimesikia habari au niseme tangazo la Mkuu wa wilaya ya Kahama kuwataka vijana kuanzia miaka 14 wasio na ajira/kazi maalumu yakufanya wahame wilaya hiyo.
Hili binafsi limenishtua sana na kujaribu kujiuliza maswali tofauti tofauti;
1. Huu umri wa miaka 14 alikosea au...
Wakuu!,
Mimi sina mambo mengi yakuongea hapa sababu hili jambo nimeliwaza tu kwa juu juu wahusika wanaweza kulifanyia kazi kwa undani zaidi.
Ni kwamba binafsi naona kwamba vishikwambi 'tablets' zilizotolewa kwa ajili ya zoezi la Sensa, hili zoezi likikamilika serikali ipeleke vishkwambi.hivyo...
Waungwana salamu [emoji1538]
Nisipoteze muda mwingi niende moja kwa moja kwenye mada.
Kujiuzuru uspika kwa Mhe. Ndugai kumezidi kuonesha ni kwa namna gani kama Taifa bado hatufahamu mambo mengi ya kisiasa, kiutawala, uraia na kiutendaji.
Wapo waliombeza Mhe. Ndugai wapo walioshitushwa na wapo...
Habari wana bodi
Mimi sina mambo mengi sana ya kuongelea kwenye hii mada zaidi kichwa cha habari kizingatiwe na wahusika ambao kama sikosei ni kitengo cha Elimu ya afya kwa umma.
Hapa pia niwajumuishe na wizara ya habari kwakuwa matangazo haya mengi yanarushwa na vyombo vya habari. nimekuwa...
Wakuu moja kwa moja kwenye hoja.
Kwa muda sasa Baraza la Samaa Tanzania limekuwa likifungia nyimbo za wasanii lakini kwa kiasi kikubwa zikiwa ni za wasanii wanaoiponda serikali au viongozi wake.
Zipo nyimbo nyingi za hovyo ambazo sio tu kutofungiwa bali zinapigwa kwenye vituo vya habara redio...
Habari Wakuu,
Leo nimeona niandike uzi kuhusu hili swala la kujifunza. Tumekuwa tukisikia malalamiko kwa muda mrefu sasa takribani miaka 20-15 juu ya elimu yetu na wasomi tunaozalisha.
Malalamiko yameongezeka zaidi miaka ya hivi karibuni kuwa huko mashuleni, vyuoni na vyuo vikuu tunazalisha...
Habarini wana Jf, [emoji1538]
Kuna kipindi niliwahi kusema hapa JamiiForums kuwa ushoga upo zaidi mikoani kuliko hata jijini Dar es Salaam. Wapo waliokataa wapo waliouliza na baadhi wachache walikubaliana nami.
Ikumbukwe, nilieleza ni kwanini tabia hii ina wahanga wengi mikoani kuliko hata...
Habari wandugu [emoji1538]
Nitaenda moja kwa moja kwenye maelezo yangu kidogo sababu hili ni swali wenye majibu watujuze au wachangiaji wengine wachangie zaidi.
Kumekuwa na utaratibu ambao sasa umeonekana kuwa kawaida au mazoea kuwachukua wanyama pori Faru na kuwaweka sijui niite kwenye...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.