Pascal Mayalla,
Uwezo wako wa kuchambua mambo na kujenga hoja umefikia kikomo. Nafikiri umri umeanza kukuathiri au utakuwa na tatizo lolote la kisaikosojia.
Kila kitu kinachofanywa na hata halmashauri lazima kusifia Magufuli. Hivi ni vitu vidogo sana vya kumhusisha Raisi wa nchi. Upumbavu wa kusifia umezidi sana kiasi kwamba mchango na ubunifu wa taasisi mbalimbali hauthaminiki na kuonekana.
nzagambadume,
Uko kwenye vita ya uchumi ukipigana na mataifa yapi? Hayo mambo unayoyaona ya barabara mbovu yamesabibishwa na wizi wa hao viongozi wa CCM. Tangu uhuru nchi iko mikononi mwa CCM na leo unadanganywa kwamba nchi yetu imeibiwa na wageni. Jaribu basi kutumia akili yako ya kuzaliwa...
Rais anaposema nchi yetu imeibiwa sana, nani wezi wa raslimali zetu kama siyo CCM? Tangu uhuru CCM ndiyo imekuwa madarakani na yeye mwenyewe amekuwa kiongozi katika kundi la wezi ambazo ni CCM. Umaskini wa Tanzania hauwezi kutenganishwa na CCM.
Kati ya upinzani na hao wazee nani amepoteza? Lowasa kapoteza sana vitu vingi ikiwemo heshima katika jamii na nguvu ndani na nje ya chama vimeyeyuka kabisa. Sumaye naye vile vile.
Ni upuuzi huo, tunashundwa kujenga vyoo kwa fedha zetu, lakini fedha za kuharibu kwa kuitisha chaguzi kwa watu waliokuwa wanahama vyama zipo. Nafikiri nchi ina viongozi wa ovyo wenye akili za matope.
Jamani CCM tuweni wa kweli, hayo majengo ya ofisi kwenye pichw hata chama chetu tunayo huko vijijini. Najua wengi mmezaliwa na kukulia mjini, hali halisi ya mazingira na makazi ya vijijini hamuifahamu vizuri.
Ni kiongozi kijana kuwahi kuwa mkuu wa serikali katika bara la Afrika lakini mambo aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya ni makubwa kwa nchi yake na majirani. Ni mwaka jana tu amekuwa Waziri Mkuu lakini mwaka huu amekuwa mshindi wa Noble Prize!! Ni kiongozi kijana mnyenyekevu na anayethamini...
Unaongea hayo kwa sababu ya amani tuliyonayo. Usilinganishe Tanzania na hayo mataifa. Misri, Sudan, Libya, jirani zetu DRC Congo na Burundi, Afrika ya Kati, unajua kilichopo. Kama huwezi kujifunza kutoka nchi hizi basi utakuwa na tatizo. Pole sana
Mtu anayejiita "mkulima" (aka kamishna wa TRA aliyetumbuliwa) ni sumu hatari na msaliti wa amani ya nchi. Siyo siri, lakini moja ya mambo ambayo yameleta utulivu na amani katika nchi yetu ni suala la kupeana kijiti cha uongozi. Nchi nyingi zenye machafuko, mapinduzi ya kijeshi duniani ni zile...
Chama tawala nacho ni mwenyekiti, ukikosana naye utapata tabu sana kwenye maisha yako ya kisiasa kama wewe ni mwanasiasa. Chama tawala ingekuwa taasisi imara sana kama wangetenganisha nafasi ya mwenyekiti na urais.
Kuna una QUOTE="ngwanduu, post: 32531032, member: 508036"]
Rais Magufuli ni mzalendo namba mija Tanzania ,Tunaona jinsi anavyohangaika kuipigania nchi yake kwa ajili ya Watanzania Tunashughudia na tunajioneo mengi unayoyafanya ni mambo makubwa sana ambayo yanahitaji ujari mkubwa sana.
Kipindi...
Membe siku zote amekuwa kimya na wala hajawahi kufanya mambo kama ya Lowassa.Kila neno analoongea mnatoa tafsiri ya kupiga kampeni. Hata miondoko yake, mnasema anatembea kama mtu anayetaka urais!! Yawezekana hata urais wenyewe hautaki.
Yaani wewe unaona suala la ndege ndilo la kitaifa zaidi? Watu walibomolewa nyumba kimara, Akwilina aliuwawa, Azory alipotea na Lissu kupigwa risasi eneo la bunge. Haya yote watawala wetu na watu wnegine hawakuyaona ya kitaifa. Leo ndiyo mnataka suala la kushikiliwa ndege tuungane kitaifa...
Hii ripoti ni muhimu sana. Lakini ukiangalia kwa undani kuna mambo kadhaa ambayo, nafikiri kwa makusudi NBS wameamua kuyaficha. Katika kipengele namba 5 kinachohusu elimu, kuna vitu wanaficha sijui wanamfichia nani? Kwa mfano, kwa upande wa elimu ya msingi na sekondari kidato cha 1 hadi 4, na 5...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.