Search results

  1. Baraka Sabi

    Hongera! Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa); Umekuwa Kielelezo cha Kuigwa

    Ulipopendekezwa kuwa Waziri Mkuu, Watanzania walio wengi hawakutegemea. Isitoshe siku Mh. Rais analitaja jina lako Bungeni, hata wewe hukutarajia. Ulighubikwa kwa chozi la furaha huku moyoni ukitafakari utaitendea nini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nafasi uliyoaminiwa. Nikupongeze kwa...
  2. Baraka Sabi

    Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu October 2020, Mungu atuongoze kuwapata Wawakilishi wenye moyo

    Ni kawaida mtu anayeomba kuwa Mwakilishi wa watu hutumia lugha ya ushawishi kwa lengo la kutafuta imani toka kwa watu anaotaka kuwaongoza. Huu ndio uhalisia kwa mujibu wa sheria na taratibu zetu za nchi. Cha kushangaza, wagombea walio wengi wamekuwa wakiwashawishi wapiga kura wao kuamini hata...
  3. Baraka Sabi

    Maisha Bora kwa kila Mtanzania: Je, Mfumo wa Elimu una Mchango gani?

    Elimu ni ujuzi, maarifa na stadi azipatazo mtu katika mazingira yanayomzunguka ama maisha yake ya kila siku, zinazomwezesha kufanikisha kwa ufanisi na weledi utekelezaji wa majukumu yake kwa faida yake mwenyewe na jamii kwa ujumla. Chimbuko la mfumo wetu wa Elimu ni kipindi cha mkoloni...
  4. Baraka Sabi

    Mnaohamahama vyama vya siasa: Je mnajua dhambi mnayoitenda na madhara yake?

    Kuwa mfuasi wa chama fulani ni uamuzi aufikiao mtu baada ya tafakuri ya kina na upembuzi yakinifu juu ya faida na hasara atakazozipata ama kukabiliana nazo. Yumkini, mfuasi huwa ni mtu aliye tayari kupambana na kukabiliana na changamoto zozote zile zinazoweza kujiitokeza dhidi ya maamuzi yake...
  5. Baraka Sabi

    COVID19 na safari ya wana wa Israel

    Ni wazi dunia nzima inazizima kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona (COVID -19) tangu kubainika kwake hapo disemba 2019. Ni gonjwa ambalo mpaka sasa limegharimu maisha ya maelfu ya wanadamu huku likiacha athari za kijamii na kiuchumi zisizoweza kuzibika hata kidogo miongoni mwa wanajamii...
Back
Top Bottom