Search results

  1. Sakasaka Mao

    Mtanzania mwenye Umri wa miaka 60 akamatwa na Mihadarati Ethiopia

    Aina ya usafiri aliouchagua na muonekano nyoronyoro wa punda ndiyo sababu ya kuhisiwa na kudakwa mapema.
  2. Sakasaka Mao

    Serikali tunaomba ufafanuzi wa milipuko ya kila siku katika Milima ya Uluguru

    Mzee tangia dunia iumbwe, labda mripuko wa volcano, lakini mlima kuporomokea mji na kuufukia usichukulie poa namna hiyo. Hata kama ni mabomu yatarindima yataishia kuubaraza tu mlima kama huo lakini hayawezi kuuporomoa.
  3. Sakasaka Mao

    Nilitembea Baba Mkwe, halafu mtoto wake ndio anataka kunioa nifanyaje?

    Mkuu siishi kwenye chungu, ninaishi tu mitaani. Kusikia 'mtaani wapo kibao', unamaanisha jambo hili lipo sana katika jamii yetu, yaani: mwanamke mmoja kuweza kufanya mapenzi ama kuolewa na ndugu wawili wa damu, aidha mtoto na babake au mtu na kaka yake kwa kujua na maisha yakaendelea...
  4. Sakasaka Mao

    Mwenezi CCM Arusha: Kama huna Kadi ya CCM umemsaliti Mungu

    Hapo tumekwenda pamoja.
  5. Sakasaka Mao

    Mwenezi CCM Arusha: Kama huna Kadi ya CCM umemsaliti Mungu

    Anza kwanza uchambuzi wa maoni yako mtoa mada. Kutuacha tujadili wanajamvi halafu wewe upo pembeni unatuzoom ni sawa na kutupia mbwa marapu rapu kisha ukajiweka pembeni kufurahia wanavyoyafakamia.
  6. Sakasaka Mao

    Ukiwa mkweli kabisa kutoka moyoni, How are you? Unaendeleje na hali?

    Ukweli kabisa kutoka moyoni utauexpose kwa mtu tu barabarani asiye mwandani wako? Tangu dunia ianze kustaarabika haijatokea hivyo hata kwa wahenga. Utamaduni wa salamu ni mfumo uliowekwa wa kiubinadamu kuonesha upendo na nidhamu, lakini si kwa malengo ya kuelezeana madhila na madhaifu pamoja...
  7. Sakasaka Mao

    Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

    Mkuu unaamini kabisa kuwa binadamu hana chanzo(mwanzo)? Hii mijadala ya kuumiza ubongo tuwe tunakuja na mpangilio wa rejea pamoja na evidence zake. Vinginevyo tukubali kutokukubaliana.
  8. Sakasaka Mao

    RC Makonda atinga Makao makuu ya CCM Dodoma Kuhojiwa

    Haka kamsemo kananifurahishaga sana. 😎🤓😜😣🤗
  9. Sakasaka Mao

    Dr Kigwangala: Watanzania wataichagua tena CCM kwa Sababu imemaliza Tatizo lao la Maji, Katiba Mpya siyo Kipaumbele chao!

    Kuna umasikini mkubwa, bora angelikuwa kaleta maendeleo sasa! Nzega vijijini ni jimbo la mwisho Tz kwa kuunganishiwa miundo mbinu ya maji na umeme. Tunavyoongea, vibomba na nguzo za umeme ndo wanaanza kutandika. Kwenye jimbo lake wananchi hawataki kusikia hizo taka taka zake za kilaghai...
  10. Sakasaka Mao

    Ewe Muajiriwa: Mara paap umesitishiwa ajira yako, utafanyaje?

    Distinguish hiyo kazi ni nini na ajira ni nini ili watu wakuelewe.
  11. Sakasaka Mao

    Nilitembea Baba Mkwe, halafu mtoto wake ndio anataka kunioa nifanyaje?

    Kuna furaha inayoletwa na jambo la aibu?
  12. Sakasaka Mao

    Nilitembea Baba Mkwe, halafu mtoto wake ndio anataka kunioa nifanyaje?

    Hiyo nadhani inatumika kudistinguish maneno ili msomaji aielewe taarifa kwa usahihi. Kama ni hivyo, habari hii yote haiwezi kusimuliwa kutokana na wahusika wote kukosa sifa za viwakilishi. Mfano: mchumba-siyo mchumba kwa sababu bado hawajafika nyumbani na kutambulishana na kisha kutolewa...
  13. Sakasaka Mao

    Nilitembea Baba Mkwe, halafu mtoto wake ndio anataka kunioa nifanyaje?

    Kiuhalisia hii habari siyo halisi kwa vigezo vifuatavyo: Kutembea na huyo mzee na kisha kuchumbiwa na kijana bila kujua siyo kosa. Binti kwenda kutambulishwa kwa wazazi na kukuta hawara yake ndiye mkwe, jambo hilo na uchumba huo ungeliishia hapo hapo na thread hii ingeliletwa kwa kichwa cha...
  14. Sakasaka Mao

    Waziri Hamza: Serikali Ijenge Daraja Kuunganisha Dar-Zanzibar

    Fikra ni kula tu basi! Kikitaka kufanyika hiki kwa ajili ya maendeleo pamoja na kesho ya vizazi vijavyo, utasikia hoja za kula kula zinaanza! WaTz tumegawanyika kimaoni pakubwa sana na ndiyo maana tunatawalika kwa sahani za wali na tisheti.
  15. Sakasaka Mao

    Naishi na Mwanamke Nisiemfahamu, Nahitaji Namna Nzuri ya Kumuacha

    Kabla ya kukueleza cha kukusaidia, tueleze kwanza, katika hayo maisha yenu ya siku mbili tatu umempenda pigo zake? Namaanisha namna ambayo wewe unataka mwanamke awe(nje ndani). Ukileta hilo jibu, mengine yote ni mepesi namna ya kuyaweka sawa na kusaidiana.
  16. Sakasaka Mao

    Wairan 8000 ni Wayahudi

    Picha hiyo ni ya panya, ndezi hana mkia.
  17. Sakasaka Mao

    Wairan 8000 ni Wayahudi

    Swali ulilouliza ni la utata mno kwa watu wengi kiuhalisia. Tofauti na dini na madhehebu mengi yalivyo. Uyahudi unaenda na vyote ulivyouliza na kuvitolea majibu: dini, kabila na tamaduni. ie: kuna wayahudi wa dini lakini rangi, tamaduni na mataifa tofauti. Kuna wayahudi wa rangi na taifa...
  18. Sakasaka Mao

    Wosia wa Gardner lazima uheshimiwe, wimbo wake wa "Do you want a beer" lazima upigwe msibani

    Mnakoelekea mtagombana! Ushaona wapi mafahari wawili wakashea bando halafu ikabakia kuwa 'pisi'?
  19. Sakasaka Mao

    Mkuu wa Mkoa Arusha Paul Makonda: Kiongozi Mzima Kujieleza Hujui, Mnapataje Hizi Nafasi TARURA?

    Nimesikiliza, kwa kweli hajui kujieleza. Si yeye peke yake aliyeshindwa, bali ni viongozi wengi waliosimama kutaka kuokoa jahazi wameshindwa kutafsiri maana na kazi halisi za Tarula ni nini!
  20. Sakasaka Mao

    Mkuu wa Mkoa Arusha Paul Makonda: Kiongozi Mzima Kujieleza Hujui, Mnapataje Hizi Nafasi TARURA?

    Mi sijawahi kufoji mkuu. Ila ninafahamu kinagaubaga ghushi zilianza mwaka '74, sera ya elimu ya msingi ilipobadilika kupiga marufuku watoto wasirudie wanapofeli darasa la saba.
Back
Top Bottom