Habari za asubuhi. Pole Sana kwa kadhia hii. Umeziona mara nyingi je ngapi umetuletea tufanye review ndugu yangu? Tumetangaza call center yetu hadi namba zangu binafsi unatuma ujumbe. Hebu Leo lete sasa tufanye review tuone nani huyo anakiuka huduma kwa usawa. Shukrani
Wasaalam Wana Jukwaa wote.
Tunaelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia hapo Mei 15, 2024 ambapo, nchi yetu tutaungana na zingine duniani kuadhimisha.
Familia ni chanzo cha jamii yetu hivyo, ni kiungo muhimu sana kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Malezi bora kwa watoto ndani ya...
Utaratibu wa kuasili watoto mapacha unafana na watoto wengine. Kanuni ya kuasili 3(e) hairuhusiwi kuwatenganisha watoto ndugu.
Kuhusu vigezo vikuu; vigezo vyote kuasili ni vikuu kwa ulinzi na usalama wa mtoto na ni njia mojawapo ya kujiridhisha kwamba mtu ametimiza vigezo
Umri wa kuasili...
Ndiyo Sasa nimepata fursa ngoja niyakusanye sasa hivi nimpe kamishna wa ustawi anipe majibu nirudi hapa sasa nikupe. Mambo mengi ndugu zangu, kuna wakati napotea kuendelea na mengine narejea tena. Subiri tafadhali, shukrani
Naomba niyachukue maswali yenu yote kesho Kamishna wa Ustawi ayajibu vizuri kisha nitapandisha hapa majibu yote. Wengine nao waulize tu. Ahsanteni Sana kwa mwitikio wenu🤝
Ahsante Sana kwa maoni. Kwa kuwa huduma hiyo Iko wizara ya afya, tutaratibu kikao cha mashirikiano kuwasilisha maoni haya. Naomba tu muwe critical, Changomoto Iko eneo gani la huduma hiyo tafadhali
Wakati ule ikitungwa sheria iliyopo ilikuwa hivyo, ila sheria zote hubadilika kwa nyakati kulingana na maoni ya watumiaji wa sheria na taarifa za kitafiti na uzoefu mbalimbali. Hivyo, tunapokea maoni. Shukrani
Muda ni Mwalimu mwema kwa Kila swali. Tuzidi kupambanua kile Mungu ameweka ndani yetu, muda wetu ni mfupi na unapita kasi, saa inakuja ya kuuona uso wake na kupimwa kwa mizani yake. Nakutakia Heri na Baraka za Mungu. 🤝
Kifupi alidanganywa, angeibiwa, huo ni utapeli na ula rushwa. Hakuna malipo. Kama Yuko tayari anitumie ujumbe tuchunguze Ili aliyeomba hizo hela achukuliwe hatua. Hapa nahitaji ushirikiano wako tafadhali.
Ahsante Sana kufuatilia mjadala huu na kuchangia. Tumetoa namba hizo za call center za wizara Ili kama ikitokea tumechelewa kuona hapa basi fuatilieni kwenye namba hizo.
Ufafanuzi kwa ufupi;
1. Sheria imeruhusu kuasili mtoto wa umri wowote ila limitation ya umri imewekwa kwa waombaji/adoptive...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.