Search results

  1. Msambichaka Mkinga

    Askofu Mwamakula: DP World kujenga msikiti wa Masjid al jumaa wa Mbeya na kuendelea kusaidia dini ya kiislam nchini Tanzania!

    Kama ni kweli DP World wamesema kuwa sehemu ya faida watakayoipata kwenye bandari za Tanzania itatumika kujenga misikiti na kueneza uislam, basi hiyo kampuni itakuwa na watu wengi wajinga sana. Kama una akili huwezi kufanya kosa kama hilo. DP kama kampuni ina uwezo wa kusaidia taasisi yoyote...
  2. Msambichaka Mkinga

    Tundu Lissu apuuza wito wa DCI Kingai, asema hatoenda ofisini kwake

    Polisi kama wanamwita mtu kwenda kumhoji basi ni vema wakamweleza wanayeenda kumhoji, watamhoji kitu gani ili anayeenda kuhojiwa aweze kujiandaa kwa kile anachoenda kuhojiwa, ikibidi aende hata na vielelezo. Hatutakiwi kuishi kwa kuviziana bali kwa kutendeana haki.
  3. Msambichaka Mkinga

    Rais Samia: Lazima tuwafundishe Watoto wetu kuhusu uzazi wa mpangilio

    China na India wako mbali wapi, wakati ndio watu wanaoongoza kwa kutangatanga Duniani?
  4. Msambichaka Mkinga

    Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

    Ruzuku ni kutokana na kura za Urais.
  5. Msambichaka Mkinga

    Uongozi wa Rais Samia Usitiwe Najisi

    Kwa hakika, na bila mashaka, uongozi wa Rais Samia umeonesha ushupavu. Wakati viongozi waoga huwaogopa wapinzani wao wa kisiasa, Rais Samia, bila woga, anawaweka karibu. Tangu mfumo wa vyama vingi uanze, ni Rais Kikwete ndiye aliyekuwa anashikilia rekodi ya kukutana na viongozi wa vyama vya...
  6. Msambichaka Mkinga

    Mabadiliko Makubwa yanahitajika. Rais Samia 2025 apitishwe ili Kusimamia Mabadiliko

    Hakuna shaka hata kidogo kuwa Taifa letu hili linahitaji mabadiliko makubwa ya kutengeneza mifumo itakayoishi na kudumu, kwa kuanzia na katiba mpya. Kwa Katiba yetu ya sasa, mtu mmoja aitwaye Rais, kwa madaraka makubwa kupindukia aliyopewa na katiba, asipotaka, hakuna kinachoweza kufanyika...
  7. Msambichaka Mkinga

    Serikalini tuna Wachumi wasiojua Uchumi?

    Na hapo ndipo panapoleta ulazima wa ujenzi wa mifumo imara ya kuibana Serikali na watendaji wake waweze kutenda kwa namna ile iliyo sahihi kupitia katiba mpya iliyo bora. Kwa Tanzania, na nchi nyingi za Afrika, ni muhimu sana kuwa na Katiba imara, zinazoheshimika na sheria ambazo haziwapi uhuru...
  8. Msambichaka Mkinga

    Mnaodhani ni rahisi kumchukulia hatua Jaji Biswalo Mganga njooni mtueleze njia na namna ya kufanya hivyo

    Mbona taratibu zipo wazi? Hakuna ugumu wowote. Kamati iliyoundwa, ikija na uthibitisho kuwa Jaji mwenendo wake haumpi sifa ya kuendelea kuwa jaji, taarifa ya kamati ya uchunguzi itapelekwa kwa Jaji Mkuu. Jaji Mkuu ataunda kamati ya majaji ambayo nayo itafanya uchunguzi wake. Ikijiridhisha kuwa...
  9. Msambichaka Mkinga

    Serikalini tuna Wachumi wasiojua Uchumi?

    Kwa namna tunavyoenda, hakika nchi hii tutaendelea kunung'unika na kulaumiana milele na kuwataja wenzetu wa mahali pengine Duniani wanavyosonga mbele. Sababu mojawapo kubwa ni kwamba hatutaki kuishi kwa kufuata kanuni za maendeleo ya uchumi. Ukitaka uchumi wa nchi au hata wa kwako binafsi...
  10. Msambichaka Mkinga

    Fatma Karume na Membe Hamuitendei Haki Jamii

    Awamu ya tano, kwa wote wenye akili ilikuwa shule tosha. Mafunzo yanaweza kufafanuliwa hata katika vitabu vitano, vyenye vicha vya habari mbalimbali: 1) Neno la manabii latimia, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. 2)...
  11. Msambichaka Mkinga

    Hebu tujiulize undani wa hili ‘Tishio la UGAIDI’

    Hustahili hata kufanya ulinganifu. Italinganishaje kichuguu cha shambani kwao na Mount Everest. Linganisha mlima na milima, vichuguu navyo vilinganishwe na vichuguu vingine.
  12. Msambichaka Mkinga

    Baada ya kuruhusu mikutano ya kisiasa, Rais Samia afute Sheria zote, zilizopitishwa katika utawala wa awamu ya 5, zilizotaka kuiua Demokrasia yetu

    Upo sahihi kabisa. Sheria zile zilizolenga kuimarisha udikteta na kuua demokrasia, kuua uhuru wa maoni, zifutwe/zifanyiwe marekebisho. Sheria hizo ni pamoja na: 1) Sheria ya mitandao na vyombo vya habari 2) Sheria ya takwimu 3) Sheria ya vyama vya siasa 4) Sheria ya kinga ya viongozi...
  13. Msambichaka Mkinga

    Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

    Panua uelewa wako. Uliwahi kumsikia Mbowe anataka kufanya mkutano Dar kama mbunge wa Hai? Una uhakika Mbowe kama mbunge hakuwa anafanya mikutano kwenye eneo la jimbo lake? Jambo la muhimu ni Katiba na Sheria. Aliyezuia mikutano ya vyama vya siasa alikiuka katiba hakukiuka? Aliyezuia mikutano...
  14. Msambichaka Mkinga

    Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

    Ndugu yangu, nadhani kuna kitu hakipo sawa upande wako. Ina maana huelewi kama Mh. Mbowe ni kiongozi mkuu wa kitaifa wa CHADEMA, na eneo lake la kazi ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Uliskia alitaka kufanya mkutano Dar kama mbunge wa Hai? Panua uelewa wako.
  15. Msambichaka Mkinga

    Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

    Ukisema siasa zikome inamaanisha na wanasiasa wakome. Rais mwenyewe ni kiongozi wa kisiasa. Shughuli za siasa haimaanishi mikutano pekee yake. Chama kilichopo madarakani kitawezaje kuipima Serikali yake inavyofanya kazi kama shughuli za kisiasa zikisimama? Vyama vya siasa vitawezaje kuikosoa...
  16. Msambichaka Mkinga

    Huwa najiuliza kwanini Nyerere na Mkapa walikataa kuitwa " Dokta" japo walitunukiwa PhD za heshima!

    Wazungu, nimefanya nao kazi kwa muda mrefu, hata baadhi ya watu wa West Africa, huwezi kujua kuwa ana PhD mpaka ukaangalie CV/profile yake. Huku kwetu, nadhani ni ile athari inayoelezewa kwa kifupi na ule msemo maarufu wa Kiswahili unaosema, Maskini akipata, ....... hulia mbwata.
  17. Msambichaka Mkinga

    Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

    Katiba inasemaje? Mbowe alitaka kufanya mikutano Dar kama mbunge wa Hai au kama kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA? Vyama vya siasa vimepewa haki ya kufanya mikutano wakati wote, nchi nzima kutegemea mahitaji ya chama. Kama chama cha siasa hakiwezi kufanya mikutano wakati wote isipokuwa tu mwezi...
  18. Msambichaka Mkinga

    Mbunge Abood atunukiwa Shahada ya Udaktari (PhD)

    Kwa sasa kuna njia kama 3 hivi za kuitwa msomi. Moja ni kukaa darasani miaka mingi, ya pili kutumia muda mwingi kutafuta pesa kwa njia ya biashara au siasa. Ya tatu ni kwa kupitia uongozi uliotukuka au ugunduzi wa kiasayansi wenye faida kwa jamii. Hii ya kwanza na ya tatu, ndizo zilizozoeleka...
  19. Msambichaka Mkinga

    Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

    Msiwadanganye watu. Ruto hajapiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa bali anawashawishi watu wasihudhurie mikutano ya siasa kwa sababu, kwa maoni yake, haina maana kwa sasa. Kama mwanasiasa, ni sahihi kufanya hivyo. Kazi ya vyama vyama vya siasa na wanasiasa ni kushawishi, mamlaka yao yaishie...
  20. Msambichaka Mkinga

    Kama Lissu anapinga serikali isiweke Kodi yoyote ile kwa wananchi, yeye atatoa hela mfukoni kuendesha nchi?

    Nadhani umepotosha kusema kodi zote. Aliongelea tozo. Lakini kiuhalisia kodi ndogo, huchochea uwekezaji na faida, faida huchochea ongezeko la mtaji, ongezeko la mtaji huchochea upanuzi wa uwekezaji, upanuzi wa uwekezaji, huongeza ajira na vyanzo vya kodi, kuongezeka kwa vyanzo vya kodi na idadi...
Back
Top Bottom