Ni uungwana kukiri hadharani. Nimefuatilia mazungumzo husika club house - kweli Lissu ana kipawa cha kipekee sana kuelezea issues na kukumbuka issues. Kukiwa na Presidential Debate na candidate yeyote ataupiga mwingi sana.
Kwa kauli yake mwenyewe - kumbe swala la kustahafu ubunge 2025 lilishapangwa kabla na mikakati ya hatua inayo fuatia ilishapangwa pia. Mdogo mdogo mambo yanaanza kuwa hadharani juu ya taharuki iliyoibuka chamani mpaka kupelekea jamaa kuachia ngazi kwa kasi ya 5G na vijembe vya chifu Hangaya...
Ewe mkatoliki, Kanisa Katoliki halina MISA YA IJUMAA KUU!!! Baada ya Ibada ya Misa ya Alhamisi Kuu jioni kanisa katoliki haliadhimishi tena MISA yoyote mpaka MISA YA MKESHA WA PASAKA Jumamosi Kuu usiku
It is true, Makonda is still very young! BUT your hypothesis could hold water if there were no criminal offences involved. Jinai haifi wala haizeeki. Ukiingia uongozi wowote wenye kuheshimu utawala wa sheria na kuziruhusu mahakama kutimiza majukumu yake kwa uhuru kamili, hatakwepa mkono wa sheria.
Mazingira ya Lissu kuibiwa Passport yanaweza kweli kuwa tata, ila swala la yeye kuomba Rais asaidie yeye kupata Passport nyingine nalitazama kwa kuzingatia mazingira aliyo ondokea Lissu baada ya uchaguzi 2020. Passport ilipatikana kwa kuwa fasttracked na wale Mabalozi waliokuwa wamempa hifadhi...
Kwa hili napingana na Dkt Boganza. Lissu kafanya vema sana kusema ukweli & uwazi wa kilicho zungumzwa! La sivyo wachawi wasingekawia kumtungia stories za kusaliti au kusalimu amri!
Nadhani angekuwa Denis fake, vijana wake wa mafunzo akina Adamoo wasinge kalia kimya jambo hilo. Discrepancies kwenye maelezo yake pengine zina thibitisha mashaka ya wengi kwamba alitiwa kibano cha kutosha alipokubali ku compromise akalishwa hiyo script iliyo andaliwa na kina Kingai.
Kina...
Kazi ya kusimamia mawaziri ni ya PM - Kassimu akae mkao wa kunyolewa! Bunge likishapata Spika, hiyo kazi ya Lukuvi ya usimamizi wa mawaziri inaanza rasmi kwa jina lake kupelekwa Bungeni kuthibitishwa!!!
Vyama vya siasa kufanya siasa (including mikutano ya hadhara) hakuvunji sheria wala Katiba. Kuvizuia vyama vya siasa kufanya siasa ndio kuvunja Katiba ya nchi na hapo hakuhitajiki mjadala wa msajili & polisi bali kufanya rejea kwenye vipengele husika vya Katiba kwa utekelezaji katika ngazi zote...
Hivi kulazimisha ujenzi wa bwawa la Stiegler's Gorge, miti milioni ngapi tena vile ilikatwa? Na hilo likafanyika kwa ubabe mkubwa licha ya taarifa lukuki za ongezeko kubwa la hewa ya ukaa duniani!!!! Tukiitwa "shithole country" tunavimba kama vifutu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.