Mangi Sina wa Kibosho (aliyeshika bunduki katikati ya maaskari wake). Picha ilipigwa mwaka 1894. Alifariki miaka 4 baadaye. Wageni waliomtembelea kwenye himaya yake walisimulia kama mtu aliyekuwa hodari na shujaa na alionekana mstaarabu na mpole (kama anavyoonekana kwenye picha) lakini alikuwa...
Ukichunguza historia ni vigumu kuona ni wapi machame imekuwa na mgogoro wa kihistoria na wamarangu. Machame ilipata matatizo na kibosho miaka ya mwisho ya 1880 ambapo Mangi Sina, mtawala wa Kibosho (ambaye yeye mwenyewe alikulia Machame) aliunda zengwe na kuuwa wamachame kadhaa kule Kibosho na...
Wameru (kwa asili waliitwa waarwa) walihamia kwenye miteremko ya mlima Meru katika karne ya 15/16. Kwa asili walitokana na mababu wawili walioitwa Kaaya (aliyekuja kuwa kiongozi wa kabila au Mangi) na Mbise ambao walizaliwa na kiongozi aliyeitwa Lemireny (aliyekuwa msoma nyakati, mbashiri, na...
Mangi Gilead Abdiel Shangali alikuwa ni mangi wa mwisho kabisa kuwa hai kule uchagani miongoni mwa walioteuliwa kuwa watawala wa jadi nyakati za ukoloni. Wengine wote walishafariki. Mangi Gilead (kama alivyojulikana sana wakati wa uhai wake) alitawazwa rasmi kuwa mangi wa Machame mwaka 1952 kwa...
Unajua mwanakijiji lazima msimamizi wa uchaguzi aulize kwanza wakuu wa serikali kama atangaze hayo matokeo au nini kifanyike? Mpaka wamwambie sawa ndipo atayatangaza kama yalivyo au vinginevyo itabidi kura za Nassari apewe Sioi na za Sioi atangaziwe Nassari. CCM ndiyo imeshika hatamu, au hujui hilo?
Kwanza ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mr Mushi kwa kuwa kisababishi cha kuanza mada hii ambayo imeleta na mengi katika kujifunza juu ya historia ya uchagani. Kutokuridhika kwako hukukaa kimya na kunung'unikia vitandani kama watanzania wengi walivyo, bali uliamua kutoa dukuduku lako ili...
Snochet,
Sifahamu ni mgogoro gani huo unaouzungumzia labda utoe ufafanuzi. Kuhusu kitabu cha Kilimanjaro and its peoples, sina uhakika una maana gani kitamaliza mgogoro wakati hujakisoma bado. Vitabu vyote vilivyotajwa humu jamvini vitaweza kukusaidia kupata mwanga wa historia ya uchagani, hata...
Hapana. Hii siyo story ya kweli. Nakubali kwamba kuna masimulizi mengi mengi tu yanayotaka kuelezea kilichotokea kwenye mauaji yale ya wamachame kule Kibosho. Kwa mfano, ukienda Moshi utasikia wanasema kwamba wamachame walipatwa na mtego kule Kibosho kwa sababu wanapenda sana kula. Kwa hiyo...
Nadhani Makupa unaweza kuwa na ukweli fulani unaoueleza. Hata hivyo sidhani kama huo ni aina ya ukweli ambao utamuuma mtu kwa sababu nadhani jamvini hapa watu wanaweza kuwa na mdahalo kwa nia ya kuelimishana na siyo katika mtindo wa kupashana ambapo ndipo mtu anaweza kudhani amedhiliwa. Kuna...
Uronu,
Kuhusu tofauti tofauti zilizopo kati ya wachaga nadhani unaweza kusoma utangulizi kwenye hii website itakupa mwanga ingawa kidogo: Machame - Wikipedia, the free encyclopedia.
Juu ya koo za Machame ni vigumu sana kujua leo hii kutokana na kuongezeka kwa watu na wengine kutumia majina...
Ninakiri kwamba kuna hizi habari watu wanazizungumzia, lakini ni vigumu kuzithibitisha. Zinaonekana kama ni uvumi hivi kwa kiasi kikubwa. Ujasiri wa wanawake wa kimachame umekuwa mara kwa mara ukihusianishwa na mauaji yale yaliyotokea miaka ile ya 1886 ambapo wanaume kadha wa kadha wa kimachame...
Ni kweli. Wamachame wengi waliona wamesalitiwa na mangi Sina wa Kibosho. Ingawa alishaonekana kuwa na shari lakini hawakutegemea hali ingefikia kuwa mbaya hivyo. Ndiyo maana walipoambiwa amefariki wengi walikwenda ili kumzika mtu wao waliomfahamu siku nyingi. Walikwenda majemedari wa vita na...
Ni kweli Kithuku. Ukifahamu historia za huko tulikotoka utashangaa sana hasa kwa wachaga. Harakati za kisiasa uchagani zilianza miaka mingi sana siyo jana au juzi kama tunavyofahamu katika historia ya nchi hii ya Tanzania. Ukumbuke pia kwamba, wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961 tayari...
Naona nisimulie kwa ufupi historia ya mangi Sina wa Kibosho kwa ajili ya msaada wa baadhi ya watu kwenye forum hii. Ukweli ni kwamba Sina halikuwa jina lake la asili alilopewa na wazazi wake. Kwa wale watakaotaka taarifa zaidi waniandikie kwenye email yangu hapo chini, ila hapa nitasema...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.