Habari za Leo!! Kuna ndugu humu aliwahi kuandika kuwa yupo Dodona na anaweza kusaidia kupeleka barua kwenye Wizara mbalimbali.
Nimejaribu kuutafuta ule Uzi wake siuoni na sikumbuki vizuri kichwa cha habari. Kama anasoma Uzi huu naomba mawasiliano yake.
Shukurani.
Habari wana jukwaa, ndugu zangu nipo Morogoro nina ukwaju mwingi, kama kuna mtu anajua soko lilipo au aniunganishe na masoko. Natanguliza shukrani zangu[emoji120][emoji120][emoji120] Namba zangu za simu-0627912202
Habari za leo wadau!
Naomba msaada , gari yangu aina ya Wish taa ya oil inawaka moja kwa moja. Imeshabadilishwa vitu vingi hadi fundi kanyoosha mikono.
Naomba wajuzi mnisaidie ifanyiwe nini tena?
Habari za leo wanajamvi!! Wakulima wa mpunga dakawa-Morogoro, Wana kilio!! Wafugaji wanaingiza mifugo mashambani kwa jeuri, wakulima hawana cha kufanya!! Ukikamata ng'ombe upeleke polisi, mwenyewe hatokei wanasubiri giza wanawaswaga na kuondoka nao.
Kuna kipindi kwa ustaarabu kabisaa walikaa...
Habari waungwana. Kilimo cha mahindi kwa takribani miaka 3 sasa hapa nchini kwetu kimevamiwa na viwavi wanaoshambulia shina na kuathiri mavuno kabisaa. Hali hii imesababisha matumizi ya madawa makali na gharama kuubwa sana kwa wakulima. Lipo suluhisho la kustawisha mahindi bila kutumia kemikali...
Habari za leo wanajukwaa!! Nimepita maeneo ya Morogoro stendi ya haisi mjini, kwa kweli Kuna changamoto kuubwa!! Bajaji na pikipiki zimeziba kabisaa barabara iendayo kwa mkuu wa Mkoa!! Wanapaki katikati ya barabara na wajeuri!! Naomba kwa heshima kabisaa mamlaka husika ishughulikie hili!! Pale...
Habari zenu!! Nahitaji msaada kama kichwa Cha mada kinavyojieleza!! Nataka kutengeneza vifungashio Kama njia ya ujasiriamali. Naomba anaefahamu sehemu ninayoweza kupata anisaidie!!
Natanguliza shukrani¡
Wandugu naomba mnisaidie kutoa ushuhuda hapa kwa aliewahi kutumia hizo mbolea hapo juu. Mimi nimetumia kwenye mahindi ni wiki ya 3 sasa sioni mabadiliko ninachokiona ni mahindi yanazidi kuwa njaanooo¡!
Kwa yeyote mwenye tatizo la kisukari au kumjua mtu mwenye kisukari awasaliane na namba hii 0716439433 . Imemsaidia saana ndugu yangu alikuwa akatwe mguu lakini amepona kabisaa!! KIZURI KULA NA WENZIOO!!
Habari za jioni wanajukwaa! Nahitaji kujuzwa kuhusu sheria hii: Abiria anaekaa kiti cha nyuma baada ya siti za mbele ni lazima afunge mkanda?? Maana nimekutana na utata leo jioni, kuna trafiki alinisimamisha abiria wangu wa nyuma hakuwa amefunga mkanda, kwa jazba kachukua leseni na kadi kapeleka...
Ndugu wanajamvi naomba msaada wa ushauri jinsi ya kumshauri shemeji yangu mke wa rafiki yangu! Nina rafiki yangu wa siku nyingi nahisi anakaribia miaka hamsini sasa (50), ana mke mzuri sana anaejiheshimu na muwajibikaji. Ila huyu rafiki yangu ana matatizo jamani sio mwaminifu kabisa hata kidogo...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.