Kuna urasimu mkubwa sana kwenye ofisi za NSSF Mwanza ukilinganisha na mikoa mingine, bila kuwa na ndugu au jamaa anayekujua faili lako la mafao linaweza kuzungushwa hata mwaka mzima.
Mimi na wafanyakazi wezangu tuliacha kazi siku moja kwenye kampuni binafsi mimi nikiwa branch ya Mwanza...
Dkt.Benson Bagonza Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe alikuwa akihojiwa na Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu ambaye alimuuliza " Baba Askofu ningependa nikuulize, wewe umekuwa ukitoa mawazo yako hadharani juu ya masuala ya kisiasa huwa hakuna 'contradiction' kwamba unaingiza labda Siasa ndani...
Ibara ya 47 ya Katiba inasema, kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.
Sasa nashangaa hata barua tu ya uteuzi hadi isainiwe na Rais mwenyewe tena nje ya nchi, kuna ulazima gani wa Rais kusaini nje ya nchi, kama kazi ndogo kama...
Maridhiano yalitaka kuwatoa kwenye reli ila kwa sasa naona mmerudi kwenye mstari wenu ulionyooka, tunaiona Chadema tuliyoizoea.
Hotuba ya jana imedhihirisha hilo, ni hotuba iliyojaa hofu iliyochanganyikana na hasira. Ametumia muda mwingi kuizungumzia Chadema kuliko kilichompeleka, ilionekana...
Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Kuhusu Katiba Mpya tunaanza na Elimu Watanzania waijue, unaanzaje kumwambia Mtu akupe maoni yake kitu hakijui. Viongozi wa Kisiasa tunadhani tuna Haki ya kuburuza Watu, tunachokisema sisi Watu wote wafuate, tunageuza Watu makasuku”.
Kamati ya Warioba ilizunguka...
Moto wa petroli una tabia kuu moja, unapoumwagia maji ili kuuzima unaibukia pembeni tena kwa nguvu zaidi ya ule wa mwanzo tena una tabia ya kulipuka.
Deusdedith Soka kijana aliyeandamana kupinga mkataba wa DPW jana kachomewa nyumba yake na watu wasiojulikana, Mdude, Mwambukusi na Dr. Slaa...
Wakati wa utawala wa Magufuli madhehebu ya dini ya Kikristo yalipoona uminywaji wa demokrasia na uhuru wa kujieleza, kupotea kwa watu uliokuwa ukifanywa na serikali, hayakukaa kimya yalitoa Nyaraka mbali mbali kumuonya Rais Magufuli na serikali yake.
Lilianza Baraza la Maaskofu wa kanisa la...
Kama ni kusali nenda kasali ukipewa nafasi ya kusalimia waumini toa fungu la biblia au msitari wa Quran lkn ukianza kuongelea siasa au kuwananga wanasiasa kwenye kibweta na wewe unaingiza siasa kanisani. Nyerere kila Jumapili alikuwa anahudhuria misa St. Peter’s lkn ilikuwa nadra sana kupanda...
Enzi za utawala wa Mwinyi miaka ya 80, mwanasiasa machachari Joseph Mtikila alikuwa akimuita Rais Mwinyi ni ‘TX’ kutoka Zanzibar na aliwahi kumwambia arudi mwenyewe Zanzibar kabla hajarudishwa kwenye jeneza, hii ilikuwa kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Jangwani kwa waliokuwepo wakati huo...
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema.
Pamoja na serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kupongezwa na wadau mbali mbali wa haki za binadamu katika maeneo mengi ikiwemo kutoa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni uhuru, sakata la...
Sielewi kwa nini hadi sasa jeshi la polisi halijachukua hatua zozote zile kuhusiana na kitendo cha kiharifu cha wale Vijana, sijui ni kwanini Msajili wa Vyama vya Siasa hajakemea, na sijui ni kwa nini Viongozi wa Dini hawajajitokeza kukemea.
Wako wapi wanaojiita viongozi wa vyama walinda amani...
Kabla ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964, Zanzibar pamoja na korido lote (km 10) la mwambao wa Pwani ya Afrika Mashariki vikijumuisha visiwa vya Lamu na Mafia vilitawaliwa na Ukoo wa Sultan Sayyid wa Oman.
Sultan aliitawala Zanzibar na mwambao wote kuanzia Tanga hadi Lindi, korido lote toka...
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu akiwa Mkoani Kagera, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, amemjibu Kinana aliyewatuhumu Viongozi waandamizi wa CHADEMA kukosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hasani aliyewafutia kesi.
Lissu amesema, hawawezi kushukuru kwa kufutiwa kesi za uwongo...
Tarehe 24/10/2007 Balozi Dr. W.P. Slaa, akiwa viwanja vya Mwembeyanga Temeke alitaja majina 11 akiwemo Rais mstaafu Mkapa na Rais aliyekuwa madarakani Mh Kikwete kuwa ni miongoni mwa Mafisadi wa nchi.
Akiongea na waandishi wa habari kwenye hotel ya Regency 13 June, Slaa alisema,
“Waliohudhuria...
Siasa za mivutano ‘Confrontational Politics’ aliziweza Mwendazake, sidhani kama Rais Samia ataziweza.
Samia alikuja na hoja ya ‘Maridhiano’, hoja ambayo ilipokelewa vizuri na pande zote ingawa kwa shingo upande, baadhi hawakufurahishwa.
Kwa kiasi kikubwa siasa za vyama vya Upinzani hasa...
Imetokea kwa bahati mbaya au ilikuwa imepangwa na waarabu DP World kwa ujanja wao au ni uvivu wa wanasheria wetu kusoma kilichoandikwa kwa makini, na ni nani hasa aliandaa andiko hili. —-AND—.
.
Barua hiyo ya wito kutoka ofisi ya DCI inamtaka Dkt. Nshala kufika kwa ajili ya mahojiano
Ofisi hii inafanya uchunguzi kuhusiana na kauli ulizotoa tarehe 03 Julai 2023 na kisha kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na mkataba wa uwekezaji katika...
Tumewahi kuona mikataba mikubwa ya kuuza au kubinafsisha raslimali zetu ikisainiwa kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali lkn huu wa kuuza bandari zetu unaoneka kuwa utavunja rekodi ya kuwa mkataba mbovu kuwahi kusainiwa na rais aliye madarakani na utamwachia legacy mbaya Rais Samia.
Tukiondoa...
Mara nyingi tumekuwa tukiwaona hawa vijana wakijitokeza haraka kutetea au kufanya maandamano kupongeza kunapotokea sintofahamu hasa yanapoguswa maslahi ya serikali ya CCM na viongozi wao wakuu, lakini tofauti na sasa ukitoa tamko la Mwenyekiti wao Kawaida sijawasikia au kuwaona wakiandamana mkoa...
Nimemsikia Mbunge Lucy Mayenga akiwaomba wabunge wenzake watafakari upya kuhusu mkataba wa DP World.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema hawatapuuza maoni ya wananchi wanayotoa kuhusu huo mkataba.
Hii tafsiri yake nini, ni kuwa Wabunge na WM wamegundua kosa lao, kuwa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.