Search results

  1. kmdh

    Akipita mzungu karibu na uzio wa Ikulu hana kosa, ila apite mtu mweusi ni kosa na mateso juu

    Watanzania tunawaona wazungu ni miungu watu. Mfano mtu mweusi ukienda kushtaki polisi unazungushwa, lakini mzungu akienda kushtaki mara moja wanafuatilia. Hata pale airport, mimi sijawahi kuona mzungu anakaguliwa.
  2. kmdh

    Vijana Wasomi Wapewa Changamoto ya Kujiajiri Badala ya Kusubiria Kuajiriwa!

    Kusema wasomi wajiajiri ni ukwepaji wa majukumu wa serikali tuu. Serikali kazi yake ni kuinua uchumi ambao unaleta ajira kwa wananchi. Kama serikali kazi ya kuinua uchumi na kuleta ajira imewashinda, wawape hayo majukumu wengine.
  3. kmdh

    Vikosi maalumu 16 bora na hatarishi zaidi duniani, Tanzania ni ya tatu!

    Huko si wako kama walinda amani (peacekeepers)? Kupigana vita na kulinda amani ni vitu viwili tofauti bro.
  4. kmdh

    Utamaduni wa wanaume kupiga wanawake umepitwa na wakati

    Habarini wakuu Huyu dada hata kama ametembea nje ya ndoa, kupigwa kama mnyama ni haki kweli. Hii imekuwa ni tabia ya baadhi ya wanaume wengi kuwapiga wanawake wao kama wanapiga ngoma. Tazama video hiyo namna mwanaume anavyompiga mwanamke kama anaua nyoka.Mi ninavyoona utamaduni wa mwanume...
  5. kmdh

    Mchina atembeza kipigo Songea na kujeruhi wawili

    Kumpiga kofi mwanaume mwenzako ni kumdhalilisha sana. Watoto wadogo na wanawake ndiyo wanapigwa makofi siyo wanaume. Wanaume lege lege nchi hii. Ndiyo maana vigogo wanafanya wanalotaka kwa sababu wanajua fika sisi tumelegea.
  6. kmdh

    Bimkubwa agoma kurudi Africa, kisa mfumo wa maisha mbovu

    Asilimia kubwa ya utajiri wa nchi hii umeshikiliwa na wachache sana yaani ni chini ya 1%. Hao ndiyo wamefaidika na uchumi ulivyopanda. Wengine wengi maisha yao yamerudi nyuma au hayajabadilika sana. Na huko tunakoelekea maisha ya wengi yataendelea kuwa duni maana viongozi wetu hawana sera za...
  7. kmdh

    JWTZ na Jeshi la China wakiwa katika mafunzo ya kijeshi, Kigamboni Dar es salaam

    Usijidanganye mkuu. Kama polisi na FFU wakishindwa kuzima ghasia za siasa, jeshi litaitwa. Sisi hatuko nchi zilizokamaa kidemokrasia ambazo unaweza kusema watawala wetu hawatavuka mipaka ya kutumia jeshi kuzima ghasia.
  8. kmdh

    JWTZ na Jeshi la China wakiwa katika mafunzo ya kijeshi, Kigamboni Dar es salaam

    Mkuu ulifuatilia yaliyotokea kule Misri? Uliona jinsi jeshi lao lilivyozima ghasia za siasa?
  9. kmdh

    JWTZ na Jeshi la China wakiwa katika mafunzo ya kijeshi, Kigamboni Dar es salaam

    Haya si mafunzo ya vita, haya ni mafunzo ya kuzima ghasia za siasa. Na ndiyo maana yanaonyeshwa kwenye vyombo vya habari ili myaone.
  10. kmdh

    Waafrika wapata kichapo India, mnaoenda India kwa matibabu kuweni makini

    "My body, whenever I see a black person in the metro, tenses with anxiety,” the blogger wrote. “Like seeing kids playing near traffic, I fear for them.” Source...
  11. kmdh

    Mungu nisaidie nisipate mtoto wa kike

    Nimekupata lakini kuna vitu tuna assume ni common knowledge ndiyo maana sijaandika. Mfano kama mwanamke hayuko kwenye siku zake za ovulation hapati mimba. Cha muhimu ni hizo mbinu nilizoandika zina mafanikio kwangu mimi binafsi na kwa wengine wengi waliozitumia.
  12. kmdh

    Mungu nisaidie nisipate mtoto wa kike

    Hebu highlight hapo nilipoandika mwanamke anaweza kupata mimba siku zote.
  13. kmdh

    Mungu nisaidie nisipate mtoto wa kike

    Ukitaka kupata mtoto wa kiume kuna mbinu lazima utumie. Hakikisha mwanamke anafika kileleni wakati wa tendo la ndoa. Sababu ni kwamba mbegu za kiume (Y chromosome) zinaogelea kwa kasi kuliko mbegu za kike (X chromosome) lakini mbegu za kiume zinakufa mapema. Kwa hiyo mwanamke akifika kileleni...
  14. kmdh

    Mungu nisaidie nisipate mtoto wa kike

    Faida ya mtoto wa kiume ni kuendeleza ukoo wenu. Watoto wa kike wanaolewa na wanaendeleza ukoo wa waume zao ndiyo maana ni muhimu kupata watoto wa kiume. Kuhusu ni mtoto yupi atakusaidia, hayo yanategemea na malezi. Kama mtoto wako wa kiume umemlea vizuri, atakusaidia sana tuu.
  15. kmdh

    Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

    Sasa kodi zao si ndiyo zinaletwa huku kwetu kupitia NGO's, benki ya dunia, umoja wa mataifa n.k.? Pamoja na kwamba tunawakejeli hawa wabeba maboksi, lakini kodi wanazolipa huko wanapoishi zinatusitiri.
  16. kmdh

    Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

    Sheria hiyo imepitwa na wakati na ni ya kuvunjwa kama haitabadilishwa. Haiendani na dunia ya karne ya 21.
  17. kmdh

    Wapalestina washerehekea ushindi

    Kama Israel ingeshinda, Hamas wasingebakia pamoja na silaha zao. Na jinsi Israel ilivyouwa raia wa Palestine ambao hawana hatia, imejishushia sana hadhi.
  18. kmdh

    Watanganyika mnatuharibia Zanzibar

    Huu mjadala umenivunja mbavu. Ha ha ha.
  19. kmdh

    Niko kwenye Jeshi la akiba la wanajeshi wa Tanzania, Utaninyimaje haki ya uraia EX-POLICE wako?

    Hata mimi najiuliza hawa wanaosema watu wa diaspora siyo wazalendo, walikuwa wapi wakati nchi inauzwa kwa manufaa ya wachache? Kama kweli nchi hii ingekuwa na wazalendo tusingeburuzwa kiasi hiki. Ni kelele tuu za mitandaoni naona au inawezekana ni wale wale mafisadi wanaogopa competition. Teh...
  20. kmdh

    Niko kwenye Jeshi la akiba la wanajeshi wa Tanzania, Utaninyimaje haki ya uraia EX-POLICE wako?

    Tuacheni unafiki. Hata sisi hapa mjini siyo kwetu. Wazazi wetu walikimbilia mjini kutafuta maisha. Kama wa diaspora ni wasaliti, basi hata sisi ambao hatuna asili za kizaramo hapa mjini pia ni wasaliti. Maana tumeikimbia mikoa yetu na vijiji vyetu na tusiitwe tena wachaga, wanyakyusa, wahaya n.k.
Back
Top Bottom