Hili Jimbo lilichukuliwa na Esther Bulaya baada ya wananchi kumkataa Steven Wassira. Sasa tangu achaguliwe hadi leo hii hata haeleweki na hatujui kuwa yako wapi maana tangu bunge limeisha wabunge wengine tunawaona majimboni mwao lakini huyu wa kwetu hatumuoni. Je, tulimchagua ili apate nafasi ya...
Wadau wenzangu sheria inasema kuwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wasibebe mishikaki na badala yake wabebe abiria mmoja lakini naona kama sheria hii haisimamiwi vizuri na wahusika kama ilivyoaagizwa.
Mfano angalia huyu hapa,.
Wadau wenzangu sheria inazungumziaje hili maana kuna watu wanaweka mziki au kwaya kwa sauti ya juu sana katikati ya miji ya watu hata kama kuna yowe sehemu ya uhalifu hamuwezi kusikia. Hili limekaa vipi maana inakera sana wengine hatupati usingizi.
Hapa Bunda sukari imepanda bei toka 60,000 hadi 70,000 kwa mfuko wa kilo 25 kwa bei ya jumla ambapo kilo ni sh. 2800 lakini rejareja wanauza sh. 4,000 hadi 5,000. Cheki hii hapa.
polisi wetu hawana mapokezi mazuri kwa raia.
Leo nilikuwa kituo cha polisi nikamsikia polisi mmoja wa kike mwenye namba WP 6010 akimjibu vibaya raia aliyeenda kutoa taarifa kuhusu jambo alikokuwa nalo hata kufikia hatua ya kumwambia kuwa yeye hajamwajiri.
Kitendo hicho kilinisikitisha sana na...
Magari madogo maarufu kama hiace yanabeba watu kwa kubananisha ndani ya gari halafu juu ya bodi wanajaza mizigo kama mnavyoona hapa.
Je, askari wetu wa usalama barabarani hawaoni,? Ajali ikitokea ndipo sababu zitakuwa nyingi Wakati wanakuwa wanawaona tu. Hapa kuna majipu yaliyoiva.
Nasikitika sana kuona wafanyabiashara kuuza vitu vilivyokwisha mda wa matumizi( Expire date).
Sijui wanauza bila kujua ama wanajua lakini wanauza tu kwa kuwa hawajawahi kuona kama kuna ufuatiliaji wowote?
Serikali itazame hadi mikoani kubaini tatizo hili maana wengi wataumia.
Vitu hivyo...
Mkuu wa wilaya ya Bunda Mh. Joshua Mirumbe awa mbogo kwa Polisi katika kikao kilichofanyika hapa Bunda katika mtaa wa Mapinduzi kujadili wizi wa kutumia silaha za moto unaotokea mara kwa mara katika mji huu.
Wananchi waliilalimikia jeshi la Polisi kutofika kwenye tukio kwa wakati licha ya...
Majambazi wamevamia duka la Muuza simu usiku wa saa tisa na kupora Simu zote na pesa katika eneo la genge la jioni.
Kabla ya tukio hilo wakawa wamepiga risasi Nyasura mbugani mwendo wa saa nne usiku.
Baada ya tukio walipiga risasi zaidi ya 10 na Polisi hawakuweza kujitokeza kujibu mashambuzi...
Mwaka huu mvua inanyesha kama miaka ya zamani maana kila siku ni mvua hakuna kupimzika.
Madhara yametokea mengi sana kiasi kwamba hata mazao yanapata shida sana kwa kulemewa na maji.
Je, kwingineko vipi?
Majambazi wamevamia hapa Bunda mjini katika stendi ya zamani majira ya saa mbili kasoro usiku na kupora katika maduka pamoja na kuua Muuza vitumbua baada ya kupiga yowe.
Katika tukio hilio lilitokea mapema tena umbali wa kama mita 600 kutoka kituo cha Polisi wilaya lakini Polisi hawakuweza...
TRA imesema kuwa mwisho wa usajili wa pikipiki hizo kwa hiari unaelekea ukingoni. Hivyo basi, amewaomba ambao hawajasajili wafanye hivyo mapema ili kuepukana na usumbufu wanaoweza kukumbana nao.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.