Hiyo ndio Tanzania bwana. Mipango mingi ya kuvutia lakini utekelezaji zero. Ati sasa ndio wanatafuta fedha za kununua mafuta mazito kwa ajili ya kuendesha mitambo ya IPTL walikuwa wapi wakati wote? Yaani kaaazi kweli kweli.
Mheshimiwa Solar Power Je, huo usafiri wa umma uko wapi? Ni huu wa watu kusubiri saa kadhaa vituoni bila kujua watafika lini kazini au kurudi makwao saa ngapi? Je, ni huu usafiri ambao watu hupitia madirishani badala ya milangoni ili kuwahi siti? Kama ni huu basi wazo lako haliwezi kutekelezeka...
Halafu kuondoa yale mambo ya msingi katika rasimu hiyo ya katiba kama mamlaka ya Rais, uwepo wa serikali ya mapinduzi ZNZ, Uwepo na au muundo wa muungano na muundo wa serikali n.k ili yasijadiliwe ama kutolewa maoni na wananchi maana yake nini? Si afadhali wangekaa huko huko serikalini...
Hivi wadau Arsenal tuna mkosi gani? mbona mechi za muhimu na za kugangamala tunafungwa au tumejitahidi sana sare? Mfano ni mechi ya leo na Birmingham city yaani tunafungwa dakika za majeruhi! Kwa kweli inavunja moyo sana.
Mhe. Rungu naungana kabisa na tasia I na Shakazulu. Unafikiri kama lingekuwa timbwili kweli hiyo kanga au hiyo bukta ingekaa mahali pake kama hivyo? Yaani hata miguu yao ni misafi kabisa. Kweli hawa wanajifurahisha tu.
Mhe. Mwanakiiji mimi ninakubaliana kabisa na mawazo yako kuhusu muundo uliopendekeza wa serikali kwa kweli umekaa vizuri sana. Kama kweli tunaweza kuweka muundo huu halafu huko mbeleni kutokana na jinsi utakavyofanya kazi na matunda kuanza kuonekana basi tunaangalia tena jinsi ya kuuboresha ili...
Kwanza mhe. huna taarifa sahihi. Ile ofisi ya Urambo Mashariki si ya Spika ni ofisi ya mbunge yeyote ambaye atachaguliwa na wananchi kuwatumikia wana Urambo hata wa chama kingine. Ni mpango mahsusi wa serikali kujenga ofisi za wabunge zenye hadhi kama ile katika majimbo yote ya uchaguzi likiwemo...
Hiyo ndio CCM chama ambacho kimesahau kuangalia na kusimamia maslahi ya wengi (wananchi) na kukumbatia maslahi ya watu wachache au kikundi cha watu. Kwa mtazamo wangu maamuzi kama haya ndio yaliuwa vyama vingine vya ukombozi Afrika kama KANU-Kenya na UNIP-Zambia na CCM wanaelekea huko huko...
Inaelekea hiki chama bado kina wadharau wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi ambao hawawezi kuhudhuria kampeni za chama hicho kwani kwa muda wa kampeni wanakuwa vibaruani mwao. Zaidi ya hayo inaelekea kuwa hiki chama kimekuwa na zile kampeni za kijima hivi hawaoni nchi zilizoendelea...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.